Qiuhe, Japani
Nilizaliwa katika familia ya Kikatoliki. Tangu nilipokuwa mdogo, nilihudhuria Misa kanisani na babu na bibi yangu. Kutokana na ushawishi wa mazingira yangu na imani yangu kwa Mungu, nilijifunza kuimba maandiko mengi tofauti na kufanya kaida mbalimbali za dini.
Mnamo 2009, niliwasili Japani ili kusoma. Wakati mmoja, katika chumba cha bweni cha mwanafunzi mwenzangu, kwa bahati nilikutana na kiongozi wa kikundi kidogo cha Kikristo aliyekuja kueneza injili. Nilifikiri: Waprotestanti na Wakatoliki humwamini Mungu mmoja. Wote wawili huamini katika Bwana Yesu. Matokeo yake, nilikubali mwaliko wa kiongozi huyo wa kundi ndogo kujiunga naye kanisani. Baada ya kusikiliza wachungaji wakihubiri na kusikia baadhi ya ndugu wa kiume na wa kike wakizungumza juu ya Biblia, nilipata ufahamu fulani juu ya maisha ya Bwana Yesu. Hili lilinisababisha niwe na imani zaidi katika Bwana. Hata hivyo, baada ya miezi michache, wachungaji na wahubiri walituomba kutoa zaka kila wiki. Pia, kila juma, tulipaswa kupeana vijitabu ili kueneza injili. Wakati mwingine, tulikuwa tumechoka kiasi kwamba tungesinzia wakati wa ibada ya Jumapili. Hatukuwa tena na utaratibu wa kawaida katika maisha yetu. Wakati huo, baadhi yetu tulifanya kazi na pia kusoma. Haikutubidi tu kutafuta pesa za kulipia masomo yetu, lakini pia tulihitaji fedha za gharama zetu za kila siku. Maisha yetu yalikuwa ni magumu sana tayari, lakini bado walitaka tuwape fedha zetu na nguvu zetu. Tulikuwa tunakabiliwa na shida nyingi sana na maumivu. Hatua kwa hatua, niligundua kwamba wachungaji na wahubiri hawakuwa kwa kweli watu waliomtumikia Bwana. Kwa kawaida, kwa kuwa walikuwa ndio wale ambao waliliongoza kanisa, wangepaswa kuwa wakitusaidia kukua katika maisha yetu ya kiroho. Hata hivyo, hawakuyajali maisha yetu. Hawakufikiria kabisa kuhusu matatizo yetu ya kivitendo. Badala yake, walitaka nguvu zetu na pesa zetu. Kila kitu walichokifanya kilikuwa ni cha kusaidia kupanua kanisa lao na kuimarisha hali zao na ushawishi wao. Kwa wakati huu, tulihisi kama tulikuwa tumedanganywa. Kwa hivyo, ndugu zangu kadhaa na mimi tuliliacha kanisa.
Baada ya kuacha kanisa, nilipata kanisa moja Katoliki ambalo lilikuwa juu ya mlima. Watu katika kanisa hili walikuwa Wajapani Nilihudhuria Misa mara chache lakini nilihisi kuwa halikunifaidi kiroho. Zaidi ya hayo, ilikuwa vigumu kuhudhuria ushirika, kwa hiyo nililiacha kanisa hilo pia. Kwa njia hii, niliongoza maisha ya kuchanganyikiwa na ya utupu bila ya mwelekeo na hisia ya kusudi. ... Hili ilitokea kwa dhati mpaka Oktoba, 2016. Dada Liang, niliyekutana naye katika kanisa la Kiprotestanti katika siku za nyuma, kwa ghafla akawasiliana nami, akaniuliza jinsi nilivyokuwa na kunialika kumwona. Nikafikiri jinsi uzoefu wangu na kanisa la Kiprotestanti ulivyokuwa wa kusikitisha katika mwaka huo mmoja na matokeo yake, niliukataa mwaliko wa Dada Liang. Hata hivyo, Dada Liang alinialika tena na tena na kwa sababu ya heshima ya hisia zake, nikaamua kukutana naye.
Kupitia kwa Dada Liang, nilikutana na Dada Ma na Dada Fang. Siku moja, walizungumza nami kuhusu unabii mwingi wa Biblia. Waliniambia juu ya kazi ya Yehova Mungu na Bwana Yesu. Ufahamu wao ulikuwa mbichi sana na walizungumza kuhusu mambo ambayo sikuwahi kusikia kabla. Niliwaambia kuhusu hali ya giza niliyoishuhudia kanisani na jinsi nilivyokuwa nimevunjika moyo sana kwa kutoweza kwangu kupata chakula cha kiroho kutoka kwa kanisa na kwamba sikuwa radhi tena kuhudhuria mikutano. Dada Fang akasema: Tumeyapitia pia uliyoyapitia. Kwa sasa, dunia nzima ya kidini iko katika hali ya giza na ukiwa. Ndani ya hili, kuna makusudi ya Mungu na ukweli wa kutafuta. Kwa sasa, tuko katika nyakati za mwisho za dunia. Bwana Yesu alitabiri: “Na kwa sababu uovu utaongezeka, upendo wa wengi utapoa” (Mathayo 24:12). Uovu umeenea zaidi na zaidi katika ulimwengu wa kidini siku hizi. Wachungaji na wazee wa kanisa hawafuati mafundisho ya Bwana na hawatii amri Zake. Wao huhubiri tu na kufanya kazi kwa hadhi yao. Wao daima hujikuza na kujishuhudia wenyewe ili watu wengine watawaheshimu na kuwaabudu. Wanafanya watu wengine watoe mchango na kueneza injili. Kwa maneno tu, wao husema kusudi lao ni kuziokoa roho za watu, lakini kwa kweli, hawawaongozi watu kupitia maneno ya Bwana wala kuwasaidia watu kuweka maneno ya Bwana katika vitendo. Wao hutaka tu watu wengine kuwasikiliza. Wana uchu wa kuwafanya watu wengine wawachukue kama Mungu. Kale walianza kutembea kwenye njia ya mpinga Kristo ambayo ni ya uhasama kwa Mungu. Wamepoteza kazi ya Roho Mtakatifu na wametelekezwa na Mungu. Fikiria nyuma kwa kipindi cha nyuma wakati wa Enzi ya Sheria wakati hekalu lilikuwa limetelekezwa na lilikuwa limekuwa pango la wanyang'anyi. Makuhani walitoa sadaka duni wakati watu wa kawaida walibadilisha pesa na kuuza ng'ombe, kondoo na njiwa ndani ya hekalu. Lakini kuadibu kwa Mungu na adhabu hazikuwaangukia. Mbona hivi? Wakuu wa makuhani, waandishi na Mafarisayo waliomhudumia Mungu hawakuitii sheria, walikuwa na unafiki na waliwadanganya watu, na waliwaelekeza wateule wa Mungu kwenye njia ya kumpinga Mungu. Hili lilimsababisha Mungu kuwachukia na kuwakataa na hekalu likapoteza kazi ya Roho Mtakatifu na kuwa pango la wanyang'anyi. Ili kuwaokoa watu kuepuka kuhukumiwa kifo kwa sheria, Mungu alikuwa mwili kwa mara ya kwanza, Akafanya kazi ya ukombozi kwa jina la Yesu, Akaanza Enzi ya Neema na kuhitimisha Enzi ya Sheria. Kazi ya Roho Mtakatifu kwa hiyo ikawasogea watu waliomkubali Bwana Yesu. Hekalu halikuwa na kazi ya Roho Mtakatifu tena. Katika wakati wa leo, Bwana Yesu amerudi kama ilivyotabiriwa. Amekuja tena katika mwili. Yeye ni Mwenyezi Mungu, Kristo katika siku za mwisho na ameanza kuonyesha ukweli na kufanya kazi ya hukumu kuanzia na familia ya Mungu. Kazi ya Roho Mtakatifu imesogea kwa wale ambao wameikubali kazi ya Mungu ya siku za mwisho. Kwa kuwa dunia ya dini haijaenda sambamba na kazi ya Mungu na wachungaji wengi na wazee wa kanisa hutia hatiani na kupinga kazi mpya wa Mungu, hili limesababisha Mungu kuwachukia na kuwalaani. Hiki ndicho chanzo cha giza la ulimwengu wa kidini na ukiwa.
Baadaye, hawa ndugu wa kike wakasoma kifungu cha maneno ya Mungu ili nipate kuwa na ufahamu dhahiri. Hasa kwa sababu Mungu amefanya tena kazi mpya, kazi ya Roho Mtakatifu imesogea. Madhehebu yote ambayo hayana kazi ya Roho Mtakatifu huwa na giza na ukiwa zaidi na zaidi. Mwenyezi Mungu alisema: “kazi Yake katika maeneo mengine itakoma, na watu watalazimishwa kutafuta njia ya kweli. Itakuwa kama Yusufu: Kila mtu alimwendea kwa ajili ya chakula, na kumsujudia, kwa sababu alikuwa na vyakula. Ili kuweza kuepuka njaa watu watalazimishwa kutafuta njia ya kweli. Jumuiya yote ya kidini inakufa kwa njaa, na ni Mungu tu wa leo ndiye chemchemi ya maji ya uzima, akiwa na kisima chenye maji yasiyokauka kilichotolewa kwa ajili ya furaha ya mwanadamu, na watu watakuja na kumtegemea. Huo ndio utakuwa muda ambapo matendo ya Mungu yatafichuliwa, na Mungu atatukuzwa; watu wote katika ulimwengu wote watakuja na kumwabudu ‘mtu’ asiyekuwa wa kawaida. Je, hii haitakuwa siku ya utukufu wa Mungu?” (“Ufalme wa Milenia Umewasili” katika Neno Laonekana katika Mwili) Nilipokumbuka hali niliyoiona katika Uprotestanti na Ukatoliki, pia ikathibitishwa zaidi moyoni mwangu kwamba maneno ya Mwenyezi Mungu yaliongea juu ya hali halisi. Maneno Yake ni ya uhalisi na ya kweli. Kazi ya Roho Mtakatifu kweli imesogea Bila kujali kama ilikuwa katika Uprotestanti au Ukatoliki, kile nilichokuwa nimehisi kilikuwa ni shauku ya watu ya nje tu. Nilichojifunza tu ni maarifa ya maandiko na nadharia za kidini. Cha msingi hakukuwa na mwanga mpya wala sikuhisi ugavi wa kiroho wa maisha. Miongoni mwa watu wanaomfuata Mungu kwa kweli, ni nani ambaye hajataka kupata chakula cha kiroho? Niliona kwamba maneno ya Mwenyezi Mungu yana uwezo wa kuvunja pingu zangu na kuyafungua mafumbo ya Biblia. Maneno Yake yaliangaza moyo wangu. Moyo wangu haukukanganyikiwa tena. Kwa hakika nimepata faida nyingi! Baada ya hayo, Dada Ma alileta nakala ya kitabu Neno Laonekana katika Mwili na akasoma baadhi ya vifungu vingine: “Kazi ya kumsimamia mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu, na ina maana kuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu. Hatua hizi tatu hazihusishi kazi ya kuuumba ulimwengu, ila ni hatua tatu za kazi ya Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme” (“Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili). “Kutoka kwa kazi ya Yehova mpaka ile ya Yesu, na kutoka kwa kazi ya Yesu hadi kwa kazi iliyoko kwa awamu hii ya sasa, awamu hizi tatu zinajumlisha upana wote wa usimamizi wa Mungu, na zote ni kazi za Roho mmoja. Kutoka Alipoumba ulimwengu, Mungu Amekuwa Akisimamia wanadamu. Yeye ndiye Mwanzo na ndiye Mwisho; Yeye ndiye wa Kwanza na wa Mwisho, na Yeye ndiye mwanzilishi wa enzi na Yeye ndiye huleta enzi kwenye kikomo” (“Maono ya Kazi ya Mungu (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili). “Kazi inayofanywa kwa sasa imesukuma mbele kazi ya Enzi ya Neema; yaani, kazi katika mpango mzima wa usimamizi wa miaka elfu sita imesonga mbele. Ingawa Enzi ya Neema imekoma, kazi ya Mungu imeendelea sana. Kwa nini Ninazungumza mara kwa mara kwamba hatua hii ya kazi inajenga juu ya Enzi ya Neema na Enzi ya Sheria? Hii ina maana kwamba kazi ya wakati huu ni mwendelezo wa kazi iliyofanyika katika Enzi ya Neema na kuinua kazi ile iliyofanyika katika Enzi ya Sheria. Hatua hizi tatu zinaingiliana kwa karibu na kuunganika moja kwa inayofuata. … Ni muungano tu wa hatua tatu za kazi ndio unaweza kuchukuliwa kuwa mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita” (“Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili” katika Neno Laonekana katika Mwili). Alipomaliza kusoma maneno ya Mwenyezi Mungu, alisema, “Kutoka kwa maneno ya Mwenyezi Mungu, tunaona kuwa tangu wanadamu walipopotoshwa na Shetani, Mungu alianza kufanya kazi ya kuwaokoa wanadamu. Kazi hii imegawanywa katika hatua tatu: kazi ya Bwana Mungu katika Enzi ya Sheria, kazi ya Bwana Yesu katika Enzi ya Neema na Kazi ya Mwenyezi Mungu katika Enzi ya Ufalme ya siku za mwisho. Wakati wa Enzi ya Sheria, Yehova Mungu alitoa sheria ili mtu angetambua dhambi zake. Wakati wa Enzi ya Neema, Bwana Yesu alitundikwa msalabani ili kumkomboa mwanadamu. Sasa, katika Enzi ya Ufalme ya siku za mwisho, Mwenyezi Mungu amefanya kazi ya hukumu kwa njia ya maneno Yake juu ya msingi wa kazi ya Bwana Yesu ya ukombozi ili kutatua hali yetu ya dhambi, kufuta dhambi zetu na kututakasa kabisa na kutuokoa. Ushahidi unathibitisha kwamba Mwenyezi Mungu ni kuonekana kwa Yehova Mungu aliyetoa sheria na kuyaongoza maisha ya mwanadamu. Yeye ni ujio wa pili wa Bwana Yesu aliyewakomboa wanadamu kwa kutundikwa msalabani. Ndani ya hatua hizi tatu za kazi, bila kujali jinsi jina la Mungu na kazi zimebadilika, kusudi la kazi ya Mungu, ambalo ni nia ya kuwaokoa wanadamu, haijawahi kubadilika. Asili ya Mungu haitawahi kubadilika kamwe. Kila moja ya hatua hizi tatu za kazi imejengwa juu ya msingi wa hatua iliyotangulia. Kila hatua ni yenye kina zaidi na ya juu zaidi kuliko ya mwisho Kazi ya Mungu imefanywa kulingana na maendeleo ya enzi. Imefanywa kulingana na mahitaji ya wanadamu ili Yeye angeweza kutuokoa na kutupata vyema. Kwa maneno mengine, kazi ya sheria ya Yehova Mungu, kazi ya ukombozi ya Bwana Yesu na kazi ya hukumu ikianzia na nyumba ya Mungu inayofanyika na Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho ni aina tofauti za kazi zinazofanywa katika enzi tofauti na Mungu yule yule. Kulingana na mipango Yake mwenyewe na kulingana na mahitaji ya wanadamu, Mungu anatuokoa hatua kwa hatua.”
Wakati huu, nilihisi kwamba kazi ya Mungu ilikuwa ya ajabu sana, yenye enzi na yenye hekima. Pia nilihisi utunzaji na fikra ambazo Mungu alikuwa ameweka katika kuwaokoa wanadamu ambao walikuwa wamepotoshwa sana na Shetani na upendo mkuu wa Mungu kwetu! Maneno ya Mwenyezi Mungu yalieleza wazi juu ya ukweli huu na mafumbo ambayo sijawahi kuyasikia. Upeo wangu ulikuwa kweli umepanuka na nilichuma mengi. Niliamua kuchunguza kwa makini kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho.
Kwa kuwa kulikuwa kumechelewa sana kwa wakati huo, tuliamua kuendelea na ushirika wakati tungekutana baadaye. Kabla ya kuondoka, Dada Ma alinipa nakala ya Maneno Bora zaidi ya Mungu Kuhusu Injili ya Ufalme ili ningeweza kuchunguza kwa makini kazi ya Mungu ya siku za mwisho nikirudi nyumbani. Baada ya kurudi, kutokana na upekuzi, nilitafuta “Kanisa la Mwenyezi Mungu” kwenye mtandao. Sikufikiria kwamba ningeona propaganda hasi nyingi hivyo kutoka kwa serikali CCP na ulimwengu wa kidini ukimpinga na kumtia hatiani Mwenyezi Mungu na Kanisa Lake. Nilipoona maudhui haya, nilikuwa na uhakika zaidi kwamba Kanisa la Mwenyezi Mungu ndilo kanisa ambalo lina kazi ya Roho Mtakatifu na kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Mungu ambaye ameonekana na Anafanya kazi katika siku za mwisho. Hili ni kwa sababu, tangu wakati wa kale, njia ya kweli daima imekuwa imekandamizwa! Nilipokwenda kwa mikusanyiko na babu na bibi yangu nchini China, nilipata mateso pia kutoka kwa serikali CCP. Tulibidi tujifichefiche tulipohudhuria mikusanyiko hii. Serikali ya CCP kwa kweli ni mbaya! Wao ni serikali ya kumkana Mungu. Wanachukia ukweli na Mungu zaidi. Kwa hiyo, wanachopinga na kukandamiza labda ni njia ya kweli na kanisa la kweli. Baadaye wakati wa mkusanyiko, nikamwambia haya Dada Fang na wengine. Aliniruhusu nione tukio la ajabu, Amka Kutoka kwa Udanganyifu, katika video ya injili inayoitwa Penya Mtego. Mhusika mkuu alikuwa akitafuta, “... Lakini sielewi, kama Umeme wa Mashariki ndiyo njia ya kweli, basi kwa nini ingepingwa kwa nguvu na serikali ya CCP? Kwa nini pia viongozi wa kidini wangeishutumu kwa ghadhabu?”
Katika video, mmoja wa ndugu alijibu, “Biblia inasema, ‘dunia nzima hukaa ndani ya maovu’ (1 Yohana 5: 19). Bwana Yesu pia alisema: ‘Hiki ni kizazi kiovu’ (Luka 11: 29). Katika hali hiyo, ni kwa kiwango gani ulimwengu ni wa giza na mwovu? Katika Enzi ya Neema, ili kuwakomboa wanadamu, Bwana Yesu aliyepata mwili alitundikwa msalabani na ulimwengu wa kidini na watawala wa wakati huo. Mwenyezi Mungu wa siku za mwisho ambaye amekuja kuonyesha ukweli na kuwahukumu wanadamu pia Anakabiliwa na kupatikana na hatia na upinzani wa ulimwengu wa kidini na utawala wa kisiasa wa joka kubwa jekundu na Anakataliwa na enzi hii. Hili linatimiza maneno ya Bwana Yesu: ‘Kwa kuwa kama vile umeme, umulikavyo toka upande mmoja chini ya mbingu, na kumulika upande mwingine chini ya mbingu; ndivyo atakavyokuwa Mwana wa Adamu katika siku yake. Lakini kwanza, ni lazima apate mateso mengi, na kukataliwa na kizazi hiki’ (Luka 17:24-25). Utabiri huu wa Bwana Yesu umekwisha kutimizwa. Kila mtu ambaye huhisi kiu ya kuonekana kwa Mungu anapaswa kuona wazi kwamba Bwana amekwisha kurudi muda mrefu uliopita na yu katika maendeleo ya kufanya kazi ya hukumu ya siku za mwisho. Utabiri wa Bwana Yesu tayari umetimizwa. Inawezekana kuwa hatuoni ukweli kwa dhahiri?”
Shahidi mwingine akaendelea kusema: “Ndugu wa kiume na wa kike, serikali hii ya kisiasa ya kumkana Mungu na wengi wa viongozi wa ulimwengu wa dini ni vikosi vya kishetani vinavyomchukia Mungu na ukweli. Hili tayari limethibitishwa na ukweli kwamba Bwana Yesu alitundikwa msalabani. Hiyo ndiyo maana njia ya kweli daima itakabiliwa na kukataliwa na kupatikana na hatia na utawala wa kisiasa na ulimwengu wa kidini. Aidha, wale wote ambao hueneza njia ya kweli na kuweka ukweli katika matendo watasingiziwa na kulazimishwa nao pia. Hivi ni kama Bwana Yesu alivyosema, ‘Iwapo ulimwengu utawachukia, mwajua ya kuwa ulinichukia mimi kabla ya kuwachukia ninyi. Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda walio wake: lakini kwa sababu ninyi si wa ulimwengu, bali mimi niliwachagua katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia’ (Yohana 15:18-19). Ni kwa sababu hii hii ambapo kotekote katika enzi, wale wanaoweza kukubali njia ya kweli na kumfuata Mungu wa kweli ni watu wachache sana tu ambao wanapenda ukweli na kufuata ukweli. Hata hivyo, wengi wa watu hawathubutu kuchunguza njia ya kweli na matokeo yake ni, hupoteza fursa ya wokovu wa Mungu kwa sababu wao hufuata nguvu ya Shetani au wanaogopa kuwa wakiteswa. Hiyo ndiyo maana Bwana Yesu alionya hapo awali: ‘Ingilieni lango lililo jembamba: kwa maana lango ni pana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiliao lango hilo: Kwa kuwa lango ni jembamba, na njia imesonga, iendayo uzimani, nao waionao ni wachache’ (Mathayo 7:13-14).” Nilipoona mambo haya katika video, nilijihisi kuwa na hakika hata zaidi kwamba kile serikali ya CCP hukitesa na kutia hatiani kwa kweli ni njia ya kweli. Hili ni la hakika.
Baada ya kipindi cha kukusanya na uchunguzi, nilikuwa na ufahamu wa kina wa kazi ya hukumu ya Mungu ya siku za mwisho kutoka kwa maneno ya Mwenyezi Mungu na kushirikiana na kuwasiliana kwa ndugu wa kiume na wa kike. Pia nilipata ufahamu wa ukweli kuhusu upataji wa mwili, wokovu na wokovu kamili, kusudi la Mungu la kuwasimamia wanadamu, mwisho wa wanadamu na makusudio na njia za asili za uzima wa milele. Ukweli ambao Mungu Mwenyezi ameuonyesha ni mwingi sana. Kutoka ndani ya moyo wangu, niliamini kwa uhakika kwamba Mwenyezi Mungu ndiye kweli ujio wa pili wa Bwana Yesu. Kwa furaha niliikubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho.
Nimestahamili katika kusali kila siku na kusoma maneno ya Mungu. Mara kwa mara, nilisikiliza pia mahubiri na ushirika juu ya kuingia katika maisha na nyimbo za maneno ya Mungu na niliangalia video za injili. Kila wiki, nilikutana na ndugu zangu wa kiume na wa kike na kueneza injili na kumshuhudia Mungu pamoja nao kwa kuamili. Ninahisi kwamba maisha yangu sasa hivi ni ya fahari sana na maisha yangu ya kiroho yamelishwa na ni ya kufurahisha. Hatimaye, nimerudi kwa kanisa la kweli na nimepata “familia” yangu ya kweli. Katika siku za nyuma, makanisa niliyoyahudhuria yalikuwa na wachungaji na makasisi ambao walihitaji kushughulikiwa. Hata hivyo, katika Kanisa la Mwenyezi Mungu, ndugu zangu wa kiume, wa kike, nami sote twamheshimu Mungu kama mkuu. Uhusiano baina yetu hautofautishwi kulingana na hadhi. Kila mtu ni sawa. Pia hakuna kanuni au kaida za dini wakati wa mikusanyiko hii. Unaweza kuhudhuria kulingana na mahitaji yako na wakati wako. Hakuna mtu atakayekuzuia au kukulazimisha. Kile kila mtu huwasiliana kuhusu ni jinsi ya kutafuta na kuwa mtu mwaminifu, jinsi ya kutafuta mabadiliko katika tabia ya mtu ili kupata utakaso na wokovu, jinsi ya kutimiza wajibu wa mtu ili kulipa upendo wa Mungu na kumridhisha Mungu, nk. Bila kufahamu, chini ya uongozo wa maneno ya Mungu, nikaanza pia kutafuta mabadiliko katika tabia yangu na kuona vitu kulingana na maneno ya Mungu; pia nilikuwa na ufahamu wa na nilijua jinsi ya kutofautisha asili mbaya ya mkondo wa jamii na taratibu na njia ambazo Shetani humdanganyia mtu. Kuanzia hapo kuendelea, sikucheza tena michezo ya video wala kupoteza wakati kwa kwenda kwa KTV. Nilipokuwa na wakati, ningesoma maneno ya Mungu au ningekusanyika na ndugu zangu wa kiume na wa kike kwa ushirika ambapo tungeimba na kumsifu Mungu. Kila siku ilikuwa na wingi wa mambo. Sikujisikia tena mtupu na nisiyejiweza. Aidha, nilikuwa dhahiri kuhusu malengo yangu ya maisha. Nilijua kwamba maana ilikuwa ipatikane kupitia kwa mtu kutimiza wajibu wake mwenyewe mbele ya Mungu na kuishi kwa ajili ya Mungu kama moja wa uumbaji wake. Ninamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniongoza mimi kuitembea njia sahihi ya uzima. Niko tayari kuweka mamlaka yote, utukufu na sifa kwa miguu ya Mungu mmoja wa kweli, tangu sasa hadi milele. Amina!
Chanzo: Niliupata Mwanga wa Kweli
0 意見:
Chapisha Maoni