Inaonyesha machapisho ya hoja yaliyopangwa kwa uhusiano neema. Panga kwa tarehe Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho ya hoja yaliyopangwa kwa uhusiano neema. Panga kwa tarehe Onyesha machapisho yote
Jumatatu, 20 Mei 2019
2. Kuna tofauti ipi kati ya jinsi ambavyo Bwana Yesu alifanya kazi katika Enzi ya Neema na jinsi Mwenyezi Mungu anavyofanya katika Enzi ya Ufalme?
Maneno Husika ya Mungu:
Wakati wa kupata mwili Kwake mara ya kwanza, ilikuwa muhimu kwa Mungu kuponya wagonjwa na kufukuza mapepo kwa sababu kazi Yake ilikuwa ni kukomboa. Ili kulikomboa kabila lote la mwanadamu, Alipaswa kuwa mwenye upendo na mwenye kusamehe. Kazi Aliyoifanya kabla ya kusulubiwa ilikuwa kuponya watu na kufukuza mapepo, ambayo iliashiria wokovu Wake wa mwanadamu kutoka katika dhambi na uchafu. Kwa sababu ilikuwa ni Enzi ya Neema, ilikuwa muhimu Kwake kuponya wagonjwa, na kwa njia hiyo Alionyesha ishara na miujiza, mambo ambayo yalikuwa kiwakilishi cha neema katika hiyo enzi; kwani Enzi ya Neema ilikitwa katika kutolewa kwa neema, ikiashiriwa na amani, furaha, na baraka ya vitu, vyote vikiwa zawadi za imani ya watu kwa Yesu. Hii ni kusema kuwa, kuponya wagonjwa, kufukuza mapepo na kutoa neema ulikuwa uwezo asilia wa mwili wa Yesu katika Enzi ya Neema, mambo haya yalikuwa ni kazi ya Roho iliyopatikana katika mwili.
kutoka katika “Kiini cha Mwili Ulio na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kazi ambayo Yesu alifanyika ililingana na mahitaji ya mwanadamu katika enzi hiyo. Kazi Yake ilikuwa ni kuwakomboa wanadamu, kuwasamehe dhambi zao, na kwa hivyo tabia Yake yote ilikuwa ya unyenyekevu, uvumilivu, upendo, ucha Mungu, ustahamilivu, huruma na wema. Aliwabariki wanadamu kwa wingi na kuwaletea neema nyingi, na mambo yote ambayo wangeweza kufurahia, Aliwapa kwa ajili ya furaha yao: amani na furaha, uvumilivu Wake na upendo, huruma Yake na wema. Katika siku hizo, chote alichokutana nacho mwanadamu kilikuwa wingi wa vitu vya kufurahia tu: Moyo wake ulikuwa na amani na uhakikisho, roho yake ilifarijika, na alikuwa anaruzukiwa na Mwokozi Yesu. Sababu iliyomfanya mwanadamu aweze kufaidi mambo haya ni matokeo ya enzi alimoishi. Katika Enzi ya Neema mwanadamu alikuwa amepotoshwa tayari na Shetani, na hivyo kazi ya ukombozi wa wanadamu wote ulihitaji neema nyingi, ustahimili na uvumilivu usio na mwisho, na hata zaidi, sadaka ya kutosha kulipia dhambi za wanadamu, ili kufikia athari yake. Kile wanadamu walichoona katika Enzi ya Neema kilikuwa tu sadaka Yangu ya kulipia dhambi za binadamu, yaani, Yesu. Yote waliyojua ni kwamba Mungu angeweza kuwa mwenye huruma na uvumilivu, na yote waliyoona ni huruma ya Yesu na wema Wake. Hii yote ilikuwa ni kwa sababu wao waliishi katika Enzi ya Neema. Na hivyo, kabla ya kuweza kukombolewa, walilazimika kufurahia neema za aina nyingi ambazo Yesu aliwapa; hili pekee ndilo lilikuwa la manufaa kwao. Kwa njia hii, wangeweza kusamehewa dhambi zao kupitia kufurahia kwao neema, na pia wangeweza kuwa na nafasi ya kukombolewa kupitia kufurahia ustahimili wa Yesu na uvumilivu. Ni kwa njia ya ustahimili wa Yesu na uvumilivu pekee ndio walipata haki ya wa kupokea msamaha na kufurahia neema nyingi kutoka kwa Yesu—kama vile Yesu alivyosema: Sijakuja kuwakomboa wenye haki, ila wenye dhambi, kukubali dhambi zao zisamehewe. … Jinsi Yesu alivyowapenda wanadamu zaidi, Akisamehe dhambi zao na kuwapa huruma na wema wa kutosha, ndivyo wanadamu walizidi kuwa na uwezo wa kuokolewa, wa kuitwa wanakondoo waliopotea ambao Yesu Aliwanunua tena kwa gharama kubwa. Shetani hakuweza kuingilia katika kazi hii, kwa sababu Yesu Aliwatunza wafuasi Wake kama mama mwenye upendo anavyotunza mtoto mchanga aliye kifuani pake. Yeye hakuwa na hasira nao au kuwadharau, bali Alikuwa Amejaa faraja; Yeye kamwe hakuwa na ghadhabu miongoni mwao, lakini alistahimili dhambi zao na Akapuuza upumbavu wao na kutofahamu, hata kusema, “Uwasamehe wengine mara sabini mara saba.” Kwa hiyo moyo Wake ulirekebisha mioyo ya wengine. Ilikuwa ni kwa njia hii ndiyo watu walipokea msamaha wa dhambi kupitia uvumilivu Wake.
kutoka katika “Maelezo ya Kweli ya Kazi Katika Enzi ya Ukombozi” katika Neno Laonekana katika Mwili
Roho Mtakatifu Anafanya kazi kulingana na enzi, sio tu katika mapenzi Yake ama kulingana na masharti. Enzi zimebadilika, na enzi mpya lazima ilete kazi mpya. Huu ni ukweli wa kila hatua ya kazi, na hivyo kazi Yake haiwezi kurudiwa. Katika Enzi ya Neema, Yesu Alifanya nyingi ya kazi hiyo, kama kuponya magonjwa, kukemea mapepo, kuwekelea mikono Yake juu ya wanadamu, na kumbariki mwanadamu. Hata hivyo, kuendelea kufanya hivyo hakutasaidia chochote katika wakati huu. Roho Mtakatifu Alifanya kazi hivyo katika huo wakati, kwani ilikuwa Enzi ya Neema, na mwanadamu alipewa neema ya kutosha ili afurahie. Mwanadamu hakuhitajika kulipa gharama yoyote na angepokea neema mradi tu angekuwa na imani. Kila mtu alitendewa kwa neema kubwa. Sasa, enzi imebadilika, na kazi ya Mungu imeendelea zaidi; kupitia kuadibu na hukumu Yake, uasi wa mwanadamu na vitu vichafu katika mwanadamu vitatupiliwa mbali. Jinsi ilivyokuwa hatua ya wokovu, ilimbidi Mungu kufanya kazi hiyo, Akimwonyesha mwanadamu neema ya kutosha ili mwanadamu afurahie, ili Amkomboe mwanadamu kutoka kwa dhambi, na kwa neema amsamehe mwanadamu dhambi zake. Hatua hii ya sasa ni ya kufichua udhalimu ulio ndani ya mwanadamu kwa njia ya kuadibu, hukumu, kupigwa na maneno, na vile vile nidhamu na ufunuo wa maneno, ili baadaye binadamu waweze kuokolewa. Hii ni kazi ya undani zaidi kuliko ukombozi. Katika Enzi ya Neema, mwanadamu alifurahia neema ya kutosha na amezoea neema hii, kwa hivyo sio ya kufurahiwa na mwanadamu tena. Kazi kama hii imepitwa na wakati sasa na haitafanyika tena. Sasa, mwanadamu anaokolewa kupitia hukumu ya neno. Baada ya mwanadamu kuhukumiwa, kuadibiwa na kusafishwa, tabia yake basi inabadilika. Je sio kwa sababu ya maneno ambayo Nimenena?
kutoka katika “Fumbo la Kupata Mwili (4)” katika Neno Laonekana katika Mwili
Mungu Anapopata mwili mara hii, kazi Yake ni kuonyesha tabia Yake, kimsingi kupitia kuadibu na hukumu. Akitumia haya kama msingi, Analeta ukweli zaidi kwa mwanadamu, kuonyesha njia zaidi za matendo, na hivyo Hufikia lengo Lake la kumshinda mwanadamu na kumwokoa mwanadamu kutokana na tabia yake potovu. Hili ndilo liko katika kazi ya Mungu katika Enzi ya Ufalme.
Dibaji ya Neno Laonekana katika Mwili
Kile ambacho Nasema leo ni kuhukumu dhambi za watu na maovu yao; ni kulaani uasi wa watu. Udanganyifu na upotovu wao, na maneno na matendo yao, mambo yote ambayo hayako sambamba na mapenzi Yake yatapitia hukumu, na uasi wa watu unaamuliwa kuwa wenye dhambi. Ananena kulingana na kanuni za hukumu, naye anadhihirisha tabia Yake yenye haki kwa kuhukumu maovu yao, kulaani uasi wao, na kufichua nyuso zao zote mbaya.
kutoka katika “Jinsi Hatua ya Pili ya Kazi ya Ushindi Huzaa Matunda” katika Neno Laonekana katika Mwili
Mungu ana njia nyingi za kumkamilisha mwanadamu. Yeye hutumia mazingira ya kila aina ili shughulikia tabia potovu ya mwanadamu, na hutumia vitu mbalimbali ili kumuweka mwanadamu wazi; katika suala moja Yeye humshughulikia mwanadamu, katika jingine Yeye humuweka mwanadamu wazi, na katika jingine Yeye humfichua mwanadamu, kuzichimbua na kuzifichua “siri” katika vina vya moyo wa mwanadamu, na kumwonyesha mwanadamu asili yake kwa kuzifichua hali zake nyingi. Mungu humkamilisha mwanadamu kupitia mbinu nyingi—kupitia ufunuo, ushughulikiaji, usafishwaji, na kuadibu—ili mwanadamu aweze kujua kwamba Mungu ni wa vitendo.
kutoka katika “Ni Wale Wanaolenga Kutenda tu Ndio Wanaweza Kukamilishwa” katika Neno Laonekana katika Mwili
Mungu sasa ameanza rasmi kuwakamilisha watu. Ili kufanywa kuwa kamili, watu lazima wapitie ufunuo, hukumu, na kuadibu kwa maneno ya Mungu, na kupitia majaribio na usafishaji wa maneno Yake (kama vile jaribio la watendaji huduma). Kuongezea, watu lazima waweze kustahimili jaribio la kifo. Yaani, mtu ambaye kweli anafanya mapenzi ya Mungu anaweza kutoa sifa kutoka ndani ya kina cha moyo wake katikati ya hukumu ya Mungu, kuadibu, na majaribio, na anaweza kutii Mungu kwa ukamilifu na kujitelekeza mwenyewe, hivyo kumpenda Mungu kwa moyo wa uaminifu, nia moja, na utakatifu; huyo ndiye mtu kamili, na pia ni kazi ambayo Mungu anataka kufanya, na kile ambacho Mungu anataka kutimiza.
kutoka katika “Juu ya Hatua za Kazi ya Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Ni kupitia nini ndiyo ukamilishaji wa Mungu kwa mwanadamu hutimizwa? Kupitia tabia Yake yenye haki. Tabia ya Mungu hasa huwa na haki, ghadhabu, uadhama, hukumu, na laana, na ukamilishaji Wake wa mwanadamu hasa ni kupitia hukumu. Watu wengine hawaelewi, na huuliza ni kwa nini Mungu anaweza tu kumfanya mwanadamu kuwa mkamilifu kupitia hukumu na laana. Wao husema kwamba kama Mungu angemlaani mwanadamu, si mwanadamu angekufa? Kama Mungu angemhukumu mwanadamu, si mwanadamu angelaaniwa? Basi anawezaje hata hivyo kufanywa mkamilifu? Hayo ndiyo maneno ya watu wasioijua kazi ya Mungu. Kile ambacho Mungu hulaani ni uasi wa mwanadamu, na kile Anachohukumu ni dhambi za mwanadamu. Ingawa Yeye hunena kwa ukali, na bila kiwango cha hisi hata kidogo, Yeye hufichua yote yaliyo ndani ya mwanadamu, na kupitia maneno haya makali Yeye hufichua kile kilicho muhimu ndani ya mwanadamu, lakini kupitia hukumu kama hiyo, Yeye humpa mwanadamu ufahamu mkubwa wa kiini cha mwili, na hivyo mwanadamu hujitiisha chini ya utii mbele za Mungu. Mwili wa mwanadamu ni wa dhambi, na wa Shetani, ni wa kutotii, na chombo cha kuadibu kwa Mungu—na kwa hiyo, ili kumruhusu mwanadamu kujijua, maneno ya hukumu ya Mungu lazima yamfike na lazima kila aina ya usafishaji itumike; ni wakati huo tu ndiyo kazi ya Mungu inaweza kuwa ya kufaa.
kutoka katika “Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kwenye macho ya mwanadamu, wokovu ni upendo wa Mungu, na upendo wa Mungu hauwezi kuwa kuadibu, kuhukumu, na kulaani; wokovu lazima uwe na upendo, huruma, na, zaidi ya hayo, maneno ya faraja, na lazima wokovu uwe na baraka zisizo na mipaka kutoka kwa Mungu. Watu husadiki kwamba wakati Mungu anapomwokoa mwanadamu Anafanya hivyo kwa kumgusa yeye na kumfanya yeye kuutoa moyo wake na kumpa Yeye kupitia kwa baraka na neema Zake. Hivyo ni kusema, Anapomgusa mwanadamu Anamwokoa yeye. Wokovu kama huu ni wokovu ambao shughuli ya biashara inafanywa. Pale tu ambapo Mungu atampa yeye mara mia ndipo mwanadamu anaponyenyekea kwa jina la Mungu, na kulenga kuwa na mienendo mizuri mbele ya Mungu na kumletea Yeye utukufu. Haya si mapenzi ya Mungu kwa mwanadamu. Mungu amekuja kufanya kazi ulimwenguni ili kumwokoa mwanadamu aliyepotoka—hakuna uongo katika haya; kama upo, Asingefanya kazi Yake yeye Mwenyewe. Kitambo, mbinu Zake za wokovu zilikuwa kuonyesha upendo na huruma mkuu, kiasi cha kwamba Alijitolea Yake yote kwa Shetani ili naye aweze kuwapata wanadamu wote. Leo haifanani kamwe na kitambo: Leo, wokovu wako unatokea kwenye wakati wa siku za mwisho, wakati wa uainishaji wa kila mmoja kulingana na aina yake; mbinu za wokovu wako si upendo wala huruma, lakini kuadibu na hukumu ili mwanadamu aweze kuokolewa kabisa. Hivyo basi, kila kitu unachopokea ni kuadibu, hukumu, na kupiga bila huruma, lakini jua kwamba katika kupiga huku kusiko na huruma hakuna hata adhabu ndogo zaidi, jua kwamba licha ya namna ambavyo maneno haya yanavyoweza kuwa makali, kile kinachokupata ni maneno machache yanayoonekana kutokuwa na huruma kabisa kwako, na jua kwamba, licha ya namna ambavyo hasira Yangu itakavyokuwa, kile kitakachokujia bado ni maneno ya mafunzo, na sinuii kukudhuru, au kukuua. Je, haya yote ni ukweli, sivyo? Jua kwamba leo, haijalishi kama kutakuwa na kuhukumu kwa haki au utakasaji usio na huruma na kuadibu, yote haya ni kwa minajili ya wokovu. Haijalishi kama leo kunao uainishaji wa kila mmoja kulingana na aina yake, au uwekaji wazi wa aina za mwanadamu, matamko yote ya Mungu na kazi ni kwa ajili ya kuwaokoa wale wanaompenda Mungu kwa dhati. Kuhukumu kwa haki ni kwa ajili ya kumtakasa mwanadamu, utakasaji usio na huruma ni kwa ajili ya kumsafisha mwanadamu, maneno makali au kuadibu yote ni kwa ajili ya kutakasa, na kwa minajili ya wokovu. Na hivyo, mbinu ya leo ya wokovu haifanani na ya kitambo. Leo, kuhukumu kwa haki kunakuokoa wewe, na ni zana nzuri pia ya kumuainisha kila mmoja wenu kulingana na aina, na kuadibu kusiko na huruma kunawaletea wokovu mkubwa—na ni kipi ambacho unahitajika kusema mbele ya kuadibu na kuhukumu huku? Je, hujafurahia wokovu kutoka mwanzo hadi mwisho? … Hebu fikiria: Kama nia Yangu ya kuja ulimwenguni ingekuwa ni kushutumu na kukuadhibu wewe, na wala si kukuokoa, je, siku zako zingedumu kwa muda mrefu? Mngeweza, enyi viumbe wenye dhambi wa mwili na damu, kuishi hadi leo? Kama ingekuwa tu ni kwa ajili ya kuwaadhibu nyinyi, kwa nini Nikawa mwili na kuanza kushughulikia shughuli kubwa kama hiyo? Je, lisingekuwa neno moja tu ambalo Ningetumia kuwaadhibu nyinyi viumbe wenye kufa tu? Ningekuwa bado na akili ya kukuangamiza baada ya kukushutumu? Je, bado husadiki maneno haya Yangu? Ningeweza kumwokoa mwanadamu kupitia tu kwa upendo na huruma? Au Ningetumia tu kusulubishwa kwa minajili ya kumwokoa mwanadamu? Je, tabia Yangu yenye haki si nzuri zaidi ya kumfanya mwanadamu kuwa mtiifu kabisa? Je, haiwezi kabisa kumwokoa mwanadamu zaidi?
Ingawa maneno Yangu yanaweza kuwa makali, yote yanasemwa kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu, kwa kuwa Ninazungumza tu maneno na sio kuuadhibu mwili wa mwanadamu. Maneno haya humsababisha mwanadamu kuishi katika nuru, kujua kwamba mwanga upo, kujua kwamba mwanga ni wa thamani, hata zaidi kujua jinsi maneno haya yalivyo na manufaa kwa mtu, na kujua kwamba Mungu ni wokovu. Ingawa Nimesema maneno mengi ya kuadibu na hukumu, hayajafanywa kwako katika vitendo. Nimekuja kufanya kazi Yangu, kuzungumza maneno Yangu na, ingawa maneno Yangu yanaweza kuwa magumu, yanasemwa kwa hukumu ya upotovu na uasi wako. Madhumuni Yangu ya kufanya hili yanabaki kumwokoa mtu kutoka kwa utawala wa Shetani, kutumia maneno Yangu ili kumwokoa mwanadamu; Kusudi Langu sio kumdhuru mwanadamu kwa maneno Yangu. Maneno Yangu ni makali ili matokeo yaweze kupatikana kutoka katika Kazi Yangu. Ni katika kufanya kazi kwa njia hii tu ndipo mtu anaweza kujijua na anaweza kujitenga mbali na tabia yake ya uasi.
kutoka katika “Mnapaswa Kuweka Pembeni Baraka za Hadhi na Kuelewa Mapenzi ya Mungu kwa ajili ya Wokovu wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kondoo wa Mungu Huisikia Sauti ya Mungu
Jumapili, 5 Novemba 2017
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Maelezo ya Kweli ya Kazi Katika Enzi ya Ukombozi
Novemba 05, 2017Enzi ya Ukombozi, maneno-ya-Mwenyezi-Mungu, msalaba, Mwokozi Yesu, Neno-Laonekana-katika-Mwili, Vitabu, YesuNo comments
Maelezo ya Kweli ya Kazi Katika Enzi ya Ukombozi
Mwenyezi Mungu alisema, Mpango Wangu mzima wa usimamizi, ambao una urefu wa miaka elfu sita, unashirikisha awamu tatu, au enzi tatu: Kwanza, Enzi ya Sheria; pili, Enzi ya Neema (ambayo pia ni enzi ya Ukombozi); na mwisho, Enzi ya Ufalme.
Ijumaa, 3 Mei 2019
3. Uhusiano Kati ya Kila Moja ya Hatua Tatu za Kazi ya Mungu
Mei 03, 2019Kazi-ya-Mungu, Kumbukumbu-za-Maongezi-ya-Kristo, kumjua-Mungu, Tabia-ya-Mungu, VitabuNo comments
II. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Hatua Tatu za Kazi ya Wokovu wa Mungu kwa Wanadamu
3. Uhusiano Kati ya Kila Moja ya Hatua Tatu za Kazi ya Mungu
Maneno Husika ya Mungu:
Kutoka kwa kazi ya Yehova mpaka ile ya Yesu, na kutoka kwa kazi ya Yesu hadi kwa kazi iliyoko kwa awamu hii ya sasa, awamu hizi tatu zinajumlisha upana wote wa usimamizi wa Mungu, na zote ni kazi za Roho mmoja. Kutoka Alipoumba ulimwengu, Mungu Amekuwa Akisimamia wanadamu. Yeye ndiye Mwanzo na ndiye Mwisho; Yeye ndiye wa Kwanza na wa Mwisho, na Yeye ndiye mwanzilishi wa enzi na Yeye ndiye huleta enzi kwenye kikomo.
Jumatatu, 20 Agosti 2018
Dondoo kutoka kwa Vifungu Vinne vya Neno La Mungu Kuhusu "Fumbo la Kupata Mwili (4)"
Agosti 20, 2018Kupata-Mwili, Matamshi-ya-Kristo-wa-Siku-za-Mwisho-Chaguzi, Roho-Mtakatifu, Vitabu, YesuNo comments
Dondoo kutoka kwa Vifungu Vinne vya Neno la Mungu Kuhusu "Fumbo la Kupata Mwili (4)"
Mnapaswa kujua kuhusu hadithi ya ndani na uumbaji wa Biblia. Ufahamu huu haushikiliwi na wale ambao hawajakubali kazi mpya ya Mungu. Wao hawajui. Waelezee mambo haya ya kiini, na hawatakuwa pamoja nawe wenye kushikilia sana elimu ya vitabuni na sheria kuhusu Biblia.
Alhamisi, 16 Mei 2019
2. Kuna uhusiano gani kati ya kila hatua ya kazi ya Mungu na majina Yake?
IV. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Hatua Tatu za Kazi ya Mungu na Majina Yake
2. Kuna uhusiano gani kati ya kila hatua ya kazi ya Mungu na majina Yake?
(1) Umuhimu wa Mungu kuchukua jina la Yehova katika Enzi ya Sheria
Aya za Biblia za Kurejelea:
“Na Mungu akasema zaidi kwa Musa, Utawaambia hivi wana wa Israeli, Yehova Mungu wa baba zenu, Mungu wake Ibrahimu, Mungu wake Isaka, na Mungu wake Yakobo, amenituma kwa ninyi: jina langu ni hili milele, na hili ni kumbukumbu yangu kwa vizazi vyote” (Kutoka 3:15).
Maneno Husika ya Mungu:
“Yehova” ni jina Nililolichukua wakati wa kazi Yangu kule Uyahudi, nalo linamaanisha Mungu wa Wayahudi (Wateule wa Mungu) Anayeweza kumhurumia mwanadamu, kumlaani mwanadamu, na kuyaongoza maisha ya mwanadamu. Linamaanisha Mungu anayemiliki nguvu kuu na Amejawa na hekima. … Yaani, Yehova pekee ndiye Mungu wa watu wateule wa Uyahudi, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, Mungu wa Musa, na Mungu wa Wayahudi wote. Na hivyo katika enzi ya sasa, Wayahudi wote isipokuwa kabila la Yuda wanamwabudu Yehova. Wanamtolea kafara kwa madhabahu, na kumtumikia wakiwa wamevalia mavazi ya kikuhani katika hekalu. Wanachotumainia ni kuonekana tena kwa Yehova. … Jina Yehova ni jina mahsusi la Wayahudi walioishi chini ya sheria. Katika kila enzi na kila hatua ya kazi, jina Langu haliko bila msingi, lakini lina umuhimu wakilishi: Kila jina linawakilisha enzi moja. “Yehova” linawakilisha Enzi ya Sheria, nalo ni jina la heshima kwa Mungu aliyeabudiwa na Wayahudi.
kutoka katika “Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya ‘Wingu Jeupe’” katika Neno Laonekana katika Mwili
Wakati wa Enzi ya Sheria, kazi ya kumwelekeza mwanadamu ilifanyika katika Jina la Yehova, na awamu ya kwanza ya kazi ilifanyika duniani. Kazi ya awamu hii ilikuwa ni kujenga hekalu na madhabahu, na kutumia sheria kuwaongoza watu wa Israeli na kufanya kazi miongoni mwao. Kwa kuongoza watu wa Israeli, Alizindua kituo cha kazi Yake hapa duniani. Kwa msingi huu, Yeye Alipanua kazi yake nje ya Israeli, ambayo ni kusema kwamba, kuanzia Israeli, Aliendeleza kazi yake nje, ili vizazi vya baadaye walikuja kujua polepole kwamba Yehova Alikuwa Mungu, na kuwa Yehova Alikuwa Ameumba mbingu na nchi na vitu vyote, Alitengeneza viumbe vyote. Yeye Alieneza kazi yake kupitia kwa watu wa Israeli. Nchi ya Israeli ilikuwa ya mahali takatifu pa kwanza pa kazi ya Yehova hapa duniani, na kazi ya Mungu ya hapo mwanzoni ilikuwa kote katika nchi ya Israeli. Hiyo ilikuwa kazi ya Enzi ya Sheria.
kutoka katika “Maono ya Kazi ya Mungu (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili
Katika Enzi ya Sheria, Yehova aliweka amri nyingi za Musa kupitisha kwa Waisraeli waliomfuata kutoka Misri. Amri hizi walipewa Waisraeli na Yehova, na hazikuwa na uhusiano kwa Wamisri: zilinuiwa kuwazuia Waisraeli. Yeye alizitumia amri kuwatolea madai. Iwapo waliishika Sabato, iwapo waliwaheshimu wazazi wao, iwapo waliziabudu sanamu, na kadhalika: hizi zilikuwa kanuni ambazo kwazo walihukumiwa kuwa wenye dhambi au wenye haki. Miongoni mwao, kuna baadhi walioangamizwa kwa moto wa Yehova, baadhi waliopigwa mawe hadi kufa, na baadhi waliopokea baraka za Yehova, na haya yaliamuliwa kulingana na iwapo walizitii amri hizi au la. Wale ambao hawakuishika Sabato wangepigwa mawe hadi kufa. Wale makuhani ambao hawakuishika Sabato wangeangamizwa na moto wa Yehova. Wale ambao hawakuwaheshimu wazazi wao pia wangepigwa mawe hadi kufa. Yote haya yalikubaliwa na Yehova. Yehova alianzisha amri na sheria Zake ili, Alipokuwa akiwaongoza katika maisha yao, watu wangesikiliza na kuti neno Lake na kutoasi dhidi Yake. Alitumia sheria hizi kuidhibiti jamii ya binadamu iliyokuwa imezaliwa karibuni, ili kuweka vizuri zaidi msingi wa kazi Yake ya baadaye. Na kwa hivyo, kwa msingi wa kazi ambayo Yehova alifanya, enzi ya kwanza iliitwa Enzi ya sheria.
kutoka katika “Kazi katika Enzi ya Sheria” katika Neno Laonekana katika Mwili
Watu wa Israeli wote walimwita Yehova, Bwana wao. Wakati huo, walimwona kama kichwa cha familia zao, na Israeli yote ikawa familia kubwa ambapo kila mtu alimwabudu Bwana wao Yehova. Roho wa Bwana mara nyingi Aliwatokea, naye akanena na kutamka sauti Yake, na kutumia nguzo ya wingu na sauti kuongoza maisha yao. Wakati huo, Roho alitoa mwongozo Wake katika Israeli moja kwa moja, Akizungumza na kutoa sauti Yake kwa watu, na waliona mawingu na kusikia sauti za ngurumo, na kwa njia hii Aliyaongoza maisha yao kwa maelfu kadhaa ya miaka. Kwa hiyo, watu wa Israeli pekee wamekuwa wakimwabudu Yehova daima.
kutoka katika “Maono ya Kazi ya Mungu (2)” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kazi na matamshi Yake huko Israeli yaliwapa watu wote wa Israeli mwongozo walipokuwa wakiishi maisha yao katika nchi yote ya Israeli, na kwa njia hii yakaonyesha binadamu kwamba Yehova hakuweza tu kupuliza pumzi ndani ya mwanadamu, ili aweze kuwa na uhai kutoka Kwake na kuinuka kutoka mavumbini kuwa mwanadamu aliyeumbwa, lakini kwamba pia Angeweza kuwachoma wanadamu, na kuwalaani wanadamu, na kutumia fimbo Yake kuwatawala wanadamu. Kwa hivyo, pia waliona kwamba Yehova angeweza kuyaongoza maisha ya mwanadamu duniani, na kuzungumza na kufanya kazi miongoni mwa binadamu kulingana na saa za mchana na za usiku. Alifanya kazi hiyo ili tu viumbe Wake waweze kujua kwamba mwanadamu alitoka kwa mavumbi yaliyochaguliwa na Yeye, na aidha kwamba mwanadamu alikuwa ameumbwa na Yeye. Siyo haya tu, lakini kazi Aliyoanza huko Israeli ilikusudiwa ili kwamba watu na mataifa (ambao kwa kweli hawakuwa wametengwa na Israeli, lakini badala yake walikuwa wameenea kutoka kwa Waisraeli, ilhali bado walikuwa wa ukoo wa Adamu na Hawa) waweze kupokea injili ya Yehova kutoka Israeli, ili viumbe wote walioumbwa ulimwenguni waweze kuwa na uwezo wa kumcha Yehova na kumchukulia kuwa mkuu.
kutoka katika “Kazi katika Enzi ya Sheria” katika Neno Laonekana katika Mwili
Jina Yehova haliwezi kuwakilisha tabia yote ya Mungu. Ukweli kuwa Alitekeleza kazi katika Enzi ya Sheria sio ushahidi kuwa Mungu Anaweza tu kuwa Mungu chini ya sheria. Yehova alitengeneza sheria kwa mwanadamu na kutoa amri, Akimuuliza mwanadamu ajenge hekalu na madhabahu; kazi Aliyofanya inawakilisha tu Enzi ya Sheria. Kazi Aliyoifanya haidhibitishi kuwa Mungu ni Mungu Anayemwamuru mwanadamu kufuata sheria, Mungu Aliye hekaluni, ama Mungu Aliye mbele ya madhabahu. Haya hayawezi kusemwa. Kazi chini ya sheria inaweza tu kuwakilisha enzi moja.
kutoka katika “Fumbo la Kupata Mwili (4)” katika Neno Laonekana katika Mwili
(2) Umuhimu wa Mungu kuchukua jina la Yehova katika Enzi ya Neema
Aya za Biblia za Kurejelea:
“Malaika wa BWANA alitokea kwake ndotoni, akisema, Yusufu, wewe mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Mariamu mke wako: kwa kuwa alipata mimba kupitia Roho Mtakatifu. Na atazaa mwana, na wewe utamwita jina lake YESU: kwa sababu atawaokoa watu wake kutoka katika dhambi zao” (Mathayo 1:20-21).
“Na malaika akamwambia, Usiwe na woga, Mariamu: kwa kuwa umepata fadhili kwa Mungu. Na, tazama, utashika mimba na kumzaa mwana wa kiume, na utamwita jina lake YESU. Atakuwa mkuu, na ataitwa Mwana wa Aliye juu zaidi: na atapewa kiti cha enzi cha babake Daudi na Bwana Mungu: Na atatawala nyumba ya Yakobo milele; na ufalme wake hautakuwa na kikomo” (Luka 1:30-33).
Maneno Husika ya Mungu:
Jina la Yesu liliashiria mwanzo wa Enzi ya Neema. Wakati Yesu Alianza kufanya huduma Yake, Roho Mtakatifu Alianza kutoa ushuhuda kwa jina la Yesu, na jina la Yehova halikuzungumziwa tena, na badala yake Roho Mtakatifu Alianza kazi mpya hasa kwa jina la Yesu. Ushuhuda wa wale waliomwamini Yeye ulitolewa kwa ajili ya Yesu Kristo, na kazi waliyoifanya walifanya pia kwa ajili ya Yesu Kristo. Hitimisho Enzi ya Sheria ya Agano la Kale lilimaanisha kuwa kazi iliyofanywa hasa kutumia jina la Yehova ilikuwa imefikia kikomo. Baada ya hii, jina la Mungu halikuwa Yehova tena; badala yake Yeye Aliitwa Yesu, na kutoka hapa Roho Mtakatifu Alianza kazi hasa kwa kutumia jina la Yesu.
kutoka katika “Maono ya Kazi ya Mungu (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili
“Yesu” ni Imanueli, nalo linamaanisha sadaka ya dhambi iliyojawa na upendo, Amejawa na huruma, naye Anamkomboa mwanadamu. Alifanya kazi ya Enzi ya Neema, naye Anawakilisha Enzi ya Neema, na Anaweza tu kuwakilisha sehemu moja ya mpango wa usimamizi. … Yesu pekee ndiye Mkombozi wa wanadamu. Yeye ni sadaka ya dhambi ambayo ilimkomboa mwanadamu kutoka kwa dhambi. Yaani, jina la Yesu lilitoka katika Enzi ya Neema, nalo lilikuwepo kwa ajili ya kazi ya wokovu katika Enzi ya Neema. Jina la Yesu lilikuwepo ili kuwawezesha watu wa Enzi ya Neema kuzaliwa upya na kuokolewa, nalo ni jina mahsusi la wokovu wa binadamu wote. Kwa hiyo jina Yesu linawakilisha kazi ya ukombozi, nalo linaashiria Enzi ya Neema. … “Yesu” linawakilisha Enzi ya Neema, nalo ni jina la Mungu wa wale wote waliokombolewa katika Enzi ya Neema.
kutoka katika “Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya ‘Wingu Jeupe’” katika Neno Laonekana katika Mwili
Wakati wa Enzi ya Neema, jina la Mungu lilikuwa ni Yesu, ambalo lina maana kuwa Mungu Alikuwa Mungu ambaye Alimwokoa mwanadamu, na ya kwamba Alikuwa Mungu wa rehema na wa upendo. Mungu Alikuwa na mwanadamu. Upendo wake, huruma yake, na wokovu wake uliandamana na kila mtu. Mwanadamu angeweza tu kupata amani na furaha, kupokea baraka zake, kupokea neema yake kubwa na nyingi, na kupokea wokovu wake iwapo mwanadamu angekubali jina lake na akubali uwepo wake. Kupitia kusulubiwa kwa Yesu, wale wote ambao walimfuata Yeye walipokea wokovu na walisamehewa dhambi zao.
kutoka katika “Maono ya Kazi ya Mungu (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili
Yesu Alipokuja, Alifanya pia baadhi ya sehemu ya kazi ya Mungu, na kuongea baadhi ya maneno—lakini ni kazi gani kuu Aliyokamilisha? Alichokamilisha hasa ni kazi ya kusulubishwa. Akawa mfano wa mwili wenye dhambi ili kukamilisha kazi ya kusulubiwa na kuwakomboa wanadamu wote, na ilikuwa kwa ajili ya dhambi zote za binadamu, ndio Alitumika kama sadaka ya dhambi. Hii ndiyo kazi hasa Aliyokamilisha. Hatimaye, Alileta njia ya msalaba ili kuwaongoza wale waliokuja baadaye. Yesu Alipokuja, ilikuwa kimsingi kukamilisha kazi ya ukombozi. Aliwakomboa binadamu wote, na kuleta injili ya ufalme wa mbinguni kwa mwanadamu, na zaidi, Alileta njia ya ufalme wa mbinguni. Kwa sababu hii, waliokuja baada ya yote walisema, “Tunapaswa tutembee njia ya msalaba, na tujitoe kama kafara kwa ajili ya msalaba.” Bila shaka, hapo mwanzo Yesu pia Alifanya kazi nyingine na kuongea baadhi ya maneno ili kumfanya mwanadamu atubu na kukiri dhambi zake. Lakini huduma Yake ilikuwa bado ni kusulubiwa, na miaka mitatu na nusu Aliyotumia kuhubiri njia ilikuwa katika matayarisho ya kusulubiwa kulikokuja baadaye. Mara kadhaa ambazo Yesu Alisali zilikuwa pia ni kwa ajili ya kusulubishwa. Maisha ya mwanadamu wa kawaida Aliyoishi na miaka thelathini na tatu na nusu aliyoishi duniani yalikuwa kimsingi kwa ajili ya kukamilisha kazi ya kusulubishwa, yalikuwa ya kumpa nguvuya kutekeleza kazi hii, na kwa sababu hii Mungu Alimwaminia kazi ya kusulubiwa.
kutoka katika “Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Katika kazi ya Enzi ya Neema, Yesu Alikuwa Mungu ambaye Alimwokoa mwanadamu. Alichokuwa nacho na Aliyekuwa ni neema, upendo, huruma, uvumilivu, subira, unyenyekevu, huduma, na stahamala, na nyingi ya kazi ambayo Alifanya ilikuwa kwa ajili ya kumwokoa mwanadamu. Na kuhusu tabia Yake, ilikuwa tabia ya huruma na upendo, na kwa sababu Yeye Alikuwa na huruma na upendo, ilikuwa sharti asulubishwe msalabani kwa ajili ya mwanadamu, ili kuonyesha kwamba Mungu Alimpenda mwanadamu jinsi anavyojipenda, kwa kiasi kwamba Yeye mwenyewe Alijitoa kama kafara na kwa ukamilifu Wake. Shetani akasema, “Kwa kuwa Unampenda mwanadamu, Lazima Umpende kwakwa kiwango cha juu zaidi: Lazima Upigiliwe misumari msalabani, kumwokoa mwanadamu kutoka msalabani, kutoka kwa dhambi, na Wewe utajitolea Mwenyewe badala ya wanadamu wote.” Shetani akatoa dau ifuatayo: “Kwa kuwa Wewe ni Mungu Mwenye upendo na Mwenye huruma, lazima Umpende mwanadamu kwa kiwango cha juu zaidi: Lazima Ujitoe Mwenyewe msalabani.” Yesu akasema, “Maadamu ni kwa ajili ya wanadamu, basi Niko tayari kutoa Yangu yote.” Baadaye, Alikwenda msalabani bila kujifikiria hata kidogo, na kuwakomboa wanadamu wote.
kutoka katika “Maono ya Kazi ya Mungu (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kisha, katika Enzi ya Neema, Yesu alikuja kuwakomboa wanadamu wote walioanguka (sio Waisraeli pekee). Alionyesha rehema na wema kwa mwanadamu. Yesu ambaye mwanadamu alimwona katika Enzi ya Neema Alikuwa amejazwa na wema na siku zote Alikuwa mwenye upendo kwa mwanadamu, maana Alikuwa amekuja kuwakomboa wanadamu kutoka dhambini. Aliweza kuwasamehe wanadamu dhambi zao hadi pale ambapo kusulubiwa Kwake kuliwakomboa wanadamu kutoka dhambini kabisa. Wakati huo, Mungu alionekana kwa mwanadamu kwa rehema na wema; yaani, Alijitoa sadaka kwa ajili ya mwanadamu na Alisulubiwa kwa ajili ya dhambi za mwanadamu ili kwamba ziweze kusamehewa milele. Alikuwa mwenye rehema, mwenye huruma, mwenye upendo na mstahimilivu. Na wale wote waliomfuata Yesu katika Enzi ya Neema nao pia walitafuta kuwa wastahimilivu na wenye upendo katika mambo yote. Walistahimili mateso kwa muda mrefu, na hawakuwahi kulipiza kisasi hata walipopigwa, kulaaniwa au kupigwa mawe.
kutoka katika “Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili” katika Neno Laonekana katika Mwili
Wakati wa Enzi ya Neema, jina la Mungu lilikuwa ni Yesu. Kwa maneno mengine, kazi ya Enzi ya Neema ilifanywa hasa katika Jina la Yesu. Wakati wa Enzi ya Neema, Mungu Aliitwa Yesu. Yeye Alifanya kazi mpya zaidi ya Agano la Kale, na kazi yake ilimalizika kwa kusulubiwa, na ya kwamba huo ulikuwa ukamilifu wa kazi yake.
kutoka katika “Maono ya Kazi ya Mungu (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili
(3) Umuhimu wa Mungu kuchukua jina la Yehova katika Enzi ya Ufalme
Aya za Biblia za Kurejelea:
“Wewe utaitwa kwa jina jipya, jina ambalo kinywa cha Yehova kitalitamka” (Isaya 62:2).
“Yule ambaye anashinda nitamfanya awe nguzo katika hekalu lake Mungu wangu, na hatatoka nje tena: na nitaandika kwake jina lake Mungu wangu, na jina la mji wake Mungu wangu, ambao ni Yerusalemu mpya, ambao hukuja chini kutoka kwa Mungu wangu mbinguni: na nitaandika kwake jina langu jipya” (Ufunuo 3:12).
“Mimi ndiye Alfa na Omega, Mwanzo na tena mwisho, Akasema Bwana, ambaye yuko, na ambaye alikuweko, na ambaye atakuja, Mwenyezi” (Ufunuo 1:8).
“Tunakupa shukrani, Ee BWANA Mungu Mwenyezi, ambaye uko, na ulikuwa, utakuwa, kwa kuwa umeichukua nguvu yako kuu, na umetawala” (Ufunuo 11:17).
“Vitendo vyako ni vikubwa na vya ajabu, Bwana Mungu Mwenyezi; njia zako ni za haki na za kweli, wewe Mfalme wa watakatifu” (Ufunuo 15:3).
Maneno Husika ya Mungu:
Katika siku za mwisho, jina lake ni Mwenyezi Mungu—mwenye uweza, na yeye hutumia nguvu zake kumwongoza mwanadamu, kumshinda mwanadamu, kumtwaa mwanadamu, na mwishowe, kuhitimisha enzi hiyo.
kutoka katika “Maono ya Kazi ya Mungu (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kwa kuwa Mwenyezi Mungu—Mfalme wa ufalme—ameshuhudiwa, mawanda ya usimamizi wa Mungu yamejitokeza kabisa katika ulimwengu wote. Sio tu kwamba kuonekana kwa Mungu kumeshuhudiwa nchini China, lakini jina la Mwenyezi Mungu limeshuhudiwa katika mataifa yote na nchi zote. Wote wanaliita jina hili takatifu, wakitafuta kufanya ushirika na Mungu kwa njia yoyote iwezekanayo, wakiyafumbata mapenzi ya Mwenyezi Mungu na kuhudumu kwa uratibu katika kanisa. Roho Mtakatifu hufanya kazi kwa njia hii ya ajabu.
kutoka katika “Sura ya 8” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili
Ingawa Yehova, Yesu, na Masihi yote yanawakilisha Roho Wangu, majina haya yanaashiria tu enzi tofauti katika mpango Wangu wa usimamizi, nayo hayaniwakilishi katika ukamilifu Wangu. Majina wanayoniita watu duniani hayawezi kueleza kwa ufasaha tabia Yangu nzima na yote Niliyo. Ni majina tofauti tu ambayo Ninaitwa katika enzi tofauti. Na hivyo, enzi ya mwisho—enzi ya siku za mwisho—itakapofika, jina Langu litabadilika tena. Sitaitwa Yehova, au Yesu, wala Masihi, lakini nitaitwa Mwenyezi Mungu Mwenyewe mwenye nguvu, na chini ya jina hili Nitatamatisha enzi nzima. Nilijulikana kama Yehova wakati mmoja. Pia niliitwa Masihi, na wakati mmoja watu waliniita Yesu Mwokozi kwa sababu walinipenda na kuniheshimu. Lakini leo Mimi si yule Yehova au Yesu ambaye watu walimfahamu nyakati zilizopita—Mimi ni Mungu ambaye Amerejea katika siku za mwisho, Mungu ambaye Ataikamilisha enzi. Mimi ni Mungu Mwenyewe ambaye Anainuka katika miisho ya dunia, Nimejawa na tabia Yangu nzima, na Nimejawa na mamlaka, heshima na utukufu. Watu hawajawahi kushirikiana na Mimi, hawajawahi kunifahamu, na daima hawaijui tabia Yangu. Tangu uumbaji wa dunia hadi leo, hakuna mtu yeyote ambaye ameniona. Huyu ni Mungu anayemtokea mwanadamu katika siku za mwisho lakini Amejificha kati ya wanadamu. Anaishi kati ya wanadamu, ni wa kweli na halisi, kama jua liwakalo na moto unaochoma, Aliyejaa nguvu na kujawa mamlaka. Hakuna mtu au kitu chochote ambacho hakitahukumiwa kwa maneno Yangu, na mtu au kitu chochote ambacho hakitatakaswa kupitia moto unaowaka. Hatimaye, mataifa yote yatabarikiwa kwa ajili ya maneno Yangu, na pia kupondwa na kuwa vipande vipande kwa sababu ya maneno Yangu. Kwa njia hii, watu wote katika siku za mwisho wataona kuwa Mimi ndiye Mwokozi aliyerejea, Mimi ndiye Mungu Mwenyezi ambaye Anawashinda binadamu wote, nami Nilikuwa sadaka ya dhambi kwa mwanadamu wakati mmoja, lakini katika siku za mwisho Ninakuwa pia miale ya Jua linalochoma vitu vyote, na pia Jua la haki Linalofichua vitu vyote. Hivyo ndivyo ilivyo kazi Yangu ya siku za mwisho. Nilichukua jina hili nami Ninamiliki tabia hii ili watu wote wapate kuona kuwa Mimi ni Mungu mwenye haki, na Mimi ni jua linachoma, na moto unaowaka. Ni hivyo ili watu wote waweze kuniabudu, Mungu pekee wa kweli, na ili waweze kuuona uso Wangu wa kweli: Mimi si Mungu wa Wayahudi tu, na Mimi si Mkombozi tu—Mimi ni Mungu wa viumbe vyote katika mbingu na dunia na bahari.
kutoka katika “Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya ‘Wingu Jeupe’” katika Neno Laonekana katika Mwili
Katika kazi yake ya kuhitimisha enzi, tabia ya Mungu ni ile ya kuadibu na hukumu, ambayo inafichua yote ambayo si ya haki, na kuhukumu wanadamu hadharani, na kukamilisha wale ambao wanampenda kwa ukweli. Ni tabia tu kama hii ndiyo ambayo inaweza kufikisha enzi hii mwisho. Siku za mwisho tayari zimewadia. Kila kitu kitabainishwa kulingana na aina, na kitagawanywa katika makundi tofauti kulingana na asili yake. Huu ni wakati ambapo Mungu Atafichua hatima ya wanadamu na kikomo cha safari yao. Kama mwanadamu hatashuhudia kuadibu na hukumu yake, basi hakutakuwepo na mbinu ya kufichua uasi na udhalimu wao mwanadamu. Ni kwa njia ya kuadibu na hukumu ndipo mwisho wa mambo yote yatafunuliwa. Mwanadamu huonyesha tu ukweli ulio ndani yake anapoadibiwa na kuhukumiwa. Mabaya yataekwa na mabaya, mema na mema, na wanadamu watabainishwa kulingana na aina. Kupitia kuadibu na hukumu, mwisho wa mambo yote utafichuliwa, ili mabaya yaadhibiwe na mazuri yatunukiwe zawadi, na watu wote watakuwa wakunyenyekea chini ya utawala wa Mungu. Kazi hii yote inapaswa kutimizwa kupitia kuadibu kwa haki adhibu na hukumu. Kwa sababu upotovu wa mwanadamu umefika upeo wake na uasi wake umekua mbaya mno, ni haki ya tabia ya Mungu tu, ambayo hasa ni ya kuadibu na hukumu, na imefichuliwa kwa kipindi cha siku za mwisho, inayoweza kubadilisha na kukamilisha mwanadamu. Ni tabia hii pekee ambayo itafichua maovu na hivyo kuwaadhibu watu wote dhalimu. Kwa hivyo, tabia kama hii imejazwa umuhimu wa wakati, na ufunuo na maonyesho ya tabia yake ni kwa ajili ya kazi ya kila enzi mpya. Mungu hafichui tabia yake kiholela na bila umuhimu. Kama, wakati wa mwisho wa mwanadamu umefichuliwa katika kipindi cha siku za mwisho, Mungu bado anamfadhili binadamu kwa huruma na upendo usioisha, kama yeye bado ni wa kupenda mwanadamu, na kumkabili hukumu ya haki, bali anamwonyesha stahamala, uvumilivu, na msamaha, kama bado Yeye anamsamehe mwanadamu bila kujali ubaya wa makosa anayofanya, bila hukumu yoyote ya haki, basi kungekuwepo na mwisho wa usimamizi wa Mungu? Ni wakati gani tabia kama hii itaweza kuwaongoza wanadamu katika hatima inayofaa? Chukua, kwa mfano, hakimu ambaye daima ni mwenye upendo, mwenye roho safi na mpole. Anawapenda watu bila kujali dhambi wanazozifanya, na ni mwenye upendo na stahamala kwa watu bila kujali hao ni nani. Kisha ni lini ambapo ataweza kufikia uamuzi wa haki? Katika siku za mwisho, ni hukumu ya haki tu inaweza kubainisha mwanadamu na kuleta mwanadamu katika utawala mpya. Kwa njia hii, enzi nzima inafikishwa mwisho kupitia kwa tabia ya Mungu iliyo ya haki ya hukumu na kuadibu.
kutoka katika “Maono ya Kazi ya Mungu (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili
Mungu Anapopata mwili mara hii, kazi Yake ni kuonyesha tabia Yake, kimsingi kupitia kuadibu na hukumu. Akitumia haya kama msingi, Analeta ukweli zaidi kwa mwanadamu, kuonyesha njia zaidi za matendo, na hivyo Hufikia lengo Lake la kumshinda mwanadamu na kumwokoa mwanadamu kutokana na tabia yake potovu. Hili ndilo liko katika kazi ya Mungu katika Enzi ya Ufalme.
Dibaji ya Neno Laonekana katika Mwili
Wakati sauti ya ngurumo saba inatokea, kuna wokovu wa wale wanaonipenda, wanaonitamani kwa mioyo ya ukweli. Wale ambao ni Wangu na Niliowaamulia kabla na kuwateua wote wana uwezo wa kurudi kwa jina Langu. Wanaweza kusikia sauti Yangu, ambayo ni mwito wa Mungu. Hebu wale walio katika mwisho wa dunia waone ya kwamba Mimi ni mwenye haki, Mimi ni mwaminifu, Mimi ni upendo, Mimi ni huruma, Mimi ni muadhama, Mimi ni moto mkali, na hatimaye Mimi ni hukumu bila huruma.
Hebu wote walio duniani waone ya kwamba Mimi ndiye Mungu halisi Mwenyewe na Aliye mkamilifu kabisa. Watu wote wameshawishika kwa dhati na hakuna anayethubutu kunipinga tena, kunihukumu au kunisingizia tena. Vinginevyo, watakutana mara moja na laana na maafa yatawapata. Wao watalia na kusaga meno tu na wataleta uharibifu wao wenyewe.
Hebu watu wote wajue, na ijulikane hadi mwisho wa ulimwengu, ili kila mmoja na kila mtu ajue. Mwenyezi Mungu ndiye Mungu mmoja na wa kweli, wote tena na tena watapiga magoti chini kumuabudu na hata watoto ambao wamejifunza tu kuzungumza wataita “Mwenyezi Mungu”!
kutoka katika “Sura ya 35” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili
Ili kwamba katika enzi hii ya mwisho jina Langu litatukuzwa miongoni mwa Mataifa, kwamba matendo Yangu yataonekana na mataifa mengine na wataniita Mwenyezi kwa sababu ya matendo Yangu, na kwamba maneno Yangu yatatimika karibuni. Nitawafanya watu wote wajue kwamba Mimi siye tu Mungu wa Waisraeli, lakini Mimi ni Mungu wa Mataifa yote, hata mataifa yale Niliyoyalaani. Nitawafanya watu wote waone kwamba Mimi ndimi Mungu wa viumbe vyote. Hii ndiyo kazi Yangu kubwa zaidi, kusudio la mpango wa kazi Yangu katika siku za mwisho, na kazi ya pekee kutimizwa katika siku za mwisho.
kutoka katika “Kazi ya Kueneza Injili Ni Kazi ya Kuokoa Binadamu Pia” katika Neno Laonekana katika Mwili
Ijumaa, 20 Aprili 2018
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya “Wingu Jeupe”
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya “Wingu Jeupe”
Alhamisi, 21 Desemba 2017
Kwa nini Mungu Huchukua Jina la Mwenyezi Mungu Katika Enzi ya Ufalme?
Desemba 21, 2017Bwana-Yesu, Enzi-ya-Ufalme, Kuhusu-Sisi, Maswali-Yanayoulizwa-Mara-Nyingi, Mwenyezi-MunguNo comments
Kwa nini Mungu Huchukua Jina la Mwenyezi Mungu Katika Enzi ya Ufalme?
Watu wengi hawaelewi ni kwa nini, kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni kurudi kwa Bwana Yesu katika siku za mwisho, Bwana Yesu anaitwa Mwenyezi Mungu wakati Anapokuja kufanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho. Kwa nini haendelei kuitwa Bwana Yesu? Kwa kweli, Mungu ana jina jipya kila wakati Anapofanya hatua moja ya kazi Yake. Jina hili jipya linachukuliwa na Mungu Mwenyewe kama inavyofaa kazi hii–siyo kitu ambacho watu humuita Yeye kama wanavyotaka.
Jumatano, 1 Mei 2019
2. Kujua madhumuni na Umuhimu wa Kila Moja ya Hatua Tatu za Kazi ya Mungu
Mei 01, 2019Kazi-ya-Mungu, Kupata-Mwili, Neno-Laonekana-katika-Mwili, Tabia-ya-Mungu, VitabuNo comments
II. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Hatua Tatu za Kazi ya Wokovu wa Mungu kwa Wanadamu
2. Kujua madhumuni na Umuhimu wa Kila Moja ya Hatua Tatu za Kazi ya Mungu
(1) Lengo na umuhimu wa kazi ya Mungu katika Enzi ya Sheria
Maneno Husika ya Mungu:
Kazi ambayo Yehova alifanya kwa Waisraeli ilianzisha mahali pa Mungu pa asili miongoni mwa binadamu, ambapo pia palikuwa pahali patakatifu ambapo Alikuwapo. Aliwekea kazi Yake mipaka kwa watu wa Israeli. Mwanzoni, Hakufanya kazi nje ya Israeli; badala yake, Aliwachagua watu Aliowaona kuwa wa kufaa ili kuzuia eneo la kazi Yake.
Alhamisi, 22 Februari 2018
Imani za Kimsingi za Kanisa la Mwenyezi Mungu
Imani za Kimsingi za Kanisa la Mwenyezi Mungu
(1) Mafundisho ya Kanisa la Mwenyezi Mungu
Mafundisho ya Ukristo yanatoka kwa Biblia, na mafundisho ya Kanisa la Mwenyezi Mungu yanatoka kwa ukweli wote ulioonyeshwa na Mungu tangu wakati wa uumbaji wakati wa kazi ya Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme.
Jumamosi, 11 Agosti 2018
Kwa Nini Mungu Anaitwa kwa Majina Tofauti katika Enzi Tofauti?
Agosti 11, 2018Mambo-Muhimu-ya-Muumini-Mpya, Mwenyezi-Mungu, Roho-Mtakatifu, Vitabu, YesuNo comments
Sura ya 2 Ukweli wa Majina ya Mungu
2. Kwa Nini Mungu Anaitwa kwa Majina Tofauti katika Enzi Tofauti?
Maneno Husika ya Mungu:
Katika kila enzi, Mungu Anafanya kazi mpya na huitwa kwa jina jipya; Je, anawezaje kufanya kazi sawa katika enzi tofauti? Itakuwaje Yeye kugandamana na yale ya zamani? Jina la Yesu lilichukuliwa kuwa la kazi ya ukombozi, hivyo bado Yeye Anaweza kuitwa kwa jina moja wakati Atarudi katika siku za mwisho? Je, bado Yeye Atafanya kazi ya ukombozi?
Ijumaa, 16 Machi 2018
Maono ya Kazi ya Mungu (3)
Maono ya Kazi ya Mungu (3)
Mara ya kwanza Mungu alipopata mwili ilikuwa kupitia kutungwa mimba kwa Roho Mtakatifu, na ilihusiana na kazi Aliyokusudia kufanya. Jina la Yesu liliashiria mwanzo wa Enzi ya Neema. Wakati Yesu Alianza kufanya huduma Yake, Roho Mtakatifu Alianza kutoa ushuhuda kwa jina la Yesu, na jina la Yehova halikuzungumziwa tena, na badala yake Roho Mtakatifu Alianza kazi mpya hasa kwa jina la Yesu.
Jumatatu, 11 Desemba 2017
Ni Jinsi Gani Mwanadamu Aliyemfafanua Mungu katika Dhana Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?
Ni Jinsi Gani Mwanadamu Aliyemfafanua Mungu katika Dhana Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?
Mwenyezi Mungu alisema, Kazi ya Mungu inaendelea kusonga mbele, na ingawa madhumuni ya kazi Yake bado hayajabadilika, njia anazozitumia kufanya kazi zinabadilika mara kwa mara, na hivyo pia wale wanaomfuata Mungu. Zaidi iwapo kazi ya Mungu, zaidi mwanadamu anakuja kumjua kwa kina Mungu, na tabia ya mwanadamu inabadilika ipasavyo pamoja na kazi Yake.
Jumatatu, 1 Januari 2018
Kwa nini Umeme wa Mashariki Hutapakaa Kwenda Mbele na Maendeleo Yasiyozuilika?
Januari 01, 2018Bwana-Yesu, Kanisa-la-Mwenyezi-Mungu, Kuondoa-Ukungu-ili-kuona-Mwanga-wa-Kweli, Mwenyezi-Mungu, Umeme-wa-Mashariki, Unabii-wa-BibliaNo comments
Kwa nini Umeme wa Mashariki Hutapakaa Kwenda Mbele na Maendeleo Yasiyozuilika?
Kristo wa siku za mwisho amekuwa akifanya kazi Yake nchini China kwa zaidi ya miaka 20, kazi ambayo imetetemesha makundi mbalimbali ya kidini kwa kina. Swali la kufadhaisha zaidi kwa jumuiya za kidini wakati huu limekuwa: Wachungaji wengi na wazee wa kanisa katika jumuiya ya kidini wamefanya liwezekanalo kuuhukumu na kuushambulia Umeme wa Mashariki kupitia njia mbalimbali kama vile kueneza uvumi kuhusu na kuukashifu Umeme wa Mashariki.
Alhamisi, 26 Julai 2018
Mwenyezi Mungu Ndiye Bwana Yesu Aliyerudi
Sura ya 1 Mwenyezi Mungu Ndiye Mungu Mmoja wa Kweli Ambaye Aliumba Kila kitu
2. Mwenyezi Mungu Ndiye Bwana Yesu Aliyerudi
Maneno Husika ya Mungu:
Baada ya kazi ya Yehova, Yesu Alipata mwili ili Afanye kazi Yake miongoni mwa wanadamu. Kazi Yake haikutekelezwa kivyake, ila ilijengwa juu ya misingi ya kazi ya Yehova. Ilikuwa kazi ya enzi mpya baada ya Mungu kukamilisha Enzi ya Sheria. Vivyo hivyo, baada ya kazi ya Yesu kukamilika, Mungu bado Aliendeleza kazi Yake ya enzi iliyofuata, kwa sababu usimamizi wote wa Mungu huendelea mbele siku zote.
Maneno Husika ya Mungu:
Baada ya kazi ya Yehova, Yesu Alipata mwili ili Afanye kazi Yake miongoni mwa wanadamu. Kazi Yake haikutekelezwa kivyake, ila ilijengwa juu ya misingi ya kazi ya Yehova. Ilikuwa kazi ya enzi mpya baada ya Mungu kukamilisha Enzi ya Sheria. Vivyo hivyo, baada ya kazi ya Yesu kukamilika, Mungu bado Aliendeleza kazi Yake ya enzi iliyofuata, kwa sababu usimamizi wote wa Mungu huendelea mbele siku zote.
Ijumaa, 8 Desemba 2017
Uchaguzi Kutoka kwa Vifungu Vitatu vya Neno la Mungu juu ya “Maono ya Kazi ya Mungu”
Desemba 08, 2017Kazi ya Mungu, majina ya Mungu, Matamshi-ya-Kristo-wa-Siku-za-Mwisho-Chaguzi, Vitabu, YesuNo comments
Uchaguzi Kutoka kwa Vifungu Vitatu vya Neno la Mungu juu ya "Maono ya Kazi ya Mungu"
1. Yohana alianza kueneza injili ya ufalme wa mbinguni miaka saba kabla ya ubatizo wa Yesu. Kwa watu, kazi aliyoifanya ilionekana kuwa juu zaidi ya kazi ya baadaye ya Yesu, ilhali yeye alikuwa, hata hivyo, nabii tu. Hakufanya kazi au kuzungumza ndani ya hekalu, lakini katika miji na vijiji nje yake. Hii alifanya, bila shaka, miongoni mwa taifa la Wayahudi, hasa wale waliokuwa maskini.
Jumapili, 19 Mei 2019
1. Kuna tofauti ipi kati ya maneno yaliyoonyeshwa na Bwana Yesu katika Enzi ya Neema na maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu katika Enzi ya Ufalme?
Mei 19, 2019Kazi-ya-Mungu, Kumbukumbu-za-Maongezi-ya-Kristo, neema, siku-za-mwisho, VitabuNo comments
V. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Tofauti Kati ya Kazi ya Mungu ya Hukumu Katika Siku za Mwisho na Kazi Yake ya Ukombozi Katika Enzi ya Neema
1. Kuna tofauti ipi kati ya maneno yaliyoonyeshwa na Bwana Yesu katika Enzi ya Neema na maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu katika Enzi ya Ufalme?
Aya za Biblia za Kurejelea:
“Tubuni: kwa kuwa ufalme wa mbinguni u karibu” (Mathayo 4:17).
“Na kwamba toba na msamaha wa dhambi vinapaswa kuhubiriwa katika jina lake miongoni mwa mataifa yote, kuanzia Yerusalemu” (Luka 24:47).
“Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, atawaongoza hadi kwenye ukweli wote: kwa maana hatazungumza juu yake mwenyewe; bali chochote atakachosikia, atakinena: na atawaonyesha mambo yajayo” (Yohana 16:12-13).
“Na iwapo mtu yeyote atayasikia maneno yangu, na asiyaamini, Mimi sitamhukumu: kwa kuwa mimi sikuja ili niihukumu dunia, bali kuiokoa dunia. Yeye ambaye ananikataa mimi, na hayakubali maneno yangu, ana yule ambaye anamhukumu: neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho” (Yohana 12:47-48).
Maneno Husika ya Mungu:
Kazi ya Yesu ilikuwa kwa ajili ya ukombozi wa mwanadamu na kusulubiwa tu. Kwa hivyo, hakukuwa na haja Kwake kusema maneno zaidi ili kumshinda mtu yeyote. Mengi ya yale Aliyomfundisha mwanadamu yalitolewa kutoka kwa Maandiko, na hata kama kazi yake haikuzidi Maandiko, bado Aliweza kutimiza kazi ya kusulubiwa. Yake haikuwa kazi ya neno, wala kwa ajili ya kumshinda mwanadamu, lakini kwa minajili ya kumkomboa mwanadamu. Yeye Alihusika kama dhabihu ya dhambi tu kwa mwanadamu, na hakuhusika kama chanzo cha Neno kwa mwanadamu.
kutoka katika “Maono ya Kazi ya Mungu (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili
Wakati huo, Yesu alizungumza tu na wanafunzi Wake mfululizo wa mahubiri kwa Enzi ya Neema, kama jinsi ya kuweka vitendoni, jinsi ya kukusanyika pamoja, jinsi ya kuuliza kwa maombi, jinsi ya kuwatendea wengine, na mengineyo. Kazi Aliyoifanya ilikuwa hiyo ya Enzi ya Neema, na alielezea tu juu ya jinsi wanafunzi na waliomfuata wanapaswa kuweka vitendoni. Alifanya tu kazi ya Enzi ya Neema na hakuna hata moja ya siku za mwisho. Wakati Yehova aliandika sheria ya Agano la Kale kwa Enzi ya Sheria, mbona basi hakufanya kazi ya Enzi ya Neema? Mbona hakueleza wazi mapema kazi ya Enzi ya Neema? Hii haingekuwa ya manufaa kwa kukubali kwa mwanadamu? Alitabiri tu kwamba mtoto mchanga wa kiume angezaliwa na kuja mamlakani, lakini Hakutekeleza mapema kazi ya Enzi ya Neema. Kazi ya Mungu katika kila enzi ina mipaka ya wazi; Anafanya tu kazi ya enzi ya sasa na Hatekelezi hatua ifuatayo ya kazi mapema. Kwa njia hii tu kazi Yake ya kuwakilisha ya kila enzi inaweza kuletwa mbele. Yesu alizungumzia tu ishara za siku za mwisho, kuhusu jinsi ya kuwa mtulivu na jinsi ya kuokolewa, jinsi ya kutubu na kukiri, na pia jinsi ya kubeba msalaba na kuvumilia mateso; Kamwe hakuzungumza kuhusu jinsi mwanadamu katika siku za mwisho anapaswa kuingia ndani, ama jinsi ya kutafuta kukidhi matakwa ya Mungu.
kutoka katika “Ni Jinsi Gani Mwanadamu Ambaye Amemfafanua Mungu katika Dhana Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?” katika Neno Laonekana katika Mwili
Hebu kwanza tuangalie katika kila sehemu ya “Ibada Mlimani.” Haya yote yanahusiana na nini? Yaweza kusemekana kwa uhakika kwamba haya yote yameinuliwa zaidi, yana uthabiti zaidi na karibu zaidi katika maisha ya watu kuliko taratibu zile za Enzi ya Sheria. Kuzungumza katika muktadha wa kisasa, yanahusiana zaidi na matendo halisi ya watu.
Hebu tusome maudhui mahususi ya yafuatayo: Mnafaa kuzielewa vipi hali hizi za heri? Ni nini mnachofaa kujua kuhusu sheria? Ghadhabu inafaa kufasiliwa vipi? Wazinzi wanafaa kushughulikiwa vipi? Ni nini kinachosemwa, na ni sheria aina gani zipo kuhusu talaka, na ni nani anayeweza kutalikiwa na ni nani asiyeweza kutalikiwa? Na je, viapo, jicho kwa jicho, kuwapenda adui zako, maagizo kuhusu sadaka, n.k? Mambo haya yote yanahusu kila kipengele cha matendo ya imani ya mwanadamu kwa Mungu, na ufuataji wao wa Mungu. Baadhi ya desturi hizi zinatumika leo, lakini bado yapo katika hali ya kimsingi kuliko mahitaji ya sasa ya watu. Kwa kiasi kikubwa uko katika hali ya kimsingi ambao watu wanakumbana nao katika kuamini kwao katika Mungu. Tangu wakati Bwana Yesu alianza kufanya kazi, Alikuwa tayari anaanza kufanya kazi kwa tabia ya maisha ya binadamu, lakini yalitokana na msingi wa sheria. Je, sheria na misemo kuhusu mada hizi ilikuwa na uhusiano wowote na ukweli? Bila shaka zilikuwa nao! Taratibu, kanuni na ibada zote zingine za awali katika Enzi ya Neema zilikuwa na uhusiano, na tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho na bila shaka kwa ukweli. Haijalishi ni nini ambacho Mungu anaonyesha, kwa njia gani Anaonyesha, au Akitumia lugha gani, asili yake, na mwanzo wake, vyote vinatokana na kanuni za tabia Yake na kile Alicho nacho na kile Alicho. Hili halina kosa. Kwa hivyo ingawa haya mambo Aliyoyasema yanaonekana kuwa ya juujuu, bado hamwezi kusema kwamba mambo haya si ukweli, kwa sababu yalikuwa mambo ambayo yalikuwa ya lazima kwa watu katika Enzi ya Neema ili kuridhisha mapenzi ya Mungu na kutimiza mabadiliko katika tabia yao ya maisha. Unaweza kusema kwamba mambo yoyote yale katika ibada hayaambatani na ukweli? Huwezi! Kila mojawapo ya mambo haya ni ukweli kwa sababu yote yalikuwa mahitaji ya Mungu kwa mwanadamu; yote yalikuwa kanuni na mawanda yaliyotolewa na Mungu kuhusu namna ambavyo unaweza kuwa na mwenendo, na yanawakilisha tabia ya Mungu. Hata hivyo, kutokana na kiwango cha ukuaji wao katika maisha wakati huo, waliweza tu kukubali na kuyafahamu mambo haya. Kwa sababu dhambi ya mwanadamu ilikuwa bado haijatatuliwa, Bwana Yesu angeweza tu kuyatoa maneno haya, na Angeweza kutumia mafundisho mepesi kama hayo miongoni mwa aina hii ya upana ili kuwaambia watu wa wakati huo namna ambavyo walifaa kutenda, kile walichofaa kufanya, ndani ya kanuni na upana gani walifaa kufanya mambo, na vipi walivyofaa kuamini katika Mungu na kutimiza mahitaji Yake. Haya yote yaliamuliwa kulingana na kimo cha mwanadamu wakati huo. Haikuwa rahisi kwa watu wanaoishi katika sheria kuyakubali mafundisho haya, hivyo basi kile Alichofunza Bwana Yesu lazima kingebaki ndani ya mawanda haya.
kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” katika Neno Laonekana katika Mwili
Maneno ambayo Mungu Alizungumza katika enzi hii ni tofauti na yale yaliyozungumzwa katika Enzi ya Sheria, na kwa hivyo, pia yako tofauti na maneno yaliyonenwa katika Enzi ya Neema. Katika Enzi ya Neema, Mungu hakufanya kazi ya neno, lakini Alieleza tu usulubisho ili kuwakomboa binadamu wote. Biblia inaelezea tu ni kwa nini Yesu alikuwa Asulubiwe, na mateso ambayo Alipitia kwenye msalaba, na jinsi mwanadamu anapaswa kusulubiwa kwa ajili ya Mungu. Katika enzi hiyo, kazi yote iliyofanywa na Mungu ilikuwa kuhusu usulubisho. Katika Enzi ya Ufalme, Mungu katika mwili Anazungumza maneno ili kushinda wale wote wanaomwamini. Huu ni, “Neno kuonekana katika mwili”; Mungu amekuja katika siku za mwisho ili kufanya kazi hii, ambayo ni kusema, Amekuja kutimiza umuhimu wenyewe wa Neno kuonekana katika mwili. Ananena tu maneno, na majilio ya ukweli ni chache. Hii ndiyo dutu kamili ya Neno kuonekana katika mwili, na wakati Mungu katika mwili Anaponena maneno Yake, huku ndiko kuonekana kwa Neno katika Mwili, na ni Neno kuja katika mwili. “Mwanzoni kulikuwa na Neno, na Neno alikuwa na Mungu, na Neno alikuwa Mungu, na Neno likawa mwili.” Hii (kazi ya kuonekana kwa Neno katika mwili) ni kazi ambayo Mungu atatimiza katika siku za mwisho, na ni sura ya mwisho ya mpango Wake mzima wa uongozi, kwa hivyo Mungu lazima Aje duniani na kudhihirisha maneno Yake katika mwili. Yale yanayofanywa leo, yale yatakayofanywa baadaye, yale yatakayotimizwa na Mungu, hatima ya mwisho mwanadamu, wale watakaookolewa, wale watakaoangamizwa, na mengine mengi—kazi hii ambayo lazima itimizwe mwishowe imesemwa wazi, na yote ni kwa ajili ya kutimiza umuhimu halisi wa Neno kuonekana kwa mwili. Amri za utawala na katiba ambayo ilipeanwa hapo awali, wale ambao wataangamizwa, wale watakaoingia katika mapumziko—maneno haya lazima yatimizwe. Hii ni kazi iliyotimizwa kimsingi na Mungu katika mwili katika siku za mwisho. Anawafanya watu waelewe kule ambako wale waliopangiwa na Mungu wanapaswa kuwa na wale wasiopangiwa na Mungu wanapaswa kuwa, jinsi ambavyo watu Wake na wana Wake watawekwa kwenye vikundi, ni nini kitaifanyikia Uyahudi, ni nini kitaufanyikia Misri—katika siku za usoni, kila mojawapo ya maneno haya yatatimizwa. Hatua za kazi za Mungu zinaharakishwa. Mungu hutumia neno kama mbinu ya kumfichulia mwanadamu kinachopaswa kufanyika katika kila enzi, kinachopaswa kufanywa na Mungu katika mwili wa siku za mwisho, na huduma Yake ambayo inapaswa kufanywa, na maneno haya ni kwa ajili ya kutimiza umuhimu hasa wa Neno kuonekana kwa mwili.
kutoka katika “Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kile ambacho Nasema leo ni kuhukumu dhambi za watu na maovu yao; ni kulaani uasi wa watu. Udanganyifu na upotovu wao, na maneno na matendo yao, mambo yote ambayo hayako sambamba na mapenzi Yake yatapitia hukumu, na uasi wa watu unaamuliwa kuwa wenye dhambi. Ananena kulingana na kanuni za hukumu, naye anadhihirisha tabia Yake yenye haki kwa kuhukumu maovu yao, kulaani uasi wao, na kufichua nyuso zao zote mbaya.
kutoka katika “Jinsi Hatua ya Pili ya Kazi ya Ushindi Huzaa Matunda” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kazi inayofanywa na Mungu katika enzi hii ni hasa ya kutoa maneno kwa ajili ya uzima wa mwanadamu, kuweka wazi hulka ya asili ya mwanadamu na tabia ya mwanadamu iliyoharibika, uondoaji wa dhana za kidini, fikra za kinjozi, mitazamo iliyopitwa na wakati, vilevile maarifa na utamaduni wa mwanadamu. Hii ni lazima iwekwe wazi na kusafishwa kupitia maneno ya Mungu. Katika siku za mwisho, Mungu Anatumia maneno na siyo ishara na maajabu ili kumfanya mwanadamu kuwa mkamilifu. Anatumia maneno Yake kumweka wazi mwanadamu, kumhukumu mwanadamu, kumwadibu mwanadamu, na kumkamilisha mwanadamu, ili katika maneno ya Mungu, mwanadamu aje kuona hekima na wema wa Mungu, na aje kuelewa tabia ya Mungu, ili kupitia maneno ya Mungu, mwanadamu aone matendo ya Mungu.
kutoka katika “Kuijua Kazi ya Mungu Leo” katika Neno Laonekana katika Mwili
Ikifika kwa neno “hukumu,” utawaza juu ya maneno ambayo Yehova alizungumza kila mahali na pia maneno ya kukaripia ambayo Yesu aliwaambia Mafarisayo. Ingawa maneno haya ni yenye ukali, sio hukumu ya Mungu kwa mwanadamu; maneno tu ambayo yamezungumzwa na Mungu katika mazingira tofauti, yaani, mandhari tofauti, maneno haya ni tofauti kabisa na yale maneno anayonena Kristo wakati Anamhukumu mwanadamu siku za mwisho. Katika siku za mwisho, Kristo anatumia ukweli tofauti kumfunza mwanadamu, kufichua kiini cha mwanadamu, na kuchangua maneno na matendo yake. Maneno haya yanajumuisha ukweli mbalimbali, kama vile wajibu wa mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyofaa kumtii Mungu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu, jinsi mwanadamu anavyostahili kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na pia hekima na tabia ya Mungu, na kadhalika. Maneno haya yote yanalenga nafsi ya mwanadamu na tabia yake potovu. Hasa, maneno hayo yanayofichua vile mwanadamu humkataa Mungu kwa dharau yanazungumzwa kuhusiana na vile mwanadamu alivyo mfano halisi wa Shetani na nguvu ya adui dhidi ya Mungu. Mungu anapofanya kazi Yake ya hukumu, Haiweki wazi asili ya mwanadamu kwa maneno machache tu; Anaifunua, na kuishughulikia na kuipogoa kwa muda mrefu. Mbinu hizi za ufunuo, kushughulika, na kupogoa haziwezi kubadilishwa na maneno ya kawaida, ila kwa ukweli ambao mwanadamu hana hata kidogo. Mbinu kama hizi pekee ndizo huchukuliwa kama hukumu; ni kwa kupitia kwa hukumu ya aina hii pekee ndio mwanadamu anaweza kutiishwa na kushawishiwa kabisa kujisalimisha kwa Mungu, na zaidi ya hayo kupata ufahamu kamili wa Mungu. Kile ambacho kazi ya hukumu humletea mwanadamu ni ufahamu wa uso halisi wa Mungu na ukweli kuhusu uasi wake mwenyewe. Kazi ya hukumu humruhusu mwanadamu kupata ufahamu zaidi wa mapenzi ya Mungu, wa makusudi ya kazi ya Mungu, na wa mafumbo yasiyoweza kueleweka kwa mwanadamu. Pia inamruhusu mwanadamu kutambua na kujua asili yake potovu na asili ya upotovu wake, na pia kugundua ubaya wa mwanadamu. Matokeo haya yote huletwa na kazi ya hukumu, kwa maana asili ya kazi ya aina hii hasa ni kazi ya kuweka wazi ukweli, njia, na uhai wa Mungu kwa wale wote walio na imani ndani Mwake. Kazi hii ni kazi ya hukumu inayofanywa na Mungu.
kutoka katika “Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli” katika Neno Laonekana katika Mwili
Ingawa neno “neno” ni rahisi na la kawaida, neno kutoka kwenye kinywa cha Mungu mwenye mwili hutikisa dunia nzima; neno Lake hubadilisha moyo wa binadamu, fikira na tabia zee za binadamu, na sura nzee ya ulimwengu mzima. Kupitia enzi nyingi, Mungu pekee wa leo ndiye anayefanya kazi katika njia kama hiyo, na ni Yeye tu Anayeongea na kumwokoa binadamu hivyo. Kuanzia wakati huu kuendelea, binadamu huishi katika mwongozo wa neno, wakichungwa na kuruzukiwa na neno. Binadamu wote wanaishi katika ulimwengu wa neno, wanaishi katika laana na baraka za neno la Mungu, na hata kuna binadamu zaidi wanaoishi chini ya hukumu na kuadibu kwa neno. Maneno haya na kazi hii vyote ni kwa minajili ya wokovu wa binadamu, kwa minajili ya kutimiza mapenzi ya Mungu, na kwa minajili ya kubadilisha sura asilia ya ulimwengu wa uumbaji wa kale. Mungu aliuumba ulimwengu kwa neno, huwaongoza wanadamu kote ulimwenguni kwa neno, na pia hushinda na kuwaokoa binadamu kwa neno. Hatimaye, Yeye atatumia neno ili kuutamatisha ulimwengu mzima wa kale. Ni hapo tu ndipo mpango wa usimamizi unapokuwa mkamilifu kabisa.
kutoka katika “Enzi ya Ufalme Ndiyo Enzi ya Neno” katika Neno Laonekana katika Mwili
Wakati huo, Yesu alifanya kazi kubwa ambayo haikueleweka kwa wanafunzi Wake, na kusema mengi kwamba watu hawakuelewa. Hii ni kwa sababu, wakati huo, Hakutoa maelezo. … Yesu hakuja kumkamilisha na kumpata mwanadamu, lakini kufanya awamu moja ya kazi: kuleta injili ya ufalme wa mbinguni na kukamilisha kazi ya kusulubiwa—na punde tu Yesu Aliposulubishwa, kazi Yake ilifika mwisho kamili. Lakini kwa awamu iliyoko sasa—kazi ya ushindi—maneno mengi zaidi lazima yasemwe, kazi nyingi zaidi lazima ifanywe, na lazima kuwe na hatua nyingi. Hivyo pia ni lazima siri za kazi ya Yesu na Yehova zitafichuliwa, ili wanadamu wote waweze kuwa na ufahamu na uwazi wa imani yao, kwa kuwa hii ni kazi ya siku za mwisho, na siku za mwisho ni mwisho wa kazi ya Mungu, wakati wa kuhitimisha kazi hii. Hii awamu ya kazi itakufafanulia sheria ya Yehova na ukombozi wa Yesu, na ni hasa ili uweze kuelewa kazi nzima ya mpango wa usimamizi wa Mungu wa miaka elfu sita, na kuelewa kusudi la kazi zote Alizozifanya Yesu na maneno Aliyoyasema, na hata upofu wako wa imani kwenye na katika ibada ya Biblia. Yote haya yatakuwezesha kujua. Wewe utakuja kufahamu kazi anayoifanya Yesu na kazi ya Mungu leo; utaelewa na kushuhudia ukweli wote, uzima, na njia. Katika awamu ya kazi Aliyoifanya Yesu, kwa nini Yesu Aliondoka bila kumaliza kazi ya Mungu? Kwa sababu awamu ya kazi ya Yesu haikuwa kazi ya kumalizia. Wakati Yeye Alisulubishwa msalabani, maneno Yake pia yalifika mwisho; baada ya kusulubiwa kwake, kazi Yake kwa hivyo ilimalizika. Awamu ya sasa ni tofauti. Ni baada tu ya maneno hayo kusemwa hadi mwisho na kazi nzima ya Mungu iwe imehitimika ndipo kazi yake itakapokuwa imemalizika. Wakati wa awamu ya kazi ya Yesu, kulikuwa na maneno mengi yaliyobakia bila kusemwa, au ambayo hayakuwa yameelezwa kikamilifu kwa ufasaha. Waama, Yesu hakujali Alichosema au kile ambacho hakusema, kwa kuwa huduma yake haikuwa huduma ya maneno; na hivyo baada ya Yeye kusulubishwa msalabani Aliondoka. Awamu hiyo ilikuwa hasa kwa ajili ya kusulubiwa, na ni tofauti na awamu ya sasa. Awamu ya kazi hii ni hasa kwa ajili ya kukamilisha, kufumbua, na kuleta kazi yote kwenye hitimisho. Kama maneno hayasemwi hadi tamati yake kabisa, hakutakuwa na mbinu ya kuhitimisha kazi hii, kwa kuwa awamu hii ya kazi yote inafikishwa mwisho na kukamilika kwa kutumia maneno. Wakati huo, Yesu Alifanya kazi kubwa isiyoeleweka na mwanadamu. Akaondoka kimyakimya, na leo bado kunao wengi wasioelewa maneno Yake, ambao ufahamu wao ni potofu lakini bado unaaminika nao kwamba ni sahihi, ambao hawajui kuwa wao si sahihi. Mwishoni, awamu hii ya sasa itafikisha kazi ya Mungu mwisho ulio kamilifu, na kutoa hitimisho Lake. Wote watakuja kufahamu na kujua mpango wa usimamizi wa Mungu. Dhana zilizo ndani ya mwanadamu, nia yake, fahamu yake potofu, dhana zake kuhusu kazi ya Yehova na Yesu, maoni yake kuhusu watu wa Mataifa mengine na michepuko yake ingine na makosa yake yatarekebishwa. Na mwanadamu ataelewa njia yote ya haki ya uzima, na kazi yote anayofanya Mungu, na ukweli wote. Wakati hayo yatafanyika, awamu hii ya kazi itafikia kikomo.
kutoka katika “Maono ya Kazi ya Mungu (2)” katika Neno Laonekana katika Mwili
Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kondoo wa Mungu Huisikia Sauti ya Mungu