Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Haleluya! Twakushukuru na kukusifu Wewe, Mwenyezi Mungu! Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Ukaribisheni Urejeaji wa Bwana Yesu | Sifa na Ibada “Mungu Ameleta Utukufu Wake Mashariki”

Mungu aliipa Israeli utukufu Wake kisha Akauhamisha mbali na pale, na kuwaleta Waisraeli na kuwaleta watu wote Mashariki. Mungu amewaelekeza wote kwenye mwanga ili waweze kuungana tena na kuwa pamoja na mwanga, wasilazimike kuutafuta tena, kuutafuta mwanga.

Je, Biblia ndiye Bwana, au ni Mungu? | “Bwana Wangu Ni Nani” ( Filamu za Injili )

Liu Zhizhong ni mzee katika kanisa moja la mtaani la nyumba nchini China. Amekuwa muumini kwa zaidi ya miaka 30, na amesisitiza bila kukoma kwamba “Biblia ni ufunuo wa Mungu,” “Biblia inamwakilisha Mungu, kuamini katika Mungu ni kuamini katika Biblia, kuamini katika Biblia ni kuamini katika Mungu.”

Karibu Kurudi kwa Bwana Yesu | Drama ya Muziki “ Kwaya ya Injili ya Kichina Onyesho la 19” | Haleluya

Mungu ametutunza daima–Yeye amesikiliza maombi yetu! Anajua tumekuwa tukitamani kurejea Kwake! Sasa kwa hakika Amerejea! Tunasubiri nini bado? Tafadhali endelea kutazama drama yenye muziki ya Kanisa la Mwenyezi Mungu—Kila Taifa Humwabudu Mungu wa Vitendo!

NYENDO ZA MATESO YA KIDINI NCHINI CHINA (Christian Videos) swahili

Wakristo wanaoteswa katika filamu hii ni watu kutoka kwa vikundi vya kidini na madhehebu tofauti ambao walitafuta ukweli, na ambao waliisikia sauti ya Mungu na hivyo wakarudi kwa Mwenyezi Mungu.

Inaonyesha machapisho yaliopangwa kwa tarehe ya hoja neema. Panga kwa uhusiano Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliopangwa kwa tarehe ya hoja neema. Panga kwa uhusiano Onyesha machapisho yote

Jumanne, 17 Septemba 2019

Wimbo Mpya wa Kuabudu 2019 | “Kristo wa Siku za Mwisho Ameleta Enzi ya Ufalme” (Swahili Gospel Song)


Wimbo Mpya wa Kuabudu 2019 | “Kristo wa Siku za Mwisho Ameleta Enzi ya Ufalme” (Swahili Gospel Song)

Yesu alipokuja katika ulimwengu wa mwanadamu, Akatamatisha Enzi ya Sheria, Alileta Enzi ya Neema. Mungu mara nyingine akakuwa mwili katika siku za mwisho. Akitamatisha Enzi ya Neema, Alileta Enzi ya Ufalme. Wote wanaokubali kupata mwili kwa Mungu kwa mara ya pili wataongozwa katika Enzi ya Ufalme na kupokea uongozi Wake. Baada ya mwanadamu kusamehewa dhambi zake, Mungu alirudi mwilini kumwongoza. Atamwongoza mwanadamu kuingia katika enzi mpya. Ameanza kazi ya hukumu ili kumleta mwanadamu katika ulimwengu wa juu zaidi. Wote wanaotii utawala Wake watavuna ukweli wa juu na baraka kuu. Ee wataishi katika mwangaza! Na kupata njia, ukweli, na uzima! Yesu alifanya kazi nyingi kati ya wanadamu. Ukombozi wa wanadamu wote ndio kazi aliyomaliza pekee. Aligeuka sadaka ya mwanadamu ya dhambi, lakini hakumwondolea mwanadamu tabia yake yote potovu, upotovu wote wa mwanadamu. Kumwokoa mwanadamu kutoka kwa Shetani kulimaanisha Yesu alilazimika kuchukua dhambi za mwanadamu, lakini kazi kubwa zaidi ya Mungu ilihitaji kumwondolea mwanadamu upotovu wa Shetani. Baada ya mwanadamu kusamehewa dhambi zake, Mungu alirudi mwilini kumwongoza. Atamwongoza mwanadamu kuingia katika enzi mpya. Ameanza kazi ya hukumu ili kumleta mwanadamu katika ulimwengu wa juu zaidi. Wote wanaotii utawala Wake watavuna ukweli wa juu na baraka kuu. Ee wataishi katika mwangaza! Na kupata njia, ukweli, na uzima! kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya
Unaweza Pia Kupenda : Wimbo wa Injili "Kiini cha Kristo Ni Mungu" | Differences Between the True Christ and False Christs

Jumatatu, 2 Septemba 2019

Maneno ya Mungu : Sura ya 94

Maneno ya Mungu : Sura ya 94

Narudi Sayuni pamoja na wazaliwa Wangu wa kwanza—kweli mnaelewa maana ya kweli ya maneno haya? Nimewakumbusha tena na tena kwamba Mimi nataka mkue haraka ili mtawale na Mimi. Je, mnakumbuka? Vitu hivi vyote vinahusiana moja kwa moja na kupata mwili Kwangu. Kutoka Sayuni Nilikuja duniani katika nyama ili Nipate kupitia nyama kundi la watu ambao ni wa akili moja na Mimi, na kisha turudi Sayuni.

Jumamosi, 3 Agosti 2019

Maneno ya Mungu | Sura ya 97

Maneno ya Mungu | Sura ya 97

Nitafanya kila mtu aone matendo Yangu ya ajabu na kusikia maneno Yangu ya hekima. Ni lazima iwe kila mtu na ni lazima iwe juu ya kila suala. Hii ni amri Yangu ya utawala na ni ghadhabu Yangu. Nitahusisha kila mtu na kila jambo ili watu wote kutoka mwisho mmoja wa ulimwengu hadi mwingine wataona kwa macho yao wenyewe, la sivyo Sitaacha kamwe.

Jumapili, 28 Julai 2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 98

Sauti ya Mungu | Sura ya 98

Mambo yote yatakuja juu ya kila mmoja wenu, na yatawawezesha kujua zaidi juu Yangu na kuwa na uhakika zaidi juu Yangu. Yatawawezesha kunijua, Mungu mmoja Mwenyewe, kunijua Mimi Mwenye uweza, kunijua Mimi Mungu Mwenyewe mwenye mwili. Baadaye, Nitatoka katika mwili, Nirudi Sayuni, Nirudi katika nchi nzuri ya Kanaani, ambayo ni makazi Yangu, ndiyo hatima Yangu, na ndio msingi ambao niliumba vitu vyote.

Jumatatu, 22 Julai 2019

Sauti ya Mungu | sura ya 99

Sauti ya Mungu | sura ya 99

Kwa sababu mwendo wa kazi Yangu unaongeza kasi, hakuna anayeweza kuenda mwendo sawa na nyayo Zangu, na hakuna anayeweza kupenya akili Yangu, lakini hii ndiyo njia tu ambayo lazima isafiriwe. Hii ni “wafu” yaani wakati Ninapoongea kuhusu kufufuliwa kutoka kwa wafu (inarejelea kukosa uwezo wa kufahamu mapenzi Yangu, kukosa uwezo wa kuelewa kile Ninachomaanisha kutoka kwa maneno Yangu. Haya ni maelezo mengine ya “wafu”, na hayamaanishi kutelekezwa na Roho Wangu).

Jumanne, 16 Julai 2019

Maneno ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 101

Maneno ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 101

Sitakuwa mwenye huruma kwa yeyote anayeingilia usimamizi Wangu ama anayejaribu kuiharibu mipango Yangu. Kila mtu anapaswa kuelewa kile Ninachomaanisha kutoka kwa maneno Ninayosema na lazima aelewe vizuri kile Ninachozungumzia. Kwa kuzingatia hali iliyopo, kila mtu anapaswa kujichunguza: Ni wajibu gani unaotekeleza? Unaishi kwa ajili Yangu, au unamtumikia Shetani? Je, kila moja ya matendo yako hutoka

Jumamosi, 13 Julai 2019

Maneno ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 102

Maneno ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 102

Nimeongea hadi kwa kiwango fulani na kufanya kazi hadi kwa kiwango fulani; ninyi nyote mnapaswa kuelewa mapenzi Yangu na kwa viwango tofauti muweze kuzingatia mzigo Wangu. Sasa ndicho kipindi muhimu kutoka katika mwili kuingia katika dunia ya roho, na ninyi ndio watangulizi kwa kutagaa enzi, wanadamu wa ulimwengu wanaovuka miisho ya ulimwengu. Ninyi ni wapendwa Wangu zaidi; ninyi ndio Ninaowapenda.

Alhamisi, 4 Julai 2019

Maneno ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 106

Maneno ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 106

Wale wasioyajua maneno Yangu, wale wasioujua ubinadamu Wangu wa kawaida, na wale wanaokataa uungu Wangu wote wataangamizwa hadi wasikuwepo. Hakuna atakayeachiliwa kutokana na hili, na wote lazima wapitie hili kwa sababu ni amri Yangu ya utawala, na ndicho kifungu kikali zaidi cha amri Yangu. Wale wasioyajua maneno Yangu ni wale ambao wamesikiliza yale ambayo Nimesema wazi, ilhali bado hawayajui, kwa maneno mengine wale ambao hawaelewi masuala ya kiroho (kwa kuwa Sijaumba sehemu hii ya mwili kwa ajili ya wanadamu, Sihitaji mengi kutoka kwao; Nahitaji tu kwamba wasikilize maneno Yangu na kisha wayaweke katika matendo).

Jumatano, 3 Julai 2019

Maneno ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 107

Maneno ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 107

Wakati maneno Yangu ni makali kwa kiwango fulani, watu wengi huondoka kwa sababu ya maneno Yangu. Ni wakati huu hasa ambapo wazaliwa Wangu wa kwanza wanafichuliwa. Nimesema kuwa Sitafanya lolote, lakini Nitatumia tu maneno Yangu kutimiza mambo yote. Ninatumia maneno Yangu kuwaangamiza wote ambao Ninawachukia, na pia Ninatumia maneno Yangu kuwakamilisha wazaliwa Wangu wa kwanza. (Maneno Yangu yatakaponenwa, ngurumo saba zitatoa sauti, na wakati huo wazaliwa Wangu wa kwanza pamoja na Mimi tutabadili sura na kuingia katika ulimwengu wa kiroho.)Niliposema Roho Wangu hufanya kazi binafsi, Nilichomaanisha ni kuwa maneno Yangu hutimiza yote, na kupitia kwa hili mtu anaweza kuona kwamba Mimi ni mwenyezi.

Jumanne, 2 Julai 2019

Maneno ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 108

Maneno ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 108

Ndani Yangu, wote wanaweza kupata raha na wote wanaweza kuwa huru. Wale walio nje Yangu hawawezi kupata uhuru na furaha kwa sababu Roho Wangu hayuko pamoja na watu hawa. Watu hawa wanaitwa wafu wasio na roho. Nami Nawaita wale walio ndani Yangu watu walio hai wenye roho. Wao ni Wangu, na watarudi kwenye kiti Changu cha enzi. Wale ambao hutoa huduma na wale ambao ni wa ibilisi ni wafu wasio na roho, nao wanapaswa kuangamizwa hadi wawe katika hali ya kutokuwepo. 

Jumamosi, 29 Juni 2019

Maneno ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 110

Maneno ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 110

Kila kitu kitakapofichuliwa utakuwa wakati ambapo Nitapumzika, na hata zaidi, utakuwa wakati ambapo kila kitu kitakuwa sawa. Mimi hufanya kazi Yangu binafsi; Mimi hupanga kila kitu na kusafidi kila kitu Mwenyewe. Nitakapotoka Sayuni na Nitakaporejea, wazaliwa Wangu wa kwanza watakapokuwa wamekamilishwa na Mimi, Nitakuwa Nimemaliza kazi Yangu kubwa. Katika mawazo ya watu kitu ambacho kinafanywa ni sharti kiweze kuonekana na kuguswa, lakini jinsi Ninavyoona, kila kitu ni kikamilifu wakati ambapo Ninafanya mpango Wangu.

Jumatano, 19 Juni 2019

Maneno ya Mwenyezi Mungu | sura ya 118



Maneno ya Mwenyezi Mungu | sura ya 118

Yeyote atakayeinuka kumshuhudia Mwana Wangu, Nitampa neema; yeyote ambaye hatainuka kumshuhudia Mwana Wangu, ila badala yake apinge na kutumia dhana za mwanadamu ili Amtathmini, Nitamwangamiza. Lazima wote waone waziwazi! Kumshuhudia Mwana Wangu ni kitendo cha kunicha nako kunayaridhisha mapenzi Yangu. Usimheshimu tu Baba lakini umdhulumu na kumkandamiza Mwana. Wale wanaofanya hivyo ni wa dhuria ya joka kuu jekundu na Sihitaji watu duni kama hawa kumshuhudia Mwanangu; Nitawaangamiza katika shimo lisilo na mwisho. Nawataka watendaji huduma waaminifu na wa kweli kutoa huduma kwa Mwanangu, na Simhitaji yeyote kati ya wengine wote.

Jumatatu, 17 Juni 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | sura ya 119

  Matamshi ya Mwenyezi Mungu | sura ya 119

lazima nyote muelewe nia Zangu, nyote mnapaswa kuelewa hali Yangu ya moyo. Sasa ni wakati wa kujiandaa kurudi Sayuni, sina mawazo ya lolote isipokuwa hili. Mimi Ninatumaini tu kwamba Ninaweza kukutana nanyi siku moja hivi karibuni, na kutumia kila dakika na kila sekunde pamoja nanyi katika Sayuni. Mimi Naichukia kabisa dunia, Nauchukia kabisa mwili, na Mimi Namchukia kabisa hata zaidi kila binadamu duniani; Sina nia ya kuwaona, kwa sababu wote ni kama mapepo, bila hata chembe ya asili ya binadamu; Sina nia ya kuishi duniani, Mimi Nawachukia kabisa viumbe wote, Mimi Nawachukia kabisa wote ambao ni wa mwili na damu. Nchi yote inavunda kifo; Mimi Nataka kurudi Sayuni mara moja, ili kuiondoa harufu yote mbaya ya maiti kutoka dunia, na kufanya dunia yote ijae sifa kwa ajili Yangu.

Jumamosi, 15 Juni 2019

Kuzaliwa Upya Kupitia Neno la Mungu

Ushuhuda wa Maisha, Wakristo, Kanisa la Mwenyezi Mungu

Wang Gang Mkoa wa Shandong
Mimi ni mkulima na kwa sababu familia yangu ni maskini, daima ilinibidi nisafiri kwenda kote kutafuta kazi za muda ili kupata pesa; nilidhani kuwa ningeweza kujipatia maisha mazuri kupitia kazi yangu ya kimwili. Hata hivyo, kwa uhalisi, niliona kuwa hapakuwa na hakikisho la haki za kisheria za wafanyakazi wahamiaji kama mimi; mshahara wangu mara nyingi ulizuiliwa bila sababu yoyote. Mara kwa mara nilidanganywa na kutumiwa na wengine kwa faida yao. Baada ya kazi ngumu ya mwaka mmoja, sikupokea kile nilichopaswa kupokea. Nilihisi kwamba ulimwengu huu kwa kweli ulikuwa wa giza! Watu hutendeana kama wanyama ambapo wenye nguvu huwawinda walio dhaifu; wao hushindana wenyewe kwa wenyewe, kupigana kwa kukaribiana sana, na sikuwa na mahali pa usalama kwendelea kuishi jinsi hii. Katika maumivu mno na mfadhaiko wa roho yangu, na wakati nilipokuwa nimepoteza imani katika maisha, rafiki yangu alishirikiana wokovu wa Mwenyezi Mungu nami. Tangu wakati huo, nilikutana mara kwa mara, kusali na kuimba pamoja na ndugu wa kiume na wa kike; tuliwasiliana ukweli, na tulitumia uwezo wetu ili kufidia udhaifu wa mwingine. Nilijihisi mwenye furaha sana na aliyekombolewa. Katika Kanisa la Mwenyezi Mungu, niliona kwamba ndugu wa kiume na wa kike hawakujaribu kushindana kwa akili au kufanya utofautishaji wa kijamii; wote walikuwa wazi kabisa na walipatana wenyewe kwa wenyewe. Kila mtu alikuwa hapo kutafuta ukweli kwa bidii ili kuziacha tabia zao potovu, na kuishi kama wanadamu na kupata wokovu. Hili liliniwezesha kupitia furaha katika maisha na kuelewa umuhimu na thamani ya maisha. Kwa hiyo, niliamua kuwa ni lazima nieneze injili na kuwaruhusu watu zaidi wanaoishi gizani kuja kwa Mungu ili kupokea wokovu Wake na kuona mwanga tena. Kwa hiyo, nilijiunga na wale wa kutangaza injili na kumshuhudia Mungu. Lakini bila kutarajia, nilikamatwa na serikali ya CCP kwa kuhubiri injili na kupitia unyama mno wa mateso, utendewaji wa kikatili na kifungo cha jela.
Ilikuwa wakati wa alasiri katika majira ya baridi ya mwaka wa 2008, wakati dada wawili na mimi tulipokuwa tukiishuhudia kazi ya Mungu katika siku za mwisho kwa mlengwa wa injili, tuliripotiwa na watu waovu. Maafisa sita wa polisi walitumia udhuru wa haja ya kuangalia vibali vya makazi yetu ili kuingia kwa nguvu katika nyumba ya mlengwa wa injili. Walipokuwa wakiingia mlangoni, walisema kwa sauti kubwa: “Msisonge!” Wawili wa wale polisi waovu walionekana kuwa wazimu kabisa waliponirukia; mmoja wao alikamata kwa nguvu nguo juu ya kifua changu na mwingine akamata mikono yangu kwa nguvu na kutumia nguvu zake zote ili kuikaza nyuma yangu, kisha akaniuliza kwa ukali: “Unafanya nini? Unatoka wapi? Jina lako ni nani?” Nikauliza kwa kujibu: “Unafanya nini? Unanikamatia nini?” Waliposikia nikisema hivi, walikasirika kweli na wakasema kwa ukali: “Haijalishi sababu ni nini, wewe ndiwe tunayetafuta na unakuja nasi!” Baadaye, wale polisi waovu wakanichukua pamoja na wale dada wawili, wakatusukuma ndani ya gari la polisi na kutupeleka kwa kituo cha polisi cha mahali pale pale.
Baada ya kufika kwa kituo cha polisi, wale polisi waovu walinichukua na kunifungia ndani ya chumba kidogo; waliniamuru nichutame sakafuni na kunipangia watu wanne wanichunge. Kwa sababu nilikuwa nimechuchumaa kwa muda mrefu, nikawa nimechoka sana kiasi kwamba sikuweza kustahimili. Papo hapo nilijaribu kusimama, wale polisi waovu walinijia mbio mbio na kugandamiza kichwa changu chini ili kunizuia kusimama. Ilikuwa tu hadi wakati wa usiku walipokuja kunipekua na kuniruhusu kusimama; walipokosa kupata chochote katika utafutaji wao, wote waliondoka. Muda mfupi baadaye, nikasikia mayowe yenye kutia hofu ya mtu aliyekuwa akiteswa katika chumba cha pili, na wakati huo, niliogopa sana: Sijui ni mateso gani na matendo katili watakayotumia kwangu baadaye! Nilianza kumwomba Mungu kwa moyo wangu kwa dharura: “Ee Mwenyezi Mungu, ninaogopa sana hivi sasa, naomba Unipe imani na nguvu, nifanye imara na jasiri ili niweze kuwa shahidi Kwako. Kama siwezi kuvumilia mateso yao na matendo ya ukatili, kama itanilazimu kujiua kwa kuuma ulimi wangu, sitawahi kukusaliti Wewe kama Yuda!” Baada ya kuomba, niliyafikiria maneno ya Mungu, “Msiogope, Mwenyezi Mungu wa majeshi hakika atakuwa pamoja nawe; Yeye anawasaidia na Yeye ni ngao yenu” (“Sura ya 26” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili). Naam, Mwenyezi Mungu ndiye tegemeo langu na Yeye yu pamoja nami; ni nini kingine cha kuogopwa? Ninahitaji kumtegemea Mungu ili kupigana na Shetani. Maneno ya Mungu yaliondoa woga kutoka moyoni mwangu, na moyo wangu uliwekwa huru.
Usiku huo, polisi wanne wa kishetani walinijia na mmoja wao akanielekeza na kuguta: “Bila shaka tulishika samaki mkubwa! Ninyi waumini wa Mwenyezi Mungu mnavuruga utaratibu wa jamii, na mnavunja sheria za kitaifa….” Aliguta alipokuwa akinisukuma ndani ya chumba cha mateso kwa ghorofa ya pili, akiniamuru nichuchumae. Chumba cha mateso kiliandaliwa na aina zote za vyombo vya mateso kama vile kamba, vijiti vya mbao, virungu, mijeledi, bunduki, nk. Vilikuwa vimepangwa kwa machafuko. Akiwa na uso uliojikunja na macho yaliyowaka kwa hasira, polisi mmoja mwovu alizishika nywele zangu kwa mkono mmoja, na kirungu cha umeme, ambacho kilitoa sauti za dhoruba za “kushambulia na kuzibua” kwa ule mkono mwingine, na akafanya madai ya kuitishia habari: “Ni watu wangapi walio katika kanisa lenu? Eneo la mkutano wenu liko wapi? Ni nani anayesimamia? Ni watu wangapi walio katika sehemu hiyo wakihubiri Injili? Ongea! Vinginevyo, utapata kinachokuja!” Nikaangalia hatari iliyotisha ya kirungu cha umeme na nikaangalia tena kwa chumba kilichojaa vyombo vya mateso; sikuweza kujizuia kuhisi fadhaa na kuogopa. Sikujua kama ningeweza kuyashinda mateso haya. Katika tu wakati huu muhimu, nilifikiria maneno ya Mwenyezi Mungu yakisema: “Lazima pia unywe kutoka kwenye kikombe kikali nilichonywea Mimi (hili ndilo alilomwambia baada ya kufufuka), lazima wewe pia utembee njia niliyotembea Mimi …” (“Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Nilitambua kwamba hiki kilikuwa kitu ambacho Mungu alituaminia na ilikuwa ni njia ya maisha ambayo Mungu binafsi alituanzishia. Katika kuitembea njia ya kumwamini Mungu na kutafuta ukweli, bila shaka ni lazima mtu apitie mateso na kuvunjika moyo. Hili ni jambo lisiloepukika, na mwishowe, shida hizi huleta baraka kutoka kwa Mungu. Ni kwa njia ya mateso tu watu wanapoweza kupokea njia ya ukweli iliyotolewa na Mungu, na ukweli huu ni uzima wa milele, ambao hutolewa na Mungu. Napaswa kutembea katika nyayo za Mungu na kukabiliana na jambo hili kwa ujasiri; sipaswi kuwa na woga au hofu. Katika kufikiria jambo hili, moyo wangu mara moja ulizalisha aina fulani ya nguvu na nikasema kwa sauti kubwa: “Ninaamini tu katika Mwenyezi Mungu, sijui chochote kingine!” Wakati polisi muovu aliposikia jambo hili, alivurugika na kunidukua kwa nguvu kwa upande wa kushoto wa kifua changu na kirungu hicho cha umeme. Alinishtua kwa karibu dakika moja. Mara moja nilisikia kama damu katika mwili wangu ilikuwa imechemshwa; nilikuwa na maumivu yasiyovumilika kutoka kwa kichwa hadi kwa mguu na nikabiringika nikipiga mayowe sakafuni. Bado hakutaka kuniacha na ghafla akaanza kunivuta na akatumia kirungu kuniinua kwa kidevu changu, akiguta: “Sema! Hutakiri chochote?” Aliguta na kunidukua upande wa kulia wa kifua changu na kirungu cha umeme, nilichomwa na umeme vibaya sana kiasi kwamba nilikuwa nikitetemeka kutoka kichwa hadi mguu. Baadaye mwili uliuma vibaya sana kiasi kwamba nilizirai kama nimelala sakafuni bila kujongea. Sikujua ni muda gani uliokuwa umepita, lakini niliamka yule polisi muovu akisema: “Je! Unajifanya kuwa mfu? Unajifanya! Endelea kujifanya!” Walinidukua tena na kirungu kwa uso na kunipiga teke kwa paja. Baadaye, waliniburuta na kuniuliza kwa ukali: “Je, utaniambia!?” Bado sikujibu. Kisha hao polisi waovu walinipiga kikatili kwa uso wangu kwa ngumi zao na jino langu moja liling’olewa, jino jingine liligongwa hadi likalegea. Mara moja mdomo wangu ulianza kuvuja damu. Katika kukabiliwa na mateso ya kichaa ya pepo hawa, niliogopa tu kwamba ningemsaliti Mungu kwa sababu ya kutoweza kuyahimili mateso yao. Wakati huu, nilifikiri tena juu ya maneno ya Mungu, “Kutoka kwa nje, wale walio na mamlaka wanaweza kuonekana kuwa waovu, lakini msiogope, kwa kuwa hii ni kwa sababu mna imani kidogo. Almuradi imani yenu ikue, hakuna kitu kitakachokuwa kigumu mno” (“Sura ya 75” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yalinipa imani na nguvu tena, na niligundua kuwa ingawa hawa polisi waovu mbele yangu walikuwa na kichaa na bila nidhamu, walipangwa na mkono wa Mungu. Wakati huo, Mungu alikuwa akiwatumia kupima imani yangu. Alimradi niliegemea imani na kumtegemea Mungu na sikukubali kushindwa nao, bila kuzuilika wangeshindwa kwa aibu. Katika kufikiri juu ya hili, nilikusanya nguvu zangu zote za mwili wangu na nikajibu kwa sauti kuu: “Kwa nini mmenileta hapa? Kwa nini mnanishtua kwa umeme kwa kirungu cha umeme? Ni kosa gani nimelifanya?” Yule polisi muovu kwa ghafla akawa mtu aliyeshtuka kiasi cha kutowaza na kukandamizwa sana na dhamiri ya hatia. Alianza kugugumiza: “Mimi … mimi … Sikupaswa kukuletea hapa?” Kisha akaondoka kwa aibu. Katika kuona hali ya aibu ya mtanziko wa Shetani, niliguswa hadi nikalia. Katika mashaka haya, kwa kweli nilipitia nguvu na mamlaka ya maneno ya Mwenyezi Mungu. Alimradi neno la Mungu linawekwa katika vitendo na kufuatwa, basi Mungu atakutunza na kukukinga na nguvu za Mungu zitaandamana nawe. Wakati huo huo, nilijihisi ninawiwa na Mungu kwa sababu ya jinsi nilivyokuwa na imani kidogo. Baadaye, afisa mmoja mrefu wa polisi aliingia na kunijia na akasema: “Unapaswa tu kutuambia ni wapi familia yako huishi na ni watu wangapi walio katika familia yako, na tutakuachilia mara moja.” Alipoona kwamba singesema chochote, alivurugika na kukamata mkono wangu kwa nguvu na kuulazimisha mkono wangu kutia alama kwa ungamo la mdomo walilokuwa wameandika. Niliona kwamba huo ungamo la mdomo halikuwa vile niliyowaambia, lilikuwa ni ushahidi ghushi na wa bandia. Nilijawa na hasira ya haki na kulishika na kulirarua vipande vipande. Yule polisi muovu mara moja aliingiwa na hasira na kunipiga na ngumi yake upande wa kushoto wa uso wangu. Kisha akanipiga makofi mara mbili katika uso kwa nguvu sana kiasi kwamba nilishikwa na kizunguzungu. Baadaye, walinipeleka kwa chumba kidogo nilichokuwemo awali.
Baada ya kurudi kwa kile chumba kidogo, nilichubuliwa na kugongwagongwa sana, maumivu yalikuwa yasiyovumilika. Moyo wangu haukuweza kujizuia kuzalisha hisia ya huzuni na udhaifu: Kwa nini waumini wanapaswa kuteseka jinsi hii? Nilihubiri Injili na nia njema za kuwaruhusu watu kuutafuta ukweli na kuokolewa, na bila kutarajia nimepitia mateso haya. Katika kufikiri juu ya hili, nilihisi zaidi kuwa nilikuwa nimekosewa. Katika maumivu yangu, nilifikiria maneno ya Mungu: “Kama binadamu, unapaswa kutumia rasilmali kwa ajili ya Mungu na kuvumilia kila mateso. Unapaswa kukubali kwa furaha na kwa hakika mateso kidogo unayopitia leo na kuishi maisha yenye maana, kama Ayubu, kama Petro. … Ninyi ni watu mnaofuatilia njia sahihi, wale wanaotafuta maendeleo. Ninyi ni watu ambao huinuka katika nchi ya joka kuu jekundu, wale ambao Mungu huwaita wenye haki. Je, hayo si maisha yenye maana zaidi?” (“Utendaji (2)” katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mwenyezi Mungu yalivutia hisia kubwa kutoka kwa wangu. Ndio, Mungu alininyunyizia na kunipa maneno Yake makarimu ya uzima, Ameniruhusu kufurahia neema Yake nyingi bure na kuniruhusu kujua siri za ukweli ambazo hakuna mtu yeyote tangu vizazi vya zamani amezielewa. Hii ni baraka maalum ambayo Mungu amenipa. Napaswa kushuhudia kwa Mungu na kuvumilia maumivu yote kwa ajili ya Mungu. Kiasi chochote cha maumivu ni cha kufaa, kwa sababu ni jambo la thamani na la maana sana! Leo, ninateswa kwa kuhubiri injili na siko tayari kupitia maumivu yoyote ya kimwili kwa ajili ya injili; ninahisi kukosewa na kutokuwa tayari. Si nimemhuzunisha Mungu kwa kufanya hivi? Si nimekosa dhamiri? Ningewezaje kustahili baraka za huruma za Mungu na utolewaji wa maisha? Vizazi vya watakatifu wamebeba ushuhuda wa nguvu na mkubwa kwa Mungu kwa sababu walifuata njia ya Mungu; waliishi maisha yenye maana. Leo nina maneno haya yote kutoka kwa Mungu, kwa hiyo mimi si ni lazima hata zaidi nitoe ushuhuda mzuri kwa ajili ya Mungu? Kwa kutafakari jambo hili, mwili wangu haukujihisi kama mchungu, nilijua sana kuwa ni neno la Mwenyezi Mungu ambalo lilinipa uwezo wa uzima, likiniruhusu kuushinda udhaifu wa mwili.
Siku iliyofuata, hao polisi waovu hawakuwa na mkakati mwingine ulioachwa kujaribu. Walinitishia wakisema: “Hutasema chochote? Basi tutakufunga gerezani!” Baadaye, walinipeleka kwa kituo cha kizuizi. Katika kituo cha kizuizi, hao polisi waovu waliendelea kutumia njia zote za mateso kwangu na mara nyingi waliwahimiza wafungwa kunipiga. Katika baridi kali ya majira ya baridi, waliwaagiza wafungwa kunimwagilia ndoo za maji baridi na kunilazimisha kuoga na maji baridi. Nilikuwa nikitetemeka kwa baridi kutoka utosini hadi kidoleni. Hapa, wafungwa walikuwa mashine ya kutengeneza pesa kwa serikali na hawakuwa na haki yoyote ya kisheria. Hawakuwa na chaguo jingine ila kuvumilia kuminywa na kutumiwa na wengine kwa faida yao kama watumwa. Gereza lilinilazimisha kuchapisha pesa za karatasi zilizotumika kama sadaka za kuteketezwa kwa wafu mchana kutwa na kunilazimisha nifanye kazi ya ziada usiku. Kama ningesimama ili kupumzika, basi mtu fulani angekuja na kunipiga sana. Mara ya kwanza, waliweka sheria kwamba nilipaswa kuchapisha vipande 2,000 vya karatasi kwa siku, kisha wakaongeza viwe vipande 2,800 kwa siku, na hatimaye hadi vipande 3,000. Kiasi hiki kilikuwa hakiwezekani kwa mtu mwenye ujuzi kukamilisha sembuse mtu asiye na ujuzi kama mimi kukamilisha. Kwa kweli, walipanga hivyo kwa makusudi ili nisiweze kukamilisha yote ili waweze kuwa na udhuru wa kunitesa na kunidhuru. Alimradi sikuweza kufikia kiasi hicho, hao polisi waovu wangeniwekea pingu za miguu kwa miguu yangu ambazo zilikuwa na uzito wa zaidi ya kilo 5, na kuifunga mikono na miguu pamoja kwa pingu. Yote niliyoweza kufanya ni kuketi pale, kuinamisha kichwa changu na kugeuza kiuno changu, vinginevyo sikuweza kusonga. Aidha, hawa polisi wakatili na wasio na hisia hawakuuliza au kujali kuhusu mahitaji yangu ya msingi. Ingawa choo kilikuwa ndani ya seli ya gereza, sikuweza kabisa kutembea na kukitumia; niliweza tu kuwaomba wenzangu katika seli kuniinua na kuniwekelea kwa choo. Kama walikuwa wafungwa bora zaidi kidogo, basi wangeweza kuniinua; kama hakuna mtu aliyenisaidia, basi singekuwa na chaguo jingine ila kujinyia katika suruali yangu. Wakati wa maumivu mno ulikuwa wakati wa chakula, kwa sababu mikono na miguu yangu ilikuwa imefungwa pamoja. Niliweza tu kuteremsha kichwa changu kwa nguvu zangu zote na kuinua mikono na miguu yangu. Ni kwa njia hii tu nilivyoweza kuiweka skonsi kinywani mwangu. Nilitumia nguvu nyingi sana kwa kila umo. Pingu zilisugua mikono na miguu yangu na zikisababisha maumivu makubwa. Baada ya muda mrefu, vifundo vya mikono yangu na vya miguu vilikuwa vimekuza sagamba nyeusi na ngumu zilizong’aa. Mara nyingi sikuweza kula wakati nilipokuwa nimefungiwa, na mara chache, wafungwa wangenipa skonsi mbili ndogo. Mara nyingi wangekula sehemu yangu na yote niliyopata ilikuwa tumbo tupu. Nilipokea hata kinywaji kidogo zaidi; awali, kila mmoja alipewa tu bakuli mbili za maji kwa siku, lakini nilikuwa nimefungiwa na sikuweza kusogea, hivyo ni kwa nadra sana niliweza kunywa maji yoyote. Mateso hayo ya kinyama yalikuwa yasiyosemeka. Kwa ujumla, niliteseka hivi mara nne na kila mara nilikuwa nimefungiwa kwa siku zisizopungua tatu na zisizozidi nane. Kila wakati ambapo njaa haikuvumilika, ningefikiria maneno ambayo Mungu aliyasema zamani: “Mwanadamu hatadumu kwa mkate pekee, lakini kwa kila neno linalotoka kinywani mwa Mungu” (Mathayo 4:4). Hatua kwa hatua nilianza kutambua kwamba Mungu anataka kutimiliza ukweli kwamba “Neno Lake lakuwa uhai wa mwanadamu” kwangu kupitia mateso ya Shetani. Katika kuelewa mapenzi ya Mungu, moyo wangu uliokolewa na nikamwomba Mungu kwa amani na kujaribu kuyaelewa maneno ya Mungu. Pasipo kujua, sikuhisi uchungu sana tena au njaa. Hili kwa hakika lilinifanya nisihisi kuwa neno la Mungu ni ukweli, njia, na uzima na bila shaka ni msingi ambao napaswa kutegemea ili kuishi. Kwa hiyo, imani yangu kwa Mungu iliongezeka bila kujua. Nakumbuka wakati mmoja polisi wa gerezani kwa makusudi walinitesa na kunifunga pingu. Kwa siku tatu mchana na usiku sikunywa hata tone la maji. Mfungwa aliyekuwa amefungwa pingu karibu na mimi akasema: “Kulikuwa na mtu fulani wa umri mdogo kabla ambaye alifungwa pingu na kunyimwa chakula jinsi hii hadi kufa. Naona kuwa hujala chochote kwa siku kadhaa na bado una uchangamfu.” Katika kusikia maneno yake, nilifikiri kwamba ingawa sikuwa nimekula au kunywa chochote kwa siku tatu mchana na usiku, sikuhisi kero ya njaa. Nilihisi sana kwamba hii ilikuwa ni nguvu ya uzima katika maneno ya Mungu ikinisaidia na kunisababisha kwa hakika kuona Mungu akionekana kwangu katika maneno Yake. Moyo wangu ulikuwa na msisimko daima; katika mazingira haya ya mateso niliweza kwa kweli kupitia uhalisi wa ukweli kwamba “Mwanadamu hataishi kwa mkate pekee, lakini kwa kila neno linalotoka kinywani mwa Mungu.” Huu kwa kweli ni utajiri wa thamani zaidi wa maisha ambao Mungu ameniridhia, na pia ni zawadi yangu ya pekee. Aidha, singeweza kamwe kuupata katika mazingira ambayo sikuhitaji kuwa na wasiwasi juu ya chakula au nguo. Sasa, mateso yangu yalikuwa na maana nyingi sana na thamani! Wakati huu, sikuweza kujizuia kufikiria maneno ya Mungu: “Kile ambacho umerithi wakati huu, kimepiku walichorithi mitume na manabii na ni kikuu zaidi kuliko alichopokea Musa na Petro. Baraka haziwezi zikapokewa kwa siku moja au mbili; sharti zipatikane kwa kujitolea kwingi. Yaani, lazima uwe na upendo uliosafishwa, imani kuu, na ukweli mwingi ambao Mungu Anakuagiza uufikie; zaidi ya hayo, sharti uelekeze uso wako kwa haki wala usikubali kushindwa, na lazima uwe na upendo usiofikia kikomo kwa ajili ya Mungu. Azimio linahitajika kutoka kwako, na vilevile mabadiliko katika tabia ya maisha yako. Upotovu wako lazima utibiwe, na lazima ukubali mipango ya Mungu pasipo kulalamika, na hata uwe mtiifu hadi kifo. Hicho ndicho unachopaswa kutimiza. Hili ndilo lengo la Mungu la mwisho, na matakwa ya Mungu kwa watu wa kundi hili” (“Je, Kazi ya Mungu Ni Rahisi Jinsi Mwanadamu Anavyodhania?” katika Neno Laonekana katika Mwili). Katika kujaribu kuyaelewa maneno ya Mungu, nilitambua kwamba baada ya mateso na majaribu baraka huja kutoka kwa Mungu, na huu ndio ugavi wa mahitaji na umwagiliwaji wa maji kwangu kutoka kwa Mungu. Sasa, ingawa maneno ambayo Mungu amenipa yamepita vizazi vya watakatifu, bado nahitaji kuwa na imani na uvumilivu ili kuwa na uwezo wa kutokukubali kushindwa wakati wa majaribu na mateso yangu, kuitii mipango ya Mungu, na kupokea wokovu wa Mungu. Kisha nitaweza kuuingia uhalisi wa neno la Mungu na kuweza kuona matendo ya ajabu ya Mungu. Kama haingekuwa kwa gharama ya shida hii, singestahili kupokea ahadi na baraka za Mungu. Kupokea nuru ya Mungu kulinielekeza kuwa na udhabiti na nguvu zaidi ndani; niliweka azimio: Shirikiana na Mungu kwa bidii na kuyaridhisha mahitaji ya Mungu katikati ya mazingira haya machungu, kumshuhudia Mungu ili niweze kuwa na mavuno makubwa mno.
Mwezi mmoja baadaye, polisi wa CCP walinishtaki na “kushukiwa kuvuruga utaratibu wa jamii na kuharibu utekelezaji wa sheria”; nilihukumiwa mwaka mmoja wa mageuzi kupitia kazi. Nilipoingia kambi ya kazi, wale polisi waovu walieneza uvumi na upuuzi miongoni mwa wafungwa, wakisema kuwa nilikuwa muumini katika Mwenyezi Mungu, jambo ambalo ni baya kuliko mauaji na wizi, na waliwachochea wafungwa kunitesa. Kwa hiyo mara nyingi nilipigwa na kuwekwa katika hali ngumu na wafungwa bila sababu yoyote. Hili lilinifanya nione kweli kwamba China ni nchi ya mateso na maumivu inayoongozwa kwa uthabiti na Shetani, pepo. Kuna giza kutoka kila pembe, na hakuna mwanga unaoruhusiwa kuwepo; hakuna mahali kabisa pa waumini wa Mwenyezi Mungu kuishi. Wakati wa mchana, hao polisi waovu walinilazimisha kufanya kazi katika karakana. Kama sikufikia kiasi nilichopaswa kufikia, wangewaacha wafungwa wanipige wakati niliporudi kwa seli yangu gerezani na kutangaza “mfanyeni mfano ili kuwaogofya wengine.” Nilipokuwa katika karakana nikihesabu mifuko, ningehesabu mifuko 100 na kisha kuifunga pamoja. Wafungwa wangekuja daima na kutoa mfuko moja au kadhaa kutoka kwa ile niliyokuwa nimehesabu, kisha wangesema kwamba sikuhesabu vizuri na kuchukua hiyo kama fursa ya kunipiga ngumi na mateke. Wakati msimamizi huyo aliponiona nikipigwa, angekuja na kuniuliza kwa unafiki kilichokuwa kikiendelea na wafungwa wangewasilisha ushahidi wa uongo kwamba sikuwa nimehesabu mifuko ya kutosha. Kisha ningelazimika kustahimili mfululizo wa ukosoaji mkali kutoka kwa msimamizi. Aidha, wangeniamuru nikariri “amri za maadili mema” kila asubuhi, na kama sikuzikariri, ningepigwa; pia wangenilazimisha kuimba nyimbo zilizokisifu chama cha Kikomunisti. Kama waliona kwamba sikuwa nikiimba au kwamba midomo yangu haikuwa ikisonga, basi usiku bila shaka ningepigwa. Pia waliniadhibu kwa kunifanya nipanguse sakafu, na kama sikupangusa kwa matarajio yao, basi ningepigwa kwa nguvu nyingi. Wakati mmoja, kwa ghafla wafungwa fulani walianza kunigonga na kunipiga mateke. Baada ya kunipiga, waliniuliza: “Kijana, unajua kwa nini unapigwa? Ni kwa sababu hukusimama na kumsalimu msimamizi wakati alipokuja!” Baada ya kila wakati nilipopigwa, nilikuwa na hasira lakini sikuthubutu kusema chochote; niliweza kulia tu na kumwomba Mungu kimyakimya, nikimwambia Yeye juu ya chuki na malalamiko moyoni mwangu kwa sababu ya mahali hapa palipo na utovu wa sheria, na kukosa mantiki. Hapakuwa na busara hapa, palikuwa na vurugu tu. Kulikuwa hakuna watu hapa, kulikuwa na pepo wenye wazimu na nge tu! Nilihisi maumivu mengi sana na shinikizo nikiishi katika shida hii; sikuwa tayari kukaa hata dakika moja zaidi. Kila wakati nilipotumbukia katika hali ya udhaifu na maumivu, ningefikiri juu ya maneno ya Mwenyezi Mungu: “Mmewahi kuzikubali baraka mlizopewa? Mmewahi kutatufa ahadi mlizopewa? Hakika, chini ya mwongozo wa mwangaza Wangu, mtapenya utawala wa nguvu za giza. Hakika, katikati ya giza, hamtaupoteza mwangaza unaowaongoza, katikati ya giza. Hakika mtakuwa bwana wa viumbe vyote. Hakika mtakuwa washindi mbele ya Shetani. Hakika, wakati wa maangamizi ya ufalme wa joka kubwa jekundu, mtasimama miongoni mwa umati mkubwa kushuhudia ushindi Wangu. Hakika mtakuwa shujaa na imara katika nchi ya Sinimu. Kupitia mateso mnayoyavumilia, mtarithi baraka zinazotoka Kwangu, hakika mtaangaza ndani ya ulimwengu wote kwa utukufu Wangu” (“Sura ya 19” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yalinitia moyo. Bila kujali kama kile Mungu alichokuwa akinifanyia kilikuwa neema na baraka au majaribu na usafishwaji, yote ilikuwa ili kunikimu na kuniokoa; ilikuwa ni kuweka ukweli ndani yangu na kufanya ukweli kuwa maisha yangu. Leo, Mungu aliruhusu mateso haya na taabu zinijie. Ingawa jambo hili lilisababishia mateso mengi, liliniruhusu kuweza kwa kweli kuwa na uzoefu kwamba Mungu yu pamoja nami; lilinifanya kwa kweli nifurahie maneno ya Mungu kuwa mkate wa maisha yangu na taa ya miguu yangu na mwanga kwa njia yangu, likiniongoza hatua kwa hatua kupitia mahali hapa padhalimu na pasipovumilika. Huu ndio upendo na ulinzi wa Mungu ambao nilifurahia na kupata wakati wa mchakato wa mateso yangu. Wakati huu, niliweza kuona kwamba nilikuwa kipofu sana na wa ubinafsi na nilikuwa mwenye uroho mno. Katika kumwamini Mungu, nilijua tu jinsi ya kufurahia neema na baraka za Mungu na sikutafuta ukweli na uhai kwa kiwango hata kidogo. Mara mwili wangu uliopitia shida kidogo, ningenung’unika bila kukoma; sikuelewa kabisa mapenzi ya Mungu na sikutafuta kuielewa kazi ya Mungu. Daima ningemfanya Mungu ahisi huzuni na maumivu juu yangu. Kwa kweli nilikuwa bila dhamiri! Kwa majuto na kujilaumu, niliomba kimya kimya kwa Mungu: “Ewe Mwenyezi Mungu, naweza kuona kwamba kila kitu unachokifanya ni kuniokoa na kunipata. Ninachukia tu kwamba mimi ni mkaidi sana, ni kipofu na sina ubinadamu. Daima nimekuelewa visivyo na sijakuwa wa kufikiria mapenzi Yako. Ee Mungu, leo neno Lako limeuamsha moyo wangu wenye ganzi na roho yangu na limenisababisha kuyaelewa mapenzi Yako. Siko tayari tena kuwa na tamaa na mahitaji yangu mwenyewe; nitatii tu mipango Yako. Hata kama ni lazima nipitie matatizo yote, bado nitaendelea kushirikiana na Wewe kwa bidii na nitatoa ushahidi mkubwa sana Kwako muda wote wa mateso ya Shetani. Nitatafuta kujitenga na ushawishi wa Shetani na kuishi kwa kudhihirisha mfano wa mtu halisi ili kukuridhisha.” Baada ya kuomba, nilielewa nia njema za Mungu, na nilijua kwamba kila mazingira ambayo Mungu aliniruhusu kupitia yalikuwa ni upendo na wokovu mkubwa wa Mungu kwangu. Kwa hiyo, singefikiria tena kujikunyata au kumwelewa Mungu visivyo. Ingawa hali ilikuwa bado ni ile ile, moyo wangu kwa kweli ulijaa furaha na ridhaa; nilihisi kuwa ni heshima na fahari kuweza kupitia shida na mateso kwa sababu ya imani yangu kwa Mwenyezi Mungu, na ilikuwa ni zawadi ya pekee kwangu, mtu mpotovu; ilikuwa baraka maalumu na neema za Mungu kwangu.
Baada ya kuwa na uzoefu wa mwaka mmoja wa shida katika jela, naona kwamba mimi ni mdogo sana wa kimo na kwamba nakosa ukweli mwingi sana. Mwenyezi Mungu kwa kweli amefidia upungufu wangu kupitia mazingira haya ya kipekee na ameniruhusu kukua. Katika dhiki yangu, Amenifanya kupata utajiri wa thamani mno katika maisha na kuelewa ukweli mwingi ambao sikuufahamu katika siku za nyuma na kuona kwa dhahiri sura mbaya kwa Shetani, pepo, na kiini cha kupinga maendeleo cha upinzani wake kwa Mungu. Nilitambua uhalifu wake muovu wa kumtesa Mwenyezi Mungu na kuwaua Wakristo. Nilipitia kwa dhati wokovu na huruma kubwa Mwenyezi Mungu aliyokuwa nayo kwangu, mtu mpotovu, na nimehisi kwamba nguvu na maisha katika maneno ya Mwenyezi Mungu yanaweza kunipa mwanga na kuwa maisha yangu na kunielekeza kumshinda Shetani na kwa ushupavu kutoka nje ya bonde la uvuli wa mauti. Vivyo hivyo, pia niligundua kwamba Mwenyezi Mungu ndiye anayeniongoza kwenye njia sahihi ya uzima. Ni njia ng’avu ya kupata ukweli na uzima! Kuanzia sasa na kwendelea, bila kujali ni mateso yapi, dhiki au majaribu hatari yanayonikabili, niko tayari kutafuta ukweli kwa bidii na kupata njia ya uzima wa milele ambayo Mwenyezi Mungu amenipa.
Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo

Alhamisi, 13 Juni 2019

Kuingiza kwenye Njia ya Imani katika Mungu

Wokovu wa Mungu, Mkristo, Ushuhuda wa Maisha

Rongguang Mji wa Harbin, Mkoa wa Heilongjian
Mnamo mwaka wa 1991, kwa neema ya Mungu, nilianza kumfuata Mwenyezi Mungu kwa sababu ya ugonjwa. Wakati huo sikujua kitu chochote kuhusu kumwamini Mungu, lakini jambo la kushangaza ni kwamba, wakati wa kula na kunywa maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu, nilifurahia. Nilihisi kwamba maneno Yake yalikuwa mazuri sana, na nilipoimba au kuomba mara nyingi niliguswa na Roho Mtakatifu hadi kiwango cha kulia. Uzuri huo ndani ya moyo wangu, furaha hiyo ilikuwa ni kama kwamba tukio la furaha lilikuwa limenijia. Hasa katika mikusanyiko wakati wa kazi kubwa ya Roho Mtakatifu, nilihisi kama nilikuwa nimevuka mipaka ya mwili na nilikuwa nikiishi katika mbingu ya tatu, kwamba kila kitu cha ulimwengu kilikuwa kimetupiliwa mbali. Siwezi kusema jinsi nilivyokuwa na furaha, jinsi nilivyoridhika moyoni mwangu. Nilihisi kwamba nilikuwa mtu mwenye furaha zaidi duniani. Kwa hivyo wakati huo niliamini kwamba kumwamini Mungu kulikuwa tu kufurahia neema Yake.
Wakati maneno mengi zaidi na zaidi ya Mungu yalikuwa yakitolewa (wakati huo yalikuwa yakitumwa kanisani siku zote, kifungu baada ya kifungu), pia nilijua zaidi na zaidi. Kisha, sikukamilishwa tena na kufurahi tu neema ya Mungu. Nilipoona “wazaliwa wa kwanza” wakitajwa katika maneno Yake na nikajifunza kwamba Mungu hutoa baraka kubwa kwa wazaliwa Wake wa kwanza, nilitafuta kuwa mmoja, nikitumaini kuwa siku zijazo ningeweza kutawala na Mungu. Baadaye, nilipoona katika maneno Yake kwamba muda Wake ulikuwa ukija hivi karibuni, nilihisi dharura zaidi, na kudhani: Nilikawia sana kumwamini Mungu; Je, sitakuwa na uwezo wa kupata baraka hii? Ninahitaji kuweka juhudi zaidi ndani ya hili. Kwa hivyo, nyumba ya Mungu iliponipangia kutekeleza wajibu, nilikuwa mwenye bidii sana. Sikuogopa shida. Niliamua kuacha kila kitu kumfuata Mungu ili niweze kupata baraka ya kuwa mwana wa kwanza. Kwa kweli, Mungu hakuwa amesema waziwazi katika maneno Yake kwamba tungeweza kuwa wazaliwa wa kwanza. Ilikuwa tu kwa sababu tulikuwa na malengo na tamaa zilizopita kiasi, tuliamini kwamba kwa kuwa Mungu alikuwa ametuita “wana” Wake na kwamba sasa Ametuinua, kwamba hakika tungekuwa wazaliwa wa kwanza. Hivi ndivyo nilivyoamini kwamba nilikuwa, kwa kawaida, nimekuwa mzaliwa wa kwanza. Baadaye niliona maneno ya Mungu ambayo yalikuwa yametolewa karibuni ambayo mara kwa mara yalitaja “watendaji-huduma,” na kulikuwa na maelezo zaidi na zaidi ya hukumu ya watendaji-huduma. Nilidhani mwenyewe: Kwa bahati ninamfuata Mwenyezi Mungu, vinginevyo ningekuwa mtendaji-huduma. Niliposoma kuhusu baraka za Mungu na ahadi za wazaliwa wa kwanza, niliamini kuwa sehemu ya hiyo ingekuwa yangu. Nilipoyasoma maneno Yake ya faraja na ya kuhimiza kwa mzaliwa Wake wa kwanza, nilihisi pia kwamba yalikuwa yakielekezwa kwangu. Nilihisi furaha hata zaidi hasa nilipoona yafuatazo “Maafa makuu hakika hayatawafikia wana Wangu, wapendwa Wangu. Nitawatunza wana Wangu kila wakati na kila sekunde. Hakika hamtavumilia uchungu na mateso hayo; badala yake, ni kwa ajili ya ukamilishwaji wa wana Wangu na utimizaji wa neno Langu ndani yao, ili kwamba muweze kutambua kudura Yangu, mkue zaidi katika maisha, mbebe mizigo kwa ajili Yangu karibuni, na kujitolea kabisa kwa ukamilisho wa mpango Wangu wa usimamizi. Mnapaswa kuwa na furaha na kuridhika na kushangilia kwa sababu ya hili. Nitawapa kila kitu, Nikiwaruhusu kuchukua usukani. Nitaiweka mikononi mwenu. Mwana akirithi mali nzima ya babake, je, ninyi wana Wangu wazaliwa wa kwanza mtaridhi zaidi kiasi gani? Kweli mmebarikiwa. Badala ya kuteseka kutokana na maafa makuu, mtafurahia baraka za milele. Utukufu ulioje! Utukufu ulioje!” (“Sura ya 68” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili). Nilidhani: Je, ninaota? Mana hii ya ajabu kutoka mbinguni imeshuka juu yangu? Sikuweza kabisa kuthubutu kuamini, lakini nilihofu kuwa kaka zangu na dada wangesema kuwa imani yangu ilikuwa ndogo sana, kwa hivyo sikuthubutu kutoamini.
Siku moja, nilikwenda kwa furaha kushiriki katika mkutano, na nikaona kwamba viongozi wawili walikuwa wamekuja kanisani. Nilipokuwa katika ushirika nao, walisema kuwa walikuwa watendaji-huduma. Baada ya kusikia hayo, nilikuwa na hofu, na nikawauliza: “Ikiwa ninyi ni watendaji-huduma, si sisi wote ni watendaji-huduma?” Walisema ukweli bila kusita: “Takribani sisi sote nchini China ni watendaji-huduma.” Niliposikia wakisema hivi, moyo wangu ulihofu. Haiwezekani! Je, huu ni ukweli? Lakini nilipoona maonyesho yao nzito, yenye uchungu na kwamba nyuso za wengine pia zilikuwa za majonzi, sikuweza kuamini. Lakini nilibadili mawazo yangu na kufikiri: Kama viongozi, walikuwa wameacha familia zao na kazi zao, walikuwa wameteseka sana na kulipa thamani kuu sana kwa ajili ya kazi ya Mungu. Nilipungukiwa kabisa ikilinganishwa nao; kama wao ni watendaji-huduma, ningesema nini kingine? Mtendaji-huduma ni mtendaji-huduma, hivyo wakati huo, sikuhisi vibaya mno.
Baada ya kwenda nyumbani, nilichukua neno la Mungu tena na kuangalia kile Mungu alichokuwa na kusema kuhusu watendaji-huduma, na nikaona haya: “Wale wanaonitumikia, sikilizeni! Mnaweza kupokea baadhi ya neema Yangu wakati mnanitumikia. Yaani, ninyi mtajua kwa wakati kuhusu kazi Yangu ya baadaye na mambo ambayo yatatokea baadaye, lakini hamtafurahia hilo kabisa. Hii ni neema Yangu. Wakati huduma Yako imekamilika, ondoka mara moja na usikawie. Wale ambao ni wazaliwa Wangu wa kwanza hawapaswi kuwa wenye kiburi, lakini mnaweza kujivunia, kwa kuwa Nimewapa baraka za milele kwenu. Wale ambao ni walengwa wa uangamizaji hampaswi kujiletea shida au kuhisi huzuni kwa ajili ya hatima yenu; ni nani aliyekufanya kuwa mzawa wa Shetani? Baada ya kufanya huduma yako kwa ajili Yangu, unaweza kurudi tena kwenye shimo lisilo na mwisho kwa sababu hutakuwa tena na matumizi Kwangu na Nitaanza kuwashughulikia na kuadibu Kwangu. Mara Ninapoanza kazi Yangu huwa Sikomi kamwe; kile Ninachofanya kitatimizwa na kile Ninachotimiza kitadumu milele. Hili linatumika kwa wazaliwa Wangu wa kwanza, wanangu, watu Wangu, na hili linawahusu ninyi pia—Mimi kuwaadibu ninyi kutakuwa kwa milele” (“Sura ya 86” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili). Mara tu nilipoyasoma maneno haya nilizongwa na uchungu ambao sikuwa nimewahi kuhisi hapo awali. Nilifunga haraka kitabu cha maneno ya Mungu na sikujaribu kukitazama tena. Mara moja hisia za kusikitisha, za kuchanganyikiwa, za kutoridhika zote zilichemka ndani ya moyo wangu mara moja. Nilidhani: Jana nilikuwa katika susu ya furaha, lakini leo nimesukumwa nje ya nyumba ya Mungu. Jana nilikuwa mwana wa Mungu, lakini leo nimekuwa adui wa Mungu, mzao wa Shetani. Jana, baraka zisizo na kikomo za Mungu zilikuwa zikinisubiri, lakini leo shimo la kuzimu ni hatima yangu, nami nitaadhibiwa hata milele. Ikiwa Hatoi baraka, basi haijalishi, lakini kwa nini bado lazima Aniadibu? Nimekosea vipi tena? Haya yote ni ya nini tena? Sikuwa tayari kukabiliana na ukweli huu; sikuweza kukabiliana na aina hii ya ukweli. Niliyafumba macho yangu na sikuwa radhi kufikiri juu ya hayo tena. Nilitumaini sana kwamba ilikuwa ndoto tu.
Kuanzia hapo kuendelea, mara tu nilipojifikiria kuwa mtendaji-huduma, nilisikia maumivu yasiyoelezeka moyoni mwangu, na sikuthubutu kuyasoma maneno ya Mungu tena. Lakini Mungu ni mwenye hekima sana, na maneno Yake ambayo huwaadibu na kuwafichua watu hayaenei tu kwa fumbo, lakini pia ni unabii wa maangamizi ya siku za baadaye na vilevile mtazamo wa ufalme na mambo yanayofanana na hayo. Hivi vyote vilikuwa vitu ambavyo nilitaka kuvijua, hivyo bado singekwepa maneno Yake. Wakati wa kusoma maneno ya Mungu, maneno Yake makali sana yaliuchoma moyo wangu mara kwa mara, na sikuwa na budi ila kukubali hukumu na kuadibiwa na Yeye. Nilihisi kwamba ghadhabu kubwa ya hukumu ya Mungu ilikuwa daima juu yangu. Kando na maumivu, nilijua ukweli halisi wa kupotoshwa kwangu na Shetani. Ilibainika kuwa nilikuwa mtoto wa joka kubwa jekundu, uzao wa Shetani, na lengo la uharibifu. Katika kukata tamaa, sikuthubutu tena kutumaini kwa tamaa baraka zozote, na nilikuwa tayari kukubali majaaliwa ya Mungu kwamba nilikuwa mtendaji-huduma. Nilipohisi kwamba ningeweza kutoa moyo wangu katika kuwa mtendaji huduma, Mungu tena aliyapanga mazingira yaliyofichua tabia potovu ambayo ilikuwa imefichwa ndani yangu. Siku moja nilipokuwa nikiyasoma maneno ya Mungu, niliona: “Baada Yangu kurudi Sayuni, wale walio duniani wataendelea kunisifu Mimi kama zamani. Wale watendaji huduma waaminifu wanabaki wakisubiri kutoa huduma Kwangu lakini kazi yao itakuwa imefika mwisho. Jambo bora zaidi wanaloweza kufanya ni kutafakari hali Yangu kuwa duniani. Wakati huo Nitaanza kushusha maafa juu ya wale ambao watakabiliwa na msiba mkubwa, lakini kama vile[a] wote wanaamini kwamba Mimi ni Mungu mwenye haki, basi bila shaka sitawaadhibu wale watendaji-huduma waaminifu nao watapokea tu neema Yangu” (“Sura ya 120” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili). Nilipoona hili, nilifikiri kwa siri: Sitafikiri tena juu ya haki ya mzaliwa wa kwanza na sitahitaji tena baraka nyingi. Sasa nitafuatilia tu kuwa mtendaji-huduma mwenye kumcha Mungu. Huu sasa ndio ufuatiliaji wangu wa pekee. Katika siku zijazo, bila kujali ni nini ambacho nyumba ya Mungu atanipangia mimi kufanya, nitakifanya kwa kujitolea kadiri ninavyoweza. Mimi kabisa siwezi kupoteza nafasi ya kuwa mtendaji-huduma mwaminifu tena. Kama hata sina uwezo wa kuwa mtendaji-huduma mcha Mungu lakini bali mtendaji-huduma tu, baada ya kumaliza huduma yangu ni lazima nirudi katika shimo la kuzimu au ziwa la moto wa jahanamu. Kwa hivyo yote ni ya nini? Sikuthubutu kuonyesha mawazo haya kwa mtu yeyote, lakini sikuweza kuepuka uchunguzi kutoka kwa macho ya Mungu. Niliyasoma maneno ya Mungu yaliyosema: “Hakuna awezaye kuielewa asili ya mwanadamu isipokuwa Mimi, na wote wanafikiria kwamba wao ni watiifu Kwangu, pasipo kujua kwamba utiifu wao ni mchafu. Uchafu huu utawaangamiza watu kwa kuwa wao ni njama ya joka kubwa jekundu. Hilo lilidhihirishwa na Mimi zamani sana; Mimi ni mwenyezi Mungu, na je, Mimi singeweza kufahamu jambo rahisi kama hili? Mimi ninaweza kupenyeza damu yako na mwili wako ili kuziona nia zako. Si vigumu Kwangu kuielewa asili ya mwanadamu, lakini watu hujaribu kuwa wajuaji, wakifikiria kwamba hakuna mtu ajuaye nia zao isipokuwa wao wenyewe. Je, hawajui kwamba, mwenyezi Mungu anaishi ndani ya mbingu na dunia na vitu vyote?” (“Sura ya 118” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili). “Watu wengi zaidi sasa wanahodhi matumaini haba, lakini matumaini hayo yanapogeuka na kuwa masikitiko hawataki kuendelea zaidi na wanaomba kurudi. Nimekwisha kusema awali kwamba Simweki yeyote hapa kinyume cha mapenzi yake, lakini tahadhari kufikiria matokeo yatakavyokuwa kwako, ni huu ni ukweli, si Mimi kukutisha wewe” (“Sura ya 118” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili). Baada ya kusoma haya, moyo wangu ulikuwa ukipapa kwa nguvu. Nilihisi kwamba Mungu kwa kweli hubaini kila kipengele cha nafsi ya mwanadamu. Tunafikiria kitu na Mungu anajua; tunaweka tumaini kidogo katika mioyo yetu na Mungu anachukizwa. Wakati huo tu ndipo nilikuwa na moyo wa kumcha Mungu. Niliamua kwamba singeendesha tena shughuli na Mungu, ila kwa uaminifu, ningetenda kama mtendaji-huduma na kutii miundo Yake.
Baadaye tu ndipo nilijua kwamba uzoefu wangu kwa miezi hii mitatu ilikuwa jaribio la watendaji-huduma. Ilikuwa kazi ya kwanza ambayo Mungu alikamilisha ndani ya watu ya jaribio kwa maneno Yake. Baada ya kupitia jaribio la watendaji-huduma, nilielewa kuwa Mungu sio Mungu mwenye huruma na upendo tu, bali ni Mungu mwenye haki, Mungu mwenye uadhama ambaye havumilii makosa ya wanadamu. Maneno Yake yana mamlaka na nguvu, ambayo hayana budi ila kuzalisha moyo wa hofu kwa mwanadamu. Nilijua pia kwamba wanadamu ni viumbe wa Mungu, kwamba tunapaswa kuamini katika Mungu na kumwabudu Yeye. Hili ndilo lililo sawa na sahihi. Hakuna haja ya sababu, ya masharti, na hakupaswi kuwa na tamaa ya makuu au hamu iliyopita kiasi. Ikiwa watu wanaamini katika Mungu ili kupata kitu kutoka Kwake, basi aina hii ya imani ni kumtumia vibaya na kumdanganya. Ni maonyesho ya kukosa dhamiri na mantiki. Hata kama watu humwamini Mungu lakini hawapati chochote na baadaye kupata adhabu Yake, wanapaswa kumwamini. Wanadamu wanapaswa kumwamini na kumtii Mungu kwa sababu Yeye ni Mungu. Nilitambua pia kwamba mimi mwenyewe ni mwana wa joka kuu jekundu, kizazi cha Shetani, na mmoja wa wale watakaoangamia. Mungu ni Bwana wa viumbe vyote, na bila kujali Anavyonitendea mimi inastahili. Yote ni ya haki, na ninapaswa kuitii mipango na mipangilio Yake bila masharti. Sipaswi kujaribu kujadiliana na Yeye, na hata zaidi sipaswi kumpinga. Nilipokumbuka uzuzu wangu mwenyewe uliofichuliwa katika jaribio hili, niliona kwamba nilikuwa kweli mwenye aibu, na kwamba nilitaka tu kupata hadhi fulani ya juu, baraka nyingi, au hata kukaa bega kwa bega na Mungu na kutawala pamoja na Yeye. Nilipoona kwamba singepata baraka nilizozitarajia bali badala yake kupitia maangamizi, nilifikiria kuhusu kumsaliti Mungu. Mafafanuzi hayo ya wazi kabisa yalinifanya nione wazi kwamba lengo langu katika kumwamini Mungu lilikuwa kubarikiwa. Nilikuwa nikijaribu kufanya shughuli za kibiashara na Mungu kwa dhahiri. Kweli nilikuwa asiye na aibu, nikipigania hadhi na Mungu kwa ulafi—hilo lilitofautiana vipi na malaika mkuu? Kwa kweli nilikuwa mwenye kiburi, na nilikuwa nimepoteza kabisa mantiki ambayo mtu anapaswa kuwa nayo. Isingekuwa hekima hiyo katika kazi ya Mungu—kutumia jaribio la watendaji-huduma ili kunishinda, kuvunja tamaa yangu ya kupata baraka—bado ningekuwa nikikimbia katika njia isiyo sahihi ya kutafuta baraka. Nisingeweza kuelewa asili yangu iliyopotoka, na hasa singekubali hukumu na adhabu ya maneno ya Mungu kwa utiifu. Katika hali hiyo, nisingeweza kamwe kuokolewa au kukamilishwa.
Baada ya kupitia jaribio la watendaji-huduma, nilidhani sikuthubutu tena kumwamini Mungu na kutekeleza wajibu wangu ili kupata baraka, na nilidhani sikuthubutu tena kufanya mambo kwa nia ya kufanya shughuli na Mungu. Nilihisi kuwa kumtumia vibaya na kumdanganya Mungu kwa njia hii kulistahili kudharauliwa sana. Lakini wakati huo huo, nilikuwa na ufahamu kwamba Mungu kutumia jaribio hili kuokoa wanadamu ni nia Yake ya fadhili, na nilijua kuwa hakuna sehemu Yake ambayo humchukia mwanadamu. Upendo Wake kwa wanadamu haujabadilika tangu Alipoumba ulimwengu, hivyo, moyoni mwangu, nilikuwa tayari kufuatilia njia ya kuridhisha na kulipiza upendo wa Mungu katika imani yangu ya baadaye Kwake na kutimiza wajibu wangu. Hata hivyo, kwa sababu nia ya kupata baraka na kuendesha shughuli na Mungu imefanywa madhubuti sana katika mioyo ya watu, haiwezekani kutatua kabisa kwa kupitia jaribio moja tu. Baada ya muda fulani kupita, mambo haya yatajidhihirisha tena. Kwa hivyo, ili kutushinda zaidi na kabisa na kutuokoa, Yeye hufanya majaribio kadhaa ya mfululizo kwetu—jaribio la nyakati za kuadibiwa, jaribio la kifo, na majaribio ya miaka saba. Kati ya majaribio haya, nililopitia zaidi na kufaidika zaidi kutokana nalo lilikuwa jaribio la miaka saba la 1999.
Mnamo mwaka wa 1999, nilichaguliwa kuwa kiongozi wa kanisa. Hii ilikuwa ni mwaka ambao injili ya ufalme ilienea sana, na nyumba ya Mungu ilihitaji kwamba tujaribu kumwokoa kila mtu aliyekuwa na uwezekano wa kuokolewa. Nilipoona utaratibu huu kutoka kwa nyumba ya Mungu, nilifikiri kazi ya Mungu ingekamilika mwaka wa 2000. Ili kujipatia roho zaidi na kupata hatima nzuri wakati ulipofika, nilijipa shughuli za injili kuanzia asubuhi hadi usiku. Kwa mintarafu ya maisha ya kanisa, nilikuwa nikihudhuria tu na kufanya mambo kwa namna isiyo ya dhati. Hata ingawa nilitambua kuwa nia zangu hazikuwa sawa, sikuwa na uwezo wa kudhibiti tamaa yangu ya kupata baraka. Wakati huo nilikuwa na shughuli nyingi, na nilihisi kuwa kufanya chochote kando na kazi ya injili kulikuwa kunanizuia, hata kula na kunywa neno la Mungu. Hivi ndivyo nilivyoanza kufanya kazi kwa ari kubwa, na bila ya kujua mwaka ulikuwa umekwisha. Nyumba ya Mungu ilikuwa imemchagua mtu wa mahali palepale ili kusaidia katika kazi, kwa hivyo nikarudi eneo la makazi yangu ya kudumu.
Nilidhani kwamba kazi ya Mungu itakapomalizika, janga kubwa hakika lingetokea, na hivyo baada ya kurudi nyumbani, nilisubiri tu janga nikiwa nyumbani kila siku, nikisubiri mwisho wa kazi ya Mungu. Nilipoona kwamba Sherehe ya Majira ya Kuchipua ilikuwa ikiwadia, kulikuwa na ushirika kutoka kwa kiongozi wa kanisa uliosema kuwa ni jambo la lazima kupitia miaka saba ya majaribio. Baada ya kusikia ujumbe huu, nilihisi kushtuka na moyo wangu ulikuwa katika msukosuko. Sikuwa na budi ila kuanza kujadiliana na Mungu: Miaka mingine saba imenikaribia—je, hii ni njia gani ya kuishi? Ee Mungu, ninakuomba Uniangamize mimi. Kwa kweli siwezi kuvumilia mateso haya tena! Siku iliyofuata, bado sikuweza kuepukana na mfadhaiko wangu. Nilidhani: Vyovyote vile, imekuwa miaka saba. Kesho ni siku nyingine—nitatoka na kuiondoa kutoka mawazo yangu. Mara tu nilipoingia kwenye basi, nilihisi Roho Mtakatifu alikuwa ndani yangu akishutumu: Wakati huo ulisema kwamba ungempenda Mungu hadi mwisho, kwamba hungemwacha kamwe, kwamba ungevumilia shida yoyote na Yeye. ... Je, wewe si mnafiki anayejaribu kumdanganya Mungu? Huku nikikabiliana na shutuma ya Roho Mtakatifu, sikuwa na budi ila kuning’iniza kichwa changu. Ilikuwa kweli. Awali, nilipokuwa nimefurahia neema ya Mungu, nilimpa ahadi, lakini sasa wakati ambapo kuna matatizo na ni lazima niyapitie, nataka kughairi neno langu. Hivyo si ahadi zangu ni za uongo tu? Mungu alinipa upendo mwingi sana, na sasa ninapokutana na mazingira ambayo sio kabisa kama ambavyo ninapenda nina hasira kubwa sana kiasi kwamba nataka kumghairi Mungu. Kwa kweli mimi ni mnyama asiye na shukrani, asiye bora kuliko mnyama! Nilipofikiri juu ya jambo hili, sikukuwa tena na hisia za kwenda nje, lakini nilirudi nyumbani na moyo mzito. Hata ingawa nilikuwa nimelazimishwa kuwa “mtiifu,” nilipofikiria ukweli kwamba bado kulikuwa na miaka saba iliyobaki katika kazi ya Mungu, niliweka huru katika moyo wangu na chochote nilichokifanya, sikuwa na haraka au wasiwasi. Nilitia bidii kila siku katika kutimiza wajibu wangu kana kwamba ilikuwa siku nyingine yoyote. Aina hii ya hali mbaya na yenye makabiliano ilinifanya nipoteze kazi ya Roho Mtakatifu hatua kwa hatua, na ingawa nilitaka kubadilisha hali yangu mwenyewe, sikuweza.
Siku moja, nilipokuwa nikila na kunywa neno la Mungu, niliona maneno Yake yaliyosema: “Wakati baadhi ya watu walipotenda wajibu wao mara ya kwanza, walijaa nguvu, kana kwamba haingewahi kuishiwa na nguvu hizo. Lakini inakuwaje kwa kadri wanapoendelea ndipo wanapoonekana kupoteza nguvu hizo? Mtu waliokuwa wakati huo na mtu waliye sasa ni sawa na watu wawili tofauti. Kwa nini walibadilika? Sababu ilikuwa gani? Ni kwa sababu imani yao kwa Mungu ilienda njia mbaya kabla ya kufikia njia sahihi. Waliichagua njia mbaya. Kulikuwa na jambo lililokuwa limefichwa ndani ya kufuatilia kwao kwa kwanza, na kwa wakati mwafaka jambo hilo likaibuka. Nini kilikuwa kimefichwa? Ni matarajio yanayokuwa ndani ya mioyo yao wakati wakimsadiki Mungu, matarajio kwamba siku ya Mungu inawadia hivi karibuni ili taabu yao itafika mwisho; matarajio kwamba Mungu atabadilika na kwamba mateso yao yote yataisha” (“Wale Ambao Wamepoteza Kazi ya Roho Mtakatifu Ndio Walio katika Hatari Kubwa Zaidi” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Maneno ya Mungu yalinifanya nitafute mzizi wa tatizo hilo. Ilibainika kuwa nilikuwa na matumaini yaliyofichika ndani ya ufuatiliaji wangu, nikitumaini kwamba siku ya Mungu ingewadia hivi karibuni na kwamba singeweza kuteseka tena, kwamba ningekuwa na majaaliwa mazuri. Wakati huo wote, ufuatiliaji wangu ulitawaliwa na tumaini hili, na wakati ambapo matumaini yangu yalikuwa bure, niliteseka na kuvunjika moyo kiasi cha kumsaliti Mungu, hata kufikiri juu ya kuponyoka kupitia kifo. Ni wakati ule tu ndipo niliona kwamba nilikuwa nimemfuata Mungu kwa miaka mingi, lakini asili yake haikuwa kufuatilia njia ya kweli; daima nililenga siku ya Mungu, na nilikuwa nimefanya biashara na Yeye ili nipate baraka Zake. Hata ingawa wakati huo sikuwa na budi ila kukaa ndani ya nyumba ya Mungu na kutomwacha, ikiwa sikutatua uchafu ndani yangu, mapema au baadaye ningempinga na kumsaliti Mungu. Baada ya kuona hali yangu hatari, ndani ya moyo wangu nikamwuliza Mungu: Ninaweza kufanya nini ili kuondoa uchafuzi wa kutumaini siku ile? Kisha, nilisoma tena maneno ya Mungu, ambayo yalisema: “Je, ulijua kwamba kwa kumwamini Mungu huko Uchina, kuweza kupitia mateso haya na kuifurahia kazi ya Mungu, kwamba wageni huwa wanawaonea wivu kabisa nyinyi wote? Matamanio ya wageni ni: Tunataka pia kupitia kazi ya Mungu, tutateseka kwa vyovyote vile kwa sababu ya hilo. Tunataka kuupata ukweli pia! Tunataka pia kupata umaizi fulani, kupata kimo fulani, lakini kwa bahati mbaya hatuna yale mazingira. … Kulifanya kundi hili la watu kuwa kamili katika nchi ya joka kuu jekundu, kuwafanya kuvumilia mateso haya, kunaweza kusemekana kuwa utukuzaji mkubwa zaidi wa Mungu. Iliwahi kusemwa: ‘Nimeuleta utukufu Wangu kutoka Israeli hadi Mashariki kitambo.’ Je, nyinyi nyote mnaelewa maana ya kauli hii sasa? Mnafaa kuitembelea vipi njia iliyo mbele? Mnafaa kuufuatilia vipi ukweli? Kama hamfuatilii ukweli basi mnawezaje kuipata kazi ya Roho Mtakatifu? Pindi utakapopoteza kazi ya Roho Mtakatifu, basi utakuwa katika hatari kubwa zaidi. Mateso ya sasa si muhimu. Je, wajua yatakufanyia nini?” (“Wale Ambao Wamepoteza Kazi ya Roho Mtakatifu Ndio Walio katika Hatari Kubwa Zaidi” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Kutoka kwa maneno haya ya Mungu, niliweza kuona kwamba kuna maana kubwa kwa watu leo kuwa na uwezo wa kuteseka, lakini sikuweza kutambua maana ya mateso hayo kweli ilikuwa nini. Nilijua tu kwamba kama ningeweza tu kubaini maana ya mateso ndio ningeweza kwa kweli kubadilisha hali yangu ya kutarajia siku ya Mungu. Hii ilikuwa njia ya kuelekea katika azimio. Ingawa sikufahamu maana ya mateso wakati huo, jambo pekee ambalo ningeweza kufanya ilikuwa kufuatilia ukweli kabisa, kutafuta ukweli zaidi, kwa sababu ikiwa tu ningepata ukweli ndio ningeweza kuelewa kweli maana ya mateso, na ndipo basi ningeweza kuondoa uchafuzi huu ndani yangu.
Kama kwamba muda ulikuwa umeongeza kasi, nilipepesa na tayari ilikuwa mwaka wa 2009. Hiyo miaka saba ilikuwa imepita muda mrefu, bila mimi kugundua. Nilikuwa nimefika mbali hivyo na hatimaye nilihisi kwamba miaka hiyo saba haikuwa muda mrefu kama nilivyofikiri. Hiyo miaka michache, katika hukumu iliyofichuliwa katika maneno ya Mungu, katika ufunuo wa majaribu ya Mungu na usafishaji, nilikuwa nimeuona uso wangu wa kweli. Niliona kwamba nilikuwa, mtoto wa joka kuu jekundu kabisa, kwa sababu nilijawa na sumu lake, kama vile sumu ya “Usiamke mapema ikiwa hakuna faida, faida huongoza katika kila kitu.” Huu ni uwakilishi bora zaidi wa sura ya joka kuu jekundu. Chini ya utawala wa sumu hii, imani yangu kwa Mungu ilikuwa tu kubarikiwa. Niliyotumia kwa ajili ya Mungu kilikuwa na mpaka wa muda, na nilitamani kuteseka kidogo na kupata baraka kubwa. Ili kuniondolea nia hii thabiti ya kubarikiwa na mtazamo wa kibiashara uliokuwa ndani yangu, Mungu alikamilisha majaribio mengi na usafishaji kwangu. Wakati huo tu ndipo uchafu katika imani yangu kwa Mungu ulipotakaswa. Na nikaona ndani ya ufunuo wa Mungu kwamba nilikuwa nimejaa tabia mbaya ya Shetani. Nilikuwa na kiburi, udanganyifu, ubinafsi na mwenye kustahili dharau, mzembe, na mwenye shingo upande. Yalinifanya nione wazi zaidi na zaidi hali yangu halisi, kuona kwamba nilikuwa nimepotoshwa sana na Shetani, kwamba nilikuwa mwana wa kuzimu. Kwamba ningeweza kumwamini Mungu na kumfuata Mungu wakati huo ilikuwa kweli kukuzwa na Yeye na neema, na kwamba ningeweza kukubali hukumu na kuadibiwa na Yeye vilikuwa baraka kubwa zaidi. Shukrani yangu kwa Mungu ilikua, mahitaji yangu yakawa madogo, utiifu wangu Kwake ukakua, na kujipenda kwangu mwenyewe kukapungua. Niliomba tu kuwa na uwezo wa kupoteza tabia yangu potovu ya kishetani, kuwa mtu ambaye anamtii na kumwabudu Mungu kweli. Tokeo hili dogo lilipatikana baada ya kazi nyingi ya Mungu isiyojulikana kiasi, ikiwa ni pamoja na jitihada Zake nyingi sana. Hadi leo, kupitia kazi ya Mungu, nimekwisha kufahamu kwamba wokovu wa watu kwa kweli si rahisi. Kazi Yake ni ya vitendo sana—kazi Yake ya kuwabadilisha na kuwaokoa wanadamu sio rahisi kama ambavyo watu wangefikiria. Hivyo, sasa mimi si kama mtoto mjinga, kutumaini tu kwamba siku ya Mungu itakuja kwa haraka, lakini daima ninahisi kuwa upotovu wangu ni mkubwa sana, kwamba ninahitaji sana wokovu wa Mungu na ninahitaji sana kupitia hukumu na kuadibiwa na Yeye, majaribio Yake na usafishaji Wake. Lazima sasa niwe na dhamiri kidogo na mantiki ambavyo vinapaswa kuwepo katika ubinadamu wa kawaida, na kikamilifu kuipitia kazi ya Mungu ya wokovu wa wanadamu. Mwishoni wakati ambapo nitaweza kuishi kwa kudhihirisha mfano wa mtu wa kweli na kupokea furaha ya Mungu, moyo wangu utatimizwa. Sasa, ninapoangalia nyuma na kufikiri juu ya kile nilichofichua juu yangu wakati ambapo miaka hiyo saba ya majaribio ilinijia, ninahisi kwamba nina deni kubwa kwa Mungu, kwamba niliujeruhi moyo Wake sana. Kama kazi ya Mungu ingekamilika mwaka 2000, mimi, ambaye nilikuwa mchafu sana kabisa, hakika ningeangamizwa. Miaka saba ya majaribio kweli ilikuwa uvumilivu wa Mungu na huruma kwangu, na aidha, ilikuwa ni wokovu wa Mungu wa kweli zaidi na halisi zaidi kwangu.
Mara nilipokuwa nimetoka katika miaka hiyo saba na nilitafakari maneno hayo kutoka kwa Mungu ambayo sikuwa nimeyaelewa awali: “Je, ulijua kwamba kwa kumwamini Mungu huko Uchina, kuweza kupitia mateso haya na kuifurahia kazi ya Mungu, kwamba wageni huwa wanawaonea wivu kabisa nyinyi wote? Matamanio ya wageni ni: Tunataka pia kupitia kazi ya Mungu, tutateseka kwa vyovyote vile kwa sababu ya hilo. Tunataka kuupata ukweli pia! Tunataka pia kupata umaizi fulani, kupata kimo fulani, lakini kwa bahati mbaya hatuna yale mazingira. … Kulifanya kundi hili la watu kuwa kamili katika nchi ya joka kuu jekundu, kuwafanya kuvumilia mateso haya, kunaweza kusemekana kuwa utukuzaji mkubwa zaidi wa Mungu. Iliwahi kusemwa: ‘Nimeuleta utukufu Wangu kutoka Israeli hadi Mashariki kitambo.’ Je, nyinyi nyote mnaelewa maana ya kauli hii sasa?” Niliweza kuelewa maana kidogo ya maneno haya; niliweza hatimaye kuhisi kuwa mateso ni yenye umuhimu kweli. Ingawa niliteseka nilipopitia majaribio haya, baada tu ya kuteseka ndipo niliona kwamba kile nilichopata kilikuwa cha thamani sana, muhimu sana. Kwa kupitia majaribio haya, niliona tabia yenye haki ya Mwenyezi na uweza wa Mungu na hekima. Nilielewa ukarimu wa Mungu, na nilionja upendo wa kina, wa baba wa Mungu kwa watoto Wake. Pia nilipitia mamlaka na nguvu katika maneno Yake, na niliona ukweli wa kupotoshwa kwangu na Shetani. Niliona dhiki ya Mungu katika kazi Yake ya wokovu, kwamba Yeye ni mtakatifu na mwenye kuheshimiwa, na kwamba watu ni wabaya na wa kudharauliwa. Pia nilipitia jinsi Mungu anavyoshinda na kuwaokoa wanadamu ili kuwaleta kwenye njia sahihi ya kumwamini. Ninapolifikiria sasa, kama Mungu hakuwa amefanya kazi hii ngumu ya majaribio kwangu baada ya majaribio, nisingeweza kuwa na ufahamu huu. Dhiki na usafishaji vina manufaa katika ukuaji wa watu katika maisha yao. Kwa kuvipitia, watu wanaweza kupata kitu cha maana na cha thamani sana katika kipindi chao cha kumwamini Mungu—ukweli. Baada ya kuona thamani na maana ya mateso, mimi tena sina ndoto ya kuingia katika ufalme nikiwa nimeabiri motokaa, lakini nina nia ya kusimamisha imara miguu yangu na kupitia kazi ya Mungu, kufuatilia kwa kweli ukweli ili kujibadili.
Kwa kupitia miaka kadhaa ya kazi ya Mungu, ndipo sasa tu nina ufahamu mdogo wa vitendo wa maneno haya kutoka kwa Mungu: “Imani ya kweli katika Mungu ina maana kupitia maneno na kazi ya Mungu kwa msingi wa imani kuwa Mungu ndiye mkuu juu ya vitu vyote. Kwa hivyo mtawekwa huru kutokana na tabia yenu ya upotovu, mtatimiza hamu ya Mungu, na mtapata kumjua Mungu. Ni kwa kupitia safari ya aina hii tu ndio mnaweza kusemekana kuwa mnaamini katika Mungu” (Dibaji wa Neno Laonekana katika Mwili). Kabla ya kupitia majaribio haya kutoka kwa Mungu, nilikuwa nimejaa nia kali ya kubarikiwa na mtazamo wa kishughuli. Hata ingawa nilijua kikanuni kuamini katika Mungu kulikuwa nini na lengo la imani katika Mungu lilikuwa nini, bado nilikuwa nimelenga tu kubarikiwa. Sikujali ukweli, sikuondoa tabia yangu potovu ili kuyakidhi mapenzi ya Mungu, au kumtambua Mungu kama lengo la ufuatiliaji wangu. Ni wakati ule tu ndipo nilielewa kwamba Mungu alipokuwa mwili kazi Yake ya msingi ilikuwa kutatua nia ya wanadamu ya kubarikiwa na mtazamo wao wa kishughuli. Ilikuwa ni kwa sababu mambo haya kweli ni vikwazo kati ya wanadamu na kuingia kwao kwenye njia sahihi ya kumwamini Mungu. Mambo haya yanapofichwa ndani ya wanadamu, hawatafuatilia ukweli. Hawatakuwa na lengo sahihi katika ufuatiliaji wao; watatembea katika njia isiyo sahihi. Hii ni njia ambayo haitambulikani na Mungu. Sasa, kazi ya Mungu ya kushinda na wokovu imeharibu ngome ya Shetani ndani yangu. Hatimaye sina wasiwasi tena, sina tena fikira za kupatia baraka au kupitia janga. Sifuatilii tena kwa uchungu tamaa zilizopita kiasi, na sizungumzii tena masharti au kutoa mahitaji ili kuepuka janga hilo. Bila uchafu huu, najihisi mwepesi, huru. Ninaweza kufuatilia ukweli kwa utulivu na kikamilifu. Hili ndilo tunda lililotokana na majaribio na usafishaji wa Mwenyezi Mungu. Ni kazi ya Mwenyezi Mungu ya majaribio na usafishaji ambavyo vimeniongoza kwenye njia ya kweli ya kumwamini Mungu. Kuanzia sasa kuendelea, bila kujali kazi zaidi ya majaribio ambayo Mungu hufanya, bila kujali jinsi usafishaji wenye maumivu ninaoupitia, nitatii na kukubali, na kuyapitia kwa kweli. Nitatafuta ukweli kutoka kwazo, na kufikia tabia isiyo na upotovu ili kukidhi mapenzi ya Mungu, ili kulipiza miaka mingi ya Mungu ya juhudi ya bidii.
Tanbihi:
a. Nakala asili inaacha “kama vile.”
Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo

Jumatano, 12 Juni 2019

Hukumu ni Mwanga

Wokovu wa Mungu, Mkristo, Ushuhuda wa Maisha

Zhao Xia Mkoa wa Shandong
Jina langu ni Zhao Xia. Nilizaliwa katika familia ya kawaida. Kutokana na ushawishi wa misemo kama “Mtu huacha jina lake nyuma popote akaapo, kama vile bata bukini hutetea popote arukapo,” na “Kama vile mti huishi kwa sababu ya ganda lake, mtu huishi kwa sababu ya uso wake,” sifa na heshima zikawa muhimu sana kwangu. Kila kitu nilichofanya kilikuwa ili kupata sifa, pongezi, na upendezwaji wa watu wengine. Baada ya kuolewa, malengo niliyojiwekea yalikuwa: Nitaishi maisha ya kitajiri zaidi kuliko wengine; Ni lazima nisiruhusu mtu yeyote kusema mambo hasi kuhusu jinsi ninavyowatendea wazee au kuhusu tabia na mwenendo wangu; na nitahakikishia mtoto wangu ataingia katika chuo kikuu cha kifahari na ana matarajio mazuri, ili kuongeza fahari zaidi katika heshima yangu. Kwa hivyo, sikuwahi kugombana na wakwe wangu. Mara nyingine, wakati walisema maneno makali kwangu, ningehisi nimekerwa mno mpaka ningejificha na kulia badala ya kuwapa uhasi. Wakati niliona wengine wakiwanunulia wazazi wao nguo wakati wa Mwaka Mpya wa Kichina na sikukuu zingine, ningeenda mara moja kumnunulia mama mkwe wangu baadhi, na ingekua pia ya ubora wa hali ya juu. Wakati jamaa walikuja kunitembelea, ningesaidia kununua vyakula na kupika. Hata wakati ilikuwa ngumu na ya kuchosha kiasi bado ningekuwa radhi kabisa. Nikihofia kuwa ningekuwa na utajiri kiasi kuliko wengine, niliacha mtoto wangu wa kike nyuma mwezi mmoja baada ya kumzaa na kurudi mara moja kazini. Matokeo yake yakawa, binti yangu alipata maumivu ya utapiamlo na akawa tu ngozi na mifupa kwa sababu hangeweza kunywa maziwa ya matiti yangu. Hali yake iliimarika tu baada ya sindano 100 za lishe, ilhali nilikuwa nimechoka sana kiasi kwamba nilikuwa na maumivu ya mgongo kila siku. Ingawa ilikuwa ngumu na yenye kuchokesha, nilivumilia shida hizo na nilijitolea kwa bidii kwa ajili ya kupata sifa nzuri. Katika miaka michache tu, nikawa mkwe maarufu katika kijiji, na familia yangu ikawa tajiri na kuonewa kijicho na watu walio karibu nasi. Matokeo yake yakawa, wakwe zangu, majirani, jamaa na marafiki wote walinisifu sana. Katika kukabiliwa na sifa na taadhimu kutoka kwa wale walio karibu nami, kiburi changu kilitoshelezwa sana. Nilihisi shida zangu wakati wa kipindi cha miaka michache iliyopita hazikuwa za bure, na nilikuwa nimefurahishwa sana kindani. Hata hivyo, maisha yangu ya utulivu yalikatishwa baada ya shemeji wangu kuolewa. Mke wake alinena nami kwa kejeli daima, akisema kuwa nilikuwa na nia fiche kwa kumtendea mama mkwe wetu vyema kwa sababu nilikuwa nataka tu mali yake. Yeye alikuwa akisema kila mara kuwa mama mkwe wetu alikuwa na upendeleo kwani alitupa sisi vitu vingi zaidi kuliko alivyowapa wao, na mara nyingi tulikuwa tukigombana kwa sababu ya haya. Nilihisi kuudhika mno na nilitaka kubishana naye hadharani ili kulalamika kutokuwa na hatia kwangu, lakini ingeweza kuharibu picha nzuri niliyokuwa nimejenga ndani ya mioyo ya watu. Kwa hivyo, ningejizuia kwa lazima, na wakati singeweza kuvumilia tena ningekuwa na kilio kikubwa kwa faragha. Baadaye, wifi huyo alisukuma bahati yake kwa kumiliki ardhi iliyosambazwa kwa upande wangu wa familia, iliyonifanya nitingike kwa hasira na nisikule au kunywa kwa masiku. Nilitaka hata pia kupambana naye hadi suluhu ipatikane. Hata hivyo, nikifikiria kwamba ingeweza kunifanya kupoteza heshima, kuharibu sifa yangu, na kufanya wale walio karibu nami kunidharau, nilimeza hayo yote, lakini ndani nilihisi nimekazwa mno kiasi kwamba nilikuwa na maumivu. Nilionekana mwenye majonzi na nilitanafusi siku nzima, nikihisi kama ilikuwa chungu sana na ya kuchosha kuishi na kutojua wakati kungekuwa na mwisho kwa maisha kama hayo.
Mwisho wa binadamu kweli ndio mwanzo wa Mungu. Pindi wakati nilikuwa na maumivu na kuhisi mnyonge, Mwenyezi Mungu alinyoosha mikono Yake ya wokovu kwangu. Siku moja, jirani yangu aliniuliza: “Unaamini katika uwepo wa Mungu?” Nilijibu: “Nani asiye? Ninaamini Mungu yupo.” Kisha akasema kwamba Mungu anayeamini ndiye Mungu pekee na wa kweli aliyeumba ulimwengu na vitu vyote, na kwamba mwanzoni, binadamu waliishi katika baraka za Mungu kwa sababu walimwabudu Mungu, lakini baada ya wao kupotoshwa na Shetani, hawaabudu tena Mungu na ndivyo basi wanaishi chini ya laana na maumivu kwa Mungu. Mwenyezi Mungu wa siku za mwisho alikuja kuwapa watu ukweli na kuwaokoa kutoka kwenye lindi kuu la taabu. Kwa kuongezea, pia aliwasiliana uzoefu wake mwenyewe wa kumwamini Mungu. Baada ya kusikiza mawasiliano yake, nilihisi kuwa nimepata msiri wangu wa karibu sana, na singeweza kujizuia kuelezea maumivu yote moyoni mwangu. Baadaye, alinisomea kifungu cha neno la Mungu: “Unapokuwa umechoka na unapoanza kuona huzuni katika ulimwengu huu, usifadhaike, usilie. Mwenyezi Mungu, Mlinzi, atakaribisha kuwasili kwako wakati wowote. Yuko kandokando yako akiangalia, akikusubiri urudi. Anasubiri siku ambayo kumbukumbu yako itarejea: ukiwa na utambuzi wa ukweli kwamba ulitoka kwa Mungu, kwa namna fulani na mahala fulani ulipopotea kwa wakati mmoja, ukianguka barabarani ukiwa hujitambui, halafu pasipo kujua unakuwa na baba. Unatambua zaidi kuwa mwenye Uweza amekuwa akiangalia, akisubiri kurejea kwako muda huu wote” (“Kutanafusi kwa Mwenye Uweza” katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yalitiririka ndani ya moyo wangu kama mkondo wenye joto, yakituliza moyo wangu wenye uchungu na huzuni, na singeweza kuzuia machozi yangu kumwagika. Wakati huo huo, nilihisi kama mtoto aliye na mateso aliyepotea na aliyerudi kwa ghafla katika kumbatio la mama yake. Kulikuwa na msisimko usioweza kusemeka na mhemuko katika moyo wangu. Niliendelea kumshukuru Mungu, kwa sababu alinichukua katika nyumba Yake na kunijalia wakati sikuwa na pengine pa kwenda. Nitafuata Mungu kwa moyo na roho yangu! Tangu wakati huo, nilisoma maneno ya Mungu, nikamwomba Mungu, na niliimba nyimbo za kumsifu Mungu kila siku, mambo yalilonifanya kutulia hasa katika moyo wangu. Kwa kuhudhuria mikutano, niliona kuwa ndugu walikuwa kama familia kubwa, ingawa wao hawana uhusiano wa damu. Uingiliano wao ulikuwa wa kawaida na wazi, ulikuwa umejaa uelewa, ustahamilivu, na uvumilivu, na haukuwa na wivu, mgongano na kupanga njama au kisingizio na unafiki. Hawakuwadhulumu maskini ilhali wakipenda matajiri, na wote waliweza kutendea kila mtu na unyofu na usawa. Moyo wangu ungehisi huru hasa wakati tuliimba nyimbo za kumsifu Mungu pamoja. Kwa sababu hiyo nilipendezwa na maisha haya ya kanisa yenye upendo na ukunjufu, ya haki na yenye furaha. Nilisadiki kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Mungu pekee wa kweli na nilifanya uamuzi wangu kuwa ningemfuata hadi mwisho.
Kupitia kusoma maneno ya Mungu, nilielewa hamu ya haraka ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu kwa kiwango kikubwa kiwezekanavyo, na kuona kwamba ndugu wengi walikuwa wakifanya kila liwezekanalo kujitoa na kujitumia kwa ajili ya kueneza injili ya ufalme. Hivyo basi pia nikajihusisha kikamilifu katika kuhubiri injili. Ili kunitakasa na kunibadili mimi, Mungu alilenga asili yangu mbovu na alitekeleza adabu na hukumu Yake juu yangu mara kwa mara. Wakati mmoja, nilikwenda kuhubiri injili kwa aliyeweza kuwa mwaminifu. Ilikuwa msimu wa kilimo wenye shughuli nyingi wakati huo. Baada ya kuona jinsi alivyokuwa na shughuli nyingi za kilimo, nilienda kufanya kazi pamoja naye huku nikimpa ushuhuda wa kazi ya Mungu ya siku za mwisho. Nani angejua ya kwamba baada ya kuzungumza naye kwa siku tatu mtawalia angekuwa hana nia ya kuukubali tu na badala yake angenikaripia: “Wewe huna haya hata! Mimi tayari nilisema siyaamini haya, na bado huachi kuhubiri.” Maneno yake yaliniumiza sana. Uso wangu ulichomeka ni kama nilikuwa nimechapwa makofi mara kadhaa hadharani, wakati moyo wangu uliuma na wimbi baada ya wimbi la maumivu hafifu yasiyo makali. Nilifikiria: Nilikuja kukuhubiria kwa nia njema na nilijichokesha nilipokusaidia na kazi yako hadi mgongo wangu ulipata maumivu, na bado badala ya kukubali hayo, ulinitendea hivi. Wewe ni katili kweli! Nilihisi nimeaibishwa mno na sikutaka kuzungumza naye tena, lakini pia nilihisi kuwa hii haikuwa inaambatana na nia za Mungu, kwa hivyo niliomba kwa ukimya moyoni mwangu na nilizuia maumivu yangu ya kindani ili kuendelea kuongea naye nilipokuwa nikimsaidia na kazi yake. Hata hivyo, haidhuru kwa bidii gani niliwasiliana sikuweza bado kumfikia. Niliporomoka kama mpira uliotolewa upepo niliporudi nyumbani. Maneno ya mlengwa wa mahubiri yangu yaliendelea kujitokeza kichwani mwangu. Nilivyofikiria zaidi kuhusu hayo ndivyo nilivyoteseka zaidi: Mbona ninajisumbua? Yote niliyoyapata kama malipo ya nia yangu njema yalikuwaa kuzomewa, kukashifiwa, na kunyanyaswa. Kwa kweli hii sio haki kabisa! Hakuna mtu aliyewahi kunitenda namna hii. Kueneza injili ni uchungu na ngumu kabisa! Hapana, siwezi kwenda nje kuhubiri injili tena! Ikiwa nitaendelea kuhubiri sitabaki na heshima yoyote ya kuona mtu yeyote. Wakati tu nilipohisi nimekosewa sana na mwenye maumivu kiasi kwamba sikuwa na hiari tena ya kuhubiri injili, maneno ya Mungu yalinipatia nuru: “Je, unajua mzigo ulio begani mwako, kazi yako na majukumu yako? Hisia yako ya kihistoria ya mwito iko wapi? … Wao ni masikini, wa kuhurumiwa, vipofu na waliopotea na wanalia gizani, ‘Njia iko wapi?’ Jinsi gani wanatamani mwangaza, kama nyota iangukayo kutoka angani, ianguke ghafla na kutawanya nguvu za giza zilizowakandamiza wanadamu kwa miaka mingi. Ni nani anayeweza kujua jinsi wanavyotumaini kwa hamu, na wanavyotamani hili usiku na mchana? Wanadamu hawa wanaoteseka mno wamebaki wafungwa katika jela za giza, bila tumaini la kuwachiliwa huru, hata ile siku ambayo mwanga utaonekana; ni lini hawatalia kwa uchungu tena? Roho hizi dhaifu ambao kamwe hazijapewa pumziko kwa hakika zinateseka na bahati hii mbaya. Kwa muda mrefu wamefungiwa nje na kamba zisizo na huruma na historia iliyokwama katika wakati. Ni nani amewahi kusikia sauti ya vilio vyao? Ni nani amewahi kuona nyuso zao zenye taabu? Umewahi kufikiria jinsi moyo wa Mungu ulivyosononeka na ulivyo na wasiwasi? Anawezaje kustahimili kuona mwanadamu asiye na hatia, Aliyemuumba kwa mikono Yake Mwenyewe akiteswa na makali? Mwishowe, wanadamu ndio wasio na bahati na waliopewa sumu. Hata ingawa wamenusurika mpaka siku hii, ni nani angefikiri kuwa wamepewa sumu na yule mwovu kwa muda mrefu? Je, umesahau kuwa wewe ni mmoja wa waathiriwa? Kwa ajili ya upendo wako kwa Mungu, una nia ya kufanya kila uwezalo kuwaokoa walionusurika? Je, huna nia , ya kutumia nguvu zako zote kulipiza Mungu anayempenda binadamu kama nyama na damu Yake Mwenyewe?” (“Unapaswa Kushughulikiaje Wito Wako wa Mustakabali?” katika Neno Laonekana katika Mwili). Mistari katikati ya maneno ya Mungu yote yalifichua hangaiko Lake na huzuni Yake yenye masikitiko na ya kuwajali watu wasio na hatia. Mungu hawezi kuvumilia kuona watu walioumbwa kwa mikono Yake mwenyewe wakidanganyika na kuumizwa na Shetani. Mungu anaendelea kusubiri kwa hamu sana kwa wanadamu kurudi katika nyumba Yake hivi karibuni ili wapokee wokovu mkubwa amewafadhili. Ilhali wakati nilipopatwa na maneno machache makali kutoka kwa mlengwa wangu wa mahubiri, nilihisi nimekosewa na kuteswa na nililalamika kuhusu shida na mateso hayo. Nilikuwa hata tena sina radhi ya kushirikiana kwa sababu nilikuwa nimefedheheka. Dhamiri na mantiki yangu ilikuwa wapi? Ili kutuokoa sisi watu potovu katika siku za mwisho, Mungu ameendelea kuwindwa na kuteswa na serikali kwa kila mara, kutelekezwa, kushutumiwa, kukufuriwa na kukashifiwa na jamii ya dini, na kuelewa visivyo na kupingwa na sisi wafuasi wa Mungu. Yale machungu na aibu Mungu amepitia ni mengi sana, ni mengi kabisa! Hata hivyo, Mungu hakuachana na wokovu Wake wa wanadamu, na aliendelea kutoa mahitaji ya wanadamu katika utulivu. Upendo wa Mungu ni mkubwa sana! Nafsi yake ni nzuri sana na yenye ukarimu! Taabu zangu leo haziwezi kulinganishwa na mateso ambayo Mungu amepitia kwa ajili ya kuokoa mwanadamu! Nilikumbuka kuwa mimi nilikuwa pia mwathiriwa, mtu yule aliyekuwa amedhuruiwa na Shetani kwa miaka. Kama Mungu hangekuwa amenyoosha mikono Yake ya wokovu kwangu, ningekuwa bado ninang’ang’ana kwa uchungu katika giza, nisiweze kupata mwanga na matumaini ya kuishi. Kwa kufurahia wokovu wa Mungu, ninapaswa kuubeba aibu na maumivu ili kufanya lote liwezekanalo kushirikiana na Mungu, kutekeleza wajibu wangu vizuri, na kuleta watu wale wasio na hatia na bado wanadhuruiwa na Shetani mbele za Mungu. Hii ni ya thamani na ya maana zaidi kuliko kazi yoyote duniani, na ni ya kufaa haijalishi ni mateso ngapi yanapaswa kuvumiliwa! Nilipofikiria juu ya haya, sikuhisi tena kwamba kuhubiri kwa injili ni kitu chenye uchungu, na badala yake nilihisi mwenye bahati kuwa na uwezo wa kuratibu na injili ya ufalme. Huu ulikuwa heshima yangu na pia kuinuliwa na Mungu. Nilifanya uamuzi wangu: Bila kujali aina gani ya shida nitakayopatana nayo katika kazi yangu ya injili, nitajitolea yangu yote na kumtegemea Mungu kuwaleta watu zaidi na zaidi wenye shauku ya Mungu mbele Yake ili kufariji moyo Wake! Baadaye, nilijirusha mwenyewe tena katika kazi ya injili tena.
Kufuatia kipindi cha mafunzo, kila nilipokutana na mlengwa wa mahubiri ambaye alikuwa na mtazamo mbaya au aliyeninenea maneno makali wakati wa kutekeleza wajibu wangu, ningekuwa na uwezo wa kukabiliana na hilo kwa njia sahihi na kuendelea kushirikiana na moyo wa upendo. Kwa sababu ya haya, nilihisi nilikuwa nimebadilika na sikuwa ninajali tena kuhusu heshima na hadhi. Lakini wakati Mungu aliweka mazingira mengine ya kunijaribu kulingana na kile nilichohitaji katika maisha, nilifichuliwa kabisa tena. Siku moja, kiongozi wa kanisa alinijulia hali hivi karibuni na pia alizungumzia nia za Mungu za wakati uliopo na njia ya utendaji. Wakati niligundua wakati wa mazungumzo kuwa alikuwa anahamishwa katika kanisa lingine ili kutimiza wajibu wake, singeweza kujisaidia kuhisi wimbi la msisimko: Kuna uwezekano kuwa nitafanywa kuwa kiongozi wa kanisa baada ya yeye kuondoka. Ikiwa ndivyo, ni lazima kabisa nishirikiane vizuri! Wakati tu nilipokuwa ninahisi furaha kisiri, dada huyo alisema kuwa dada mwingine katika kijiji changu angetutembelea kesho. Nilikuwa na wasiwasi mara tu niliposikia hayo: Anakujia nini? Yeye ndiye atafanywa kuwa kiongozi mpya wa kanisa? Singeweza kujizuia kuwa na wasiwasi: Hajakuwa akimwamini Mungu kwa muda mrefu kama vile nimefanya, na pia anakuja kutoka kijiji hicho kama mimi. Ikiwa yeye atafanywa kiongozi, basi heshima yangu itakuwa aje? Ndugu wataniona namna gani? Kwa hakika watasema kuwa mimi huwa sifuatilii ukweli kwa kiwango chake. Sikuweza kuacha kufikiria juu ya hayo. Niligaagaa na kugeuka kitandani usiku, nisiweze kulala. Wakati wa mkutano siku iliyofuata, nilitia makini mara kwa mara sauti na mtazamo wa kile kiongozi alikuwa akisema kwa sababu nilitaka kujua kwa hamu ni nani angechaguliwa kuwa kiongozi mpya wa kanisa. Kila wakati kiongozi huyo aliniangalia alipozungumza, nilihisi tumaini la kufanywa kuwa kiongozi. Sura yangu ingejawa na furaha na ningekubali kwa kichwa na kukubaliana na chochote alichosema. Kwa upande huo mwingine, wakati wowote kiongozi huyo alitazama dada huyo mwingine alipokuwa akizungumza, ningekuwa na uhakika kuwa dada huyo angetajwa kama kiongozi, na ningehisi huzuni na kuwa na masumbuko makali kwa sababu ya hilo. Wakati wa siku hizo chache, nilikuwa nimeteseka kwa ajili ya heshima na hadhi sana hadi nikawa na wasiwasi na kuchanganyikiwa. Nilipoteza hamu yangu ya kula na hata nikahisi kama muda ulikuwa unapita hasa polepole, ni kama ulikuwa umeganda. Kiongozi wa kanisa aliweza kuona hali niliyokuwa katika, kwa hivyo alipata kifungu cha neno la Mungu niweze kusoma: “Sasa nyinyi ni wafuasi, na mna ufahamu fulani wa hatua hii ya kazi. Hata hivyo, bado hamjaweka kando tamaa yenu ya hadhi. Wakati hadhi yenu iko juu mnatafuta vizuri, lakini wakati hadhi yenu iko chini hamtafuti tena. Baraka za hadhi daima ziko katika fikira zenu.” “Ingawa mmefikia hatua hii leo, bado hamjaiacha hadhi, lakini daima mnapambana kuuliza kuihusu na kila siku mnaichunguza…. Kadiri unavyotafuta zaidi kwa njia hii ndivyo utavyovuna kidogo zaidi. Kadiri ilivyo kubwa zaidi tamaa ya mtu ya hadhi, ndivyo itabidi washughulikiwe kwa uzito zaidi na ndivyo zaidi lazima wapitie usafishaji mkubwa. Mtu wa aina hiyo hana thamani kabisa! Lazima ashughulikiwe na ahukumiwe vya kutosha ili aache hilo kabisa. Mkifuatilia kwa njia hii mpaka mwisho, hamtavuna chochote. Wale ambao hawafuatilii maisha hawawezi kubadilishwa; wale ambao hawana kiu ya ukweli hawawezi kupata ukweli. Hulengi kufuatilia mabadiliko ya kibinafsi na kuingia ndani; daima wewe hulenga tamaa zile badhirifu na vitu vinavyozuia upendo wako kwa Mungu na kukuzuia kufika karibu na Yeye. Je, vitu hivyo vinaweza kukubadili? Je, vinaweza kukuleta katika ufalme?” (“Mbona Huko Tayari Kuwa Foili[a]?” katika Neno Laonekana katika Mwili). Kila mstari wa maneno ya Mungu uligonga moyo mwangu, ukinifanya nihisi kuwa Mungu alikuwa kando yangu, akifuatia kila neno na mwenendo wangu. Singeweza kujizia ila kujitafakari kwa mawazo na utendaji wangu siku hizi mbili zilizopita. Niligundua kuwa mtazamo wangu wa ufuatiliaji ulikuwa mbovu sana na uliathiriwa na misemo kama “Kama vile mti unavyoishi kwa sababu ya gome lake, mtu huishi kwa sababu ya uso wake,” na “Mtu huacha jina lake nyuma mahali popote anapoishi, kama vile bata bukini hunena kilio chake popote anapoburuka.” Siku zote nilitaka hadhi ili nipate kushinda sifa zaidi kutoka kwa wengine, kilichosababisha mimi kuteseka kwa ajili ya heshima na hadhi kiasi kwamba nilikuwa na wasiwasi na kuchanganyikiwa, nilipoteza hamu yangu ya kula na singeweza kulala, na nilijifanya kuonekana mpumbavu. Hali kama hiyo ilitengenezwa na Mungu kulingana na hali yangu. Ilikuwa upendo wa Mungu ukiniangukia. Kazi ya Mungu leo ilikuwa ya kuniokoa, kunisaidia kuepuka ushawishi wa giza wa Shetani ili nipate kupata wokovu. Njia niliyokuwa nikifuatilia ilikinzana na mapenzi ya Mungu. Singekuwa na uwezo wa kupokea idhini ya Mungu hata kama ningemwamini hadi mwisho. Ningeachwa bila chochote! Kwa hivyo nilimwomba Mungu kwa ukimya: “Ewe Mungu! Niko radhi kutii kazi Yako, kutembea katika njia sahihi ya kuamini Mungu kwa mujibu wa mahitaji Yako, na kutia juhudi kwa neno Lako ili kufikia kuelewa ukweli na kuachana na tabia yangu mbovu. Bila kujali kama nimefanywa kiongozi, nitafuatilia ukweli na kutia makini kwa kubadili mambo yangu ambayo hayakidhi malengo Yako.” Baada ya kuelewa makusudi ya Mungu, nilihisi hasa utulivu moyoni mwangu na nilifurahia kuwasiliana bila kujali maudhui yalikuwa gani. Baada ya mkutano, kiongozi wa kanisa alisema kuwa, kulingana na mapendekezo ya wengi wa ndugu, dada huyo angekuwa kiongozi mpya wa kanisa, na kuwa ningeweza kuratibu na kazi yake. Nilikuwa na utulivu sana ndani na kukubali bila kusita, kukubali kufanya kazi kwa upatanifu na dada huyo ili kutimiza wajibu wetu.
Baada ya kupitia adabu na hukumu ya Mungu wakati huu, nilipata ujuzi fulani juu ya mwelekeo wangu wa kuzingatia heshima na hadhi, na nilikuwa radhi kuachana na mwili wangu na kumwamini Mungu na kutekeleza wajibu wangu kulingana na mahitaji Yake. Hata hivyo, uchafu wangu uliotokana na sumu za Shetani zilikuwa zimezama sana. Kina cha nafsi yangu bado kilikuwa kinatawaliwa na ushawishi wa Shetani. Ili kuniokoa vyema kutoka kwa madhara ya Shetani, Mungu aliinyoosha mikono Yake ya wokovu kwangu tena. Siku moja, niliambiwa kuwa kulikuwa na dada katika kanisa ambaye hakuwa katika hali nzuri, kwa hiyo nilishauriana na dada niliyeshirikishwa naye kuhusu jinsi ya kutatua shida hii. Kwa sababu dada niliyeshiriki naye hakuhisi vizuri, nilikwenda peke yangu kutatua tatizo hilo baada ya majadiliano yetu. Nilimtafuta dada huyo usiku uo huo ili kuwasiliana naye, na tatizo hilo lilitatuliwa haraka sana. Moyo wangu ulibubujikwa kwa furaha wakati huo, nikifikiri kuwa kiongozi wa ngazi ya juu angenisifu kwa hakika kwa sababu nilikuwa nimetia jitihada nyingi sana. Hata hivyo, wakati tu nilipokuwa nikisubiria habari njema, kiongozi wa ngazi ya juu aliandika barua akitaka kuelewa hali ya dada huyo. Nilifikiria ilikuwa ni kunisifu, kwa hiyo niliifungua kwa furaha na kuisoma. Lakini nilipoona kuwa kile kilichokuwa ndani ya barua kilikuwa hasa cha kuuliza dada mwenzi vile alivyoshughulikia tatizo hilo, mara moja nikawa mwenye uchungu: Kwa uwazi ni mimi niliyeshughulikia suala hilo. Mbona usiniandikie kuniuliza juu ya hilo? Inaonekana mimi sina nafasi katika moyo wa kiongozi na ninadharauliwa. Mimi ni msichana wa kibaraka tu. Haijalishi jinsi ninavyofanya vyema sipati sifa njema yoyote kwa sababu hakuna mtu anayelizingatia kwa makini. Nilivyofikiria zaidi juu ya hilo, ndivyo nilihisi zaidi nilikuwa nimekosewa na kuhuzunika. Nilihisi nimefedheheshwa. Wakati huu, dada yangu mwenzi alikuwa na barua mkononi mwake na alikuwa karibu kuzungumza nami. Singeweza kuzuia hisia zilizokuwa ndani yangu na nikampigia kelele: “Kiongozi wa ngazi ya juu hajui jinsi suala hili lilivyotatuliwa. Hujaelewa haya? Nililifanya kazi kwa bidii kwa muda mrefu lakini hakuna hata mmoja aliyesema neno jema kulihusu, na hatimaye wewe bado ulipata sifa zote. Mbele ya kila mtu, mimi ni mtu tu wa kutumwa na kusaidia. Haijalishi ninaliwekea jitihada gani, hakuna mtu atakayelifurahia.” Baada ya kusema haya, nilihisi mwenye kudhulumiwa sana hadi nikaangua kilio. Wakati huo, maneno ya Mungu yalirudiarudia katika masikio yangu: “Kama ulitumia juhudi nyingi lakini bado Sikuchangamkii, je, utaweza kuendelea kunifanyia kazi katika uvunguvungu? Ikiwa, baada ya wewe kutumia vitu fulani kwa ajili Yangu, Sijatimiza mahitaji yako madogomadogo, je, utavunjika moyo na kusikitishwa na Mimi au hata kuwa na ghadhabu na kunitusi?” (“Tatizo Zito Sana: Usaliti (2)” katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya kushutumu ya Mungu yalinituliza polepole, na mawazo yangu yalifumbuka sana pia. Tukio ambalo lilikuwa limetoka kutokea liliendelea kucheza tena katika mawazo yangu kama sinema. Ufunuo wa Mungu ulinifanya kuona kwamba asili yangu ni ya kutisha na ya hatari sana, na kwamba imani yangu kwa Mungu na kutekeleza kwa wajibu wangu haukuwa wa kuridhisha Mungu au kupokea idhini Yake, mbali kupokea sifa na taadhimu kutoka kwa watu wengine. Mara tu matamanio yangu hayakuwa yakitoshelezwa, ningekuwa mwenye kujaa chuki; asili yangu ya unyama ungejitokeza, na kumsaliti Mungu ikawa jambo rahisi sana kufanya hata zaidi. Wakati huu, niliona kuwa nimevuka mipaka sana na kwamba nilikuwa mkatili. Maumivu niliyoyahisi yalikuwa ya kuhuzunisha sana. Nilipotubu, nikamwomba Mungu: “Ewe Mungu, nilifikiri nilikuwa nimebadilika na sikuwa ninaishi tena kwa sababu ya heshima na hadhi, na pia ningeweza kushirikiana na dada huyo. Lakini katika ufunuo Wako leo, kwa mara nyingine tena nimeweza kufunua ubaya wangu wa kishetani, daima nikihisi kuwa sikuwa na hadhi kati ya watu na kuteseka kwa sababu jitihada zangu hazikusifiwa na wengine. Ee Mungu, Shetani kweli alikuwa amenidhuru sana. Hadhi, sifa, na majivuno yote yakawa pingu zangu. Ninaomba kuwa Unaweza kuniongoza kutoka kwa ushawishi wa Shetani tena.” Baadaye, niliona kati ya maneno ya Mungu yafuatayo: “Kila mmoja wenu amepanda vilele vya juu zaidi vya umati; ninyi mmepanda kuwa mababu wa umati. Ninyi ni wadhalimu mno, na mnacharuka miongoni mwa mabuu wote kutafuta mahali salama, mkijaribu kuwameza mabuu walio wadogo kuwaliko ninyi. Ninyi ni wenye kijicho na wa husuda katika mioyo yenu, kuwashinda wale pepo ambao wamezama chini ya bahari. Mnaishi chini ya samadi, mkiwasumbua mabuu kutoka juu hadi chini ili wasiwe na amani, mkipigana wenyewe kwa wenyewe kwa muda mfupi na kisha kutulia. Ninyi hamjui hali yenu wenyewe, ilhali bado ninyi hupigana wenyewe kwa wenyewe ndani ya samadi. Ni nini ambacho mnaweza kupata kutokana na mapambano hayo? Kama ninyi kweli mngekuwa na moyo wa kunicha Mimi, mngewezaje kupigana wenyewe kwa wenyewe bila Mimi kujua? Haijalishi vile hali yako ilivyo juu, je, bado wewe si mnyoo mdogo mwenye uvundo ndani ya samadi? Utaweza kuota mbawa na kuwa njiwa angani?” (“Majani Yaangukayo Yatakaporudi kwa Mizizi Yake Utajuta Maovu Yote Ambayo Umefanya” katika Neno Laonekana katika Mwili). Kila neno la hukumu ya Mungu lilinidunga kwa uchungu ndani ya moyo wangu kama upanga mkali, likichangamsha roho yangu na kunifanya kutambua kwamba nilitekeleza wajibu wangu sio ili kumtukuza Mungu na kumshuhudia, lakini kwa sababu daima nilitaka kujionyesha, kujishuhudia mwenyewe, na nilikuwa na ndoto ya kuwa bora kuliko watu ili waweze kunienzi na kuniheshimu. Kulikuwa na uchaji wowote wa Mungu ndani ya moyo wangu? Nilichofuatilia hakikuwa sawa na kile cha malaika mkuu aliyemsaliti Mungu? Mimi ni kiumbe kilichoumbwa kilichopotoshwa kabisa na Shetani. Mbele ya Mungu, mimi ni kama uchafu, funza. Ninatakiwa kuwa ninamwabudu Mungu na kutimiza wajibu wangu nikiwa na uchaji moyoni mwangu wakati wote, lakini sikushughulika na kazi ya uaminifu, na nilitaka daima kutumia kutekeleza wajibu wangu kama fursa ya kujionyesha na kujishuhudia mwenyewe. Mungu angewezaje kutochukia na kusinywa na haya? Mungu ni mtakatifu sana na mkuu, amejaa mamlaka na uongozi, na bado anabaki kuwa mnyenyekevu na kujisetiri, hafichui utambulisho Wake kamwe ili kuwafanya watu kumtazamia na kumstahi. Badala yake, Anaendelea kwa ukimya kujitolea Kwake kote ili kuwaokoa wanadamu, kamwe hajitetei Mwenyewe au kudai sifa njema, na kamwe hadai chochote kutoka kwa wanadamu. Unyenyekevu, uadilifu, na kutokuwa na ubinafsi kwa Mungu kulinifanya nione kiburi, kuwa duni, na ubinafsi wangu, sikuwa na budi ila kuhisi aibu, kana kwamba sikuwa na mahali pa kujificha, na nilihisi kwamba nilikuwa nimepotoshwa sana na Shetani na nilihitaji sana wokovu wa hukumu, adabu, jaribio na usafishaji wa Mungu. Kwa hivyo nilianguka tena mbele ya Mungu: “Ewe, Mwenyezi Mungu! Kupitia uadibu na hukumu Yako ninaweza kuona uasi wangu , pamoja na uadilifu Wako na ukuu. Kuanzia sasa kuendelea, wakati ninapotekeleza wajibu wangu ninatumaini tu kutenda kama mwanadamu wa adabu aliye na moyo unaokuogopa Wewe, na kutupa tabia yangu ya kishetani kwa kutegemea maneno Yako.”
Baada ya kupitia adabu na hukumu ya Mungu mara kwa mara tena, maoni yangu juu ya ufuatiliaji yamebadilika hatua kwa hatua, lakini tabia ya maisha yangu haikuwa bado imepata mabadiliko kweli. Ili kunitakasa kabisa zaidi na kunisababisha kutembea kwenye njia ya sahihi ya uzima, Mungu mara nyingine tena alinipa wokovu Wake. Baadaye, nilichaguliwa kuwa kiongozi wa kanisa, nikishirikiana na dada mwingine kutekeleza wajibu wetu. Kutokana na kushindwa kwangu kwa awali, niliendelea kujikumbusha kila wakati kwamba nilihitaji kukubaliana na dada huyo ili kufanya kazi ya kanisa vizuri. Mwanzoni, ningekuwa nikijadili kila kitu na dada huyo na kufuatilia mwongozo wa Mungu pamoja, kwa hivyo tulifanikisha matokeo katika vipengele vyote vya kazi. Lakini baada ya muda fulani, niligundua kuwa dada huyo alikuwa na tabia nzuri za asili, mawasiliano yake ya ukweli yalikuwa wazi na ya kuangaza, na uwezo wake wa kikazi ulikuwa sawa kuliko wangu. Wakati wa mikutano, ndugu walikuwa wote radhi kusikiliza mawasiliano yake na wote walitafuta ushauri wake walipopatwa na shida. Nilipokabiliwa na mazingira kama hayo, nilikuwa tena nimetegwa katika mtego wa Shetani na kupumbazwa nayo: Dada huyo ni bora zaidi kuliko mimi kwa kila namna na anapendwa na ndugu bila kujali mahali anaenda. Hapana! Ni lazima nimpite kwa vyovyote vile, na niache ndugu waone kwamba mimi niko chini yake. Kwa sababu hii, nilijishughulisha kanisani kila siku mtawalia, nikipanga mikutano ya ndugu na haijalishi ni nani aliyepata matatizo ningekimbia kwao kuwasaidia kutatua suala hilo. … Inawezekana kuwa nilionekana kuwa mwaminifu na mtiifu kutoka nje, lakini malengo yangu ya ndani ingewezaje kuepuka macho ya Mungu? Uasi wangu ulifufua hasira ya Mungu, na kama matokeo nilianguka katika giza. Sikupata nuru niliposoma maneno ya Mungu, sikuwa na cha kusema wakati wa kuomba, niliwasiliana bila kusisimua wakati wa mikutano, na hata niliogopa mikutano na ndugu zangu. Nilikuwa nimefungwa kabisa na heshima na hadhi. Nilipitia kila siku bila kidokezo, ni kama nilikuwa nimebeba mzigo mkubwa mgongoni mwangu na singeweza kupumua kutokana na kubanwa. Singeweza pia kubaini tena baadhi ya masuala ya kanisa, na utendaji bora wangu wa kazi yangu ukashuka kwa kasi. Nilipokabiliwa na ufunuo kama huo kutoka kwa Mungu, sikujaribu kujijua na pia sikuwa radhi kuzungumza kwa nyofu kwa ndugu kuhusu hali yangu na kutafuta ukweli ili kuutatua, kwa hofu kuwa wangenidharau. Baadaye, kuadibu na nidhamu ya Mungu ikaniangukia. Tumbo yangu ilianza kwa ghafla kuniuma sana hadi singeweza kukaa au kusimama kwa amani. Mateso ya magonjwa na kutoridhika kutokana na kutopata hadhi kuliniacha nikizungukazunguka katikati ya maisha na kifo. Kutokana na kukataa kwangu kuyakubali matatizo yangu na kushindwa kwangu kushirikiana kwa kazi ya kanisa, kanisa halikuwa na budi ila kunibadilisha na kunituma nyumbani ili ibada ya kiroho na kujitafakari. Baada ya kupoteza hadhi yangu, nilihisi kama nilikuwa nimehukumiwa jehanamu. Kihisia, nilizama hadi katika kiwango changu cha chini kabisa na kuhisi kuwa nilikuwa nimeaibika kabisa. Niliteseka hata zaidi ndani hasa wakati nilipowaona ndugu wote wakitekeleza kikamilifu wajibu wao, wakati nilikuwa nimepoteza kazi ya Roho Mtakatifu na sikuwa na uwezo wa kutekeleza wajibu wowote. Kwa uchungu, sikuweza kujisaidia ila kujiuliza: Mbona kuna wengine wanaamini Mungu na wanaelewa ukweli zaidi na zaidi, ilhali ninaendelea kumuasi na kumpinga Mungu mara kwa mara tena kwa sababu ya heshima na hadhi? Nilimsihi Mungu mara nyingi anielekeze nipate chanzo cha kufeli kwangu. Siku moja, niliona yafuatayo kati ya maneno ya Mungu: “Watu wengine hususan humpenda Paulo sana: Wanapenda kuhutubu na kufanya kazi nje. Wanapenda kukutana pamoja; wanapenda watu wanapowasikiliza, kuwaabudu, na kuwazingira. Wanapenda kuwa na hadhi katika mawazo ya watu wengine na kufurahia wakati wengine wanathamini mfano wao. Hebu tuchanganue asili yao kutoka kwa tabia hizi: Je, mtu wa aina hii aliye na tabia hiziana asili ya aina gani? Kama kweli anatenda kwa njia hii, basi hilo linatosha kuonyesha kuwa yeye ni fidhuli na mwenye majivuno. Yeye hamwabudu Mungu kamwe; yeye hutafuta hadhi ya juu, na anataka kuwa na mamlaka juu ya wengine, kuwakalia, kuwa na hadhi akilini mwao. Kinachojitokeza kuhusu tabia yake ni ufidhuli na majivuno, kutokuwa radhi kumwabudu Mungu, na tamaa ya kuwaabudu wengine. Huu ni mfano bora wa Shetani” (“Jinsi ya Kujua Asili ya Mwanadamu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Kwa kuongezea, inasema katika “Mahubiri na Ushirika kuhusu Kuingia Katika Maisha”: “Kiini na asili ya Shetani ni usaliti. alimsaliti Mungu tangu mwanzo kabisa, na baada ya kumsaliti Mungu alidanganya, akapotosha, akachezea, na akatawala wanadamu duniani walioumbwa na Mungu, akijaribu kuwa sawa na Mungu kama na kuanzisha ufalme tofauti. … Unaona, asili ya Shetani sio ile inayosaliti Mungu? Kutoka kwa yote ambayo Shetani amefanyia wanadamu, tunaweza kuona wazi kwamba Shetani ni kwa kweli pepo mbaya anayepinga Mungu na kwamba asili ya Shetani ni ile inayomsaliti Mungu. Haya yote ni kamili” (“Jinsi ya Kupata Ujuzi wa Asili Yako Potovu” katika Mahubiri na Ushirika juu ya Kuingia Katika Maisha I). Nikizingatia haya maneno, singeweza kujizuia kutetemeka na hofu. Niliona kwamba yale niliyoyaishi kwa kudhihirisha yalikuwa kwa sura ya Shetani kabisa, na nilikuwa mwenye kiburi na mwenye majivuno, na asiyemwabudu Mungu hata kidogo. Mungu aliniinua ili nitekeleze wajibu wangu kanisani, ili nipate kuwaleta ndugu mbele za Mungu nikiwa na uchaji Kwake moyoni mwangu, na kuwafanya watu wawe na nafasi ya Mungu katika mioyo yao, na pia kuwa na uchaji na kumtii Mungu. Lakini nilipokabiliwa na kuinuliwa na Mungu, sikutia maanani nia ya Mungu katika kutekeleza wajibu wangu, na sikuhisi mzigo kuwasaidia ndugu kuingia katika maisha. Badala yake, nilitaka kila mara kuwafanya watu waniangalie kwa makini na kunisikiliza, na kwa ajili ya matamanio yangu, nilijaribu kila mara kujiinua bila kujalisha popote nilipoenda. Nilikuwa hata mwenye wivu kwa waliokuwa wazuri na mwenye husuda kwa wakakamavu, na nilishindana kwa ukaidi na wengine kwa ajili ya ukuu. Kutoka nje, nilikuwa ninashindana na wanadamu, lakini kwa kweli nilikuwa nikipigana dhidi ya Mungu. Hili ni jambo ambalo huudhi sana tabia ya Mungu. Alinihukumu na kuniadibu, kunirudia na kunifundisha nidhamu, na kuninyang’anya hadhi ili kunifanya nijitafakari na kutubu. Niliona kwamba mapenzi ya Mungu kwangu yalikuwa ya kina sana na makubwa sana! Singeweza kujizuia kuhisi majuto na kujilaumu ndani, na hata zaidi nilichukia ya kwamba upotovu wangu ulikuwa wa kina sana. Nilifuata Mungu lakini sikufuatilia ukweli, na badala yake nilifanya kazi kwa bidii bila kufikiri tu kwa sababu ya hadhi na heshima. Nilikuwa nimeshindwa kabisa kuishi kulingana na mapenzi na wokovu wa Mungu. Kadri nilivyojichungua, ndivyo nilivyoona wazi zaidi kuwa misemo niliyoishi kulingana nayo, kama vile “Kama vile mti huishi kwa sababu ya ganda lake, mtu huishi kwa sababu ya uso wake,” na “Mtu huacha jina lake nyuma popote akaapo, kama vile bata bukini hutetea popote arukapo,” yalikuwa uongo yaliyotumiwa na Shetani ili kuwapotosha na kuwadhuru wanadamu. Nilitambua kwamba Shetani alitumia mambo haya kuduwaza nafsi za watu, kupotosha mawazo yao, na kuwafanya kukuza mitazamo mbaya kuhusu maisha, kuwafanya wajitahidi kwa vyovyote vile kufuatilia vitu bure kama vile hadhi, umaarufu, utajiri na heshima, na hatimaye kupotea kutoka kwa na kumsaliti Mungu, ili waweze wote kuzingatia uwongo wake na kuifanyia kazi na kuangamizwa na kudhuruiwa kwa hiari. Nilikuwa mmoja wa watu hao ambao walikuza mtazamo mbaya wa maisha kwa msingi wa udanganyifu wa Shetani, nikawa mwenye kiburi, majivuno, dharau, na asiyekuwa na mahali pa Mungu moyoni mwangu. Niliishi katika upotovu na kumtendea Mungu kama adui. Sasa, sipaswi tena kuenda kinyume na Mungu wakati ninafurahia rehema Yake. Nitajirekebisha kabisa, nitaacha Shetani kabisa, nitampa Mungu moyo wangu kabisa, na kuishi kwa kudhihirisha mtu wa kweli ili kufariji moyo wa Mungu. Baada ya hapo, nilitaka kujua jinsi ya kuendelea na njia yangu ya baadaye, na jinsi ya kufuatilia ukweli ili kukidhi mapenzi ya Mungu. Asante kwa Mungu kwa kuniongoza tena. Kisha niliona maneno ya Mungu: “Leo, hata kama wewe si mfanyikazi, unapaswa kuwa na uwezo wa kutekeleza wajibu wa kiumbe wa Mungu, na kutafuta kujiwasilisha kwa mipango yote ya Mungu. Unapaswa kuwa na uwezo wa kutii chochote Mungu anachosema, na upitie kila aina ya madhila na usafishaji, na ingawa wewe ni dhaifu, moyoni mwako unapaswa bado uwe na uwezo wa kumpenda Mungu. Wale ambao huchukua jukumu katika maisha yao wako tayari kutekeleza wajibu wa kiumbe wa Mungu, na mtazamo wa watu kama hawa kuhusu harakati ni ule sahihi. Hawa ndio watu ambao Mungu anahitaji. … Kama kiumbe wa Mungu, mwanadamu anapaswa kutafuta kutekeleza wajibu wa kiumbe wa Mungu, na kutafuta kumpenda Mungu bila kufanya chaguo lingine kwa kuwa Mungu anastahiki upendo wa mwanadamu. Wale ambao wanatafuta kumpenda Mungu hawapaswi kutafuta faida zozote za kibinafsi au lile ambalo wanatamani binafsi; hii ndiyo njia sahihi kabisa ya ufuatiliaji” (“Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea” katika Neno Laonekana katika Mwili). Kama kioleza, maneno ya Mungu yalinipa nuru moyoni mwangu, yakinionyesha njia ambayo ninapaswa kuchukua. Mungu anatarajia kuwa watu, bila kujali kama wana hadhi na wamefikwa na hali gani, wanaweza kufanya kila wawezavyo kufuatilia ukweli, na wanaweza kutii upangaji na utaratibu wa Mungu na kutafuta kupenda na kumtosheleza Mungu. Hii ndiyo njia sahihi zaidi ya ufuatiliaji na pia ni njia ya ukweli ya uzima ambayo kiumbe kilichoumbwa kinapaswa kupitia. Hivyo basi niliamua mbele ya Mungu: Ee Mungu, asante kwa kunionyeshea njia ya ukweli ya uzima. Hadhi yangu ya awali ilikuwa kutokana na kuinuliwa na Wewe. Kutokuwa na hadhi leo pia ni kwa sababu ya haki Yako. Mimi ni kiumbe kidogo tu kilichoumbwa. Kuanzia sasa kuendelea, ninataka tu kufuatilia ukweli na kutii mipango Yako yote.
Baadaye, hali yangu ikarudi kawaida haraka kutokana na kusoma maneno ya Mungu na kuishi maisha ya kanisa. Kanisa tena lilinipangia kazi linalonifaa. Pia, nilizingatia kufuatilia ukweli katika kutekeleza wajibu wangu, wakati wowote kitu kilifanyika ningetafuta nia ya Mungu, ningejaribu kujijua mwenyewe, na kupata maneno yanayoambatana na ya Mungu ili kukitatua. Nilipokabiliwa na vitu vilivyohusisha heshima na hadhi, hata ingawa ningekuwa na mawazo fulani katika akili yangu, kwa kupitia maombi na neno la Mungu ningetafuta ukweli na kujitelekeza mwenyewe, na polepole niliweza kuwa na uwezo wa kutodhibitiwa na mambo haya na ningetekeleza wajibu wangu nikiwa na utulivu wa akili. Wakati niliona baadhi ya ndugu ambao hawakuwa wamemwamini Mungu kwa muda mrefu kama mimi wakiaminishwa na agizo, ningeweza, kwa kutafuta ukweli, kuelewa kwamba wajibu ambao unatekelezwa na mtu umejaaliwa na Mungu, na kwamba ninapaswa kutii mipango ya Mungu. Matokeo yake yakawa, niliweza kuwa na uwezo wa kuichukulia kwa njia sawa. Wakati ndugu walinishughulikia na kufichua asili yangu na kiini, ingawa nilihisi nimepoteza heshima, niliweza kuwa mtiifu kutumia sala. Hii ni kwa sababu upendo wa Mungu umeniangukia, na umefaidika sana katika kubadilisha tabia yangu ya maisha. Hapo awali, nilitia maanani katika heshima yangu sana kupindukia na sikuwa radhi kufichulia yeyote, kwa hofu kwamba wengine wangenidharau. Sasa, ninafanya mazoezi ya kuwa mtu mwaminifu kwa mujibu wa mahitaji ya Mungu, na kama nina shida yoyote nitafungua roho yangu kwa ndugu, jambo ambalo hunifanya kuhisi hasa nimefarijika na mwenye furaha katika kina cha roho yangu. Nikiyaona haya mabadiliko ndani yangu, singeweza kujisaidia ila kumshukuru na kumsifu Mungu, kwa maana mabadiliko haya yanaletwa kwangu na kazi ya adabu na hukumu ya Mungu ya siku za mwisho.
Nimemfuata Mwenyezi Mungu kwa miaka kadhaa sasa. Nikifikiria awali, ilikuwa ni sumu za Shetani ambazo zilikuwa zimemomonyoa nafsi yangu. Nilikuwa nimeishi chini ya miliki ya Shetani na niliangamizwa na kupumbazwa naye kwa miaka mingi. Sikujua thamani na maana ya maisha. Sikuweza kuona mwanga, wala sikuweza kupata furaha ya ukweli na shangwe. Nilizama katika dimbwi la simanzi na sikuweza kujinasua. Sasa, ni kupitia adhabu na hukumu ya mara kwa mara niliweza kuachana na madhara ya Shetani na kufikia faraja na uhuru. Nimepata tena dhamiri na mantiki yangu, na pia nina lengo sahihi la kufuatilia, kufuata Mungu katika njia ya ukweli na yenye kung’aa ya uzima. Kupitia adabu na hukumu ya Mungu, kwa kweli nilipitia upendo wa Mungu usio na ubinafsi na wa kweli, na kufurahia baraka na kupokea upendo ambao ulimwengu wa mwanadamu hauwezi kufurahia. Ni Mungu pekee anayeweza kumwokoa mwanadamu kutokana na bahari ya mateso ya Shetani, na ni kazi ya adabu na hukumu tu ya Mungu inayoweza kuwatakasa wanadamu kutokana na sumu za Shetani ndani yao na kuwafanya waishi kulingana na mfano wa mtu wa kweli na watembee katika njia ya ukweli ya uzima. Adabu na hukumu ya Mungu ni nuru. Ni rehema kubwa kabisa, ulinzi bora kabisa, na utajiri wenye thamani zaidi ya maisha ambayo Mungu amewapa watu. Kama vile maneno ya Mwenyezi Mungu yanasema: “… adabu na hukumu ya Mungu ndio uliokuwa ulinzi bora zaidi wa mwanadamu na neema kubwa. Ni kwa njia ya adabu na hukumu ya Mungu ndipo mwanadamu angeweza kugutuka, na kuchukia mwili, na kumchukia Shetani. Nidhamu kali ya Mungu inamweka huru kutokana na ushawishi wa Shetani, inamweka huru kutokana na dunia yake ndogo, na inamruhusu kuishi katika mwanga wa uwepo wa Mungu. Hakuna wokovu bora zaidi kuliko adabu na hukumu!” (“Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Asante kwa adhabu na hukumu ya Mungu kwa kuniokoa na kuniruhusu kuzaliwa upya! Katika njia yangu ya baadaye ya kumwamini Mungu, nitajizatiti kufuatilia ukweli, kupokea zaidi adhabu na hukumu zaidi ya Mungu, na kutoa kabisa sumu za Shetani ili kupata utakaso, kupata ujuzi wa kweli wa Mungu, na kuwa mtu ambaye kwa kweli anampenda Mungu. Utukufu wote uwe kwa Mungu. Amina!
Tanbihi:
a. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.
Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo